SUMU YA UCHUMBA NA NDOA
*💍SUMU INAYOUA UCHUMBA NA NDOA 🌹🌹*
Mwlm. Peter Francis Masanja
francispeter424@gmail.com
0679392829
The Voice of God ministry
_💫BWANA YESU ASIFIWE_
✍🏻leo napenda tuangalie sumu inayoua uchumba au ndoa
💫Unaweza pia ukaliita hilo somo adui wa uchumba na ndoa .
Inawezekana ulimpata mchumba mkakaa naye vizuri kabisa lakini ikaja ikatokea mumeachana na kila mtu kumsahau mwenzake
✍🏻Lakini leo nataka tuangalie sumu kuu inayoua au kuvunja uchumba au ndoa .
💫Zifuatazo ni sumu zinazopelekea uchumba au ndoa kuvunjika .
*1⃣ KUKOSA MAOMBI*
💻📖 1 Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
Zaburi 127 :1
💫Kuna wakati watu hujisahau na kuacha kuombea uchumba au ndoa zao
Hii humfanya shetani aingie kwa kasi na kuhakikisha uchumba unavunjika au ndoa inakosa amani kwa sababu hakuna ulinzi wa Mungu
💫Maombi ni muhimu sana katika uchumba au ndoa
💫Uchumba au ndoa ikikosa maombi ni sumu kubwa sana inayopelekea mpasuko katika eneo hili
💫Omba ulinzi ili Mungu alinde ndoa yako au uchumba wako
*2⃣ KUJIKUSANYIA MARAFIKI WENGI*
💻📖 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
Mithali 18:24
💫Sisemi kwamba kuwa na marafiki ni vibaya , hapana lakini usimwamini rafiki mpaka aingilie himaya yako ya uchumba au ndoa ni sumu kali sana
💫Rafiki anaweza kuwa kilio kwenye mahusiano yenu tena kilio kikubwa sana.
💫 Katika marafiki kuna aina fulani ya marafiki wao ndyo wanaunda kamati na kuulizana fulani kaoa mke gani huyu mbona hana hata mvuto ❓
💫Au watakwambia yule mchumba uliye naye hakufai na sababu yao kuu hawavutii yaani siyo mzuri
Hii itaua uchumba ukisikiliza maneno yao na kuyasikia.
💫Wapo pia marafiki zako ambao wanania muachane na mtu wako ili wao wammiliki
Watakachokifanya ni kupeleka taarifa za uongo kwa mwenzako ili achukia na kuchukua uamzi wa kuvunja uchumba
📖💻 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Zaburi 1 :1
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
Zaburi 1 :2
💫Na kuna wakati uliona binti ukataka kuanzisha naye mahusiano lakini akakurupuka ukamwambia rafiki yako akakwambia achana naye anasura mbaya ,
Huko ni kumkosea Mungu
💫Maamuzi ya nani awe wako usiamliwe na marafiki zako kwa kukuletea sababu za kimaumbile
Mara mfupi , mweusi mno , mnene mno , mwembamba mno
Hizi ni sababu zilizokufa na ukizisikiliza huwezi oa na ukioa utaishia kukosea .
*3⃣ MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII*
💫Hii pia inaharibu mahusiano mengi
💫Najua ni vizuri kuposti picha kwenye mitandao lakini inategemea ni picha za aina gani
💫Siyo kila zina maadili zingine huketa mtafaruku na mitazamo hasi kwa watu
💫Maisha ya uchumba na ndoa yawe na mipaka katika eneo la mitandao
*4⃣ HABARI ZILIZOBEBA MITAZAMO MIBAYA KATIKA UCHUMBA NA NDOA*
💫Wanasema kwamba vijana wengi siyo waaminifu wanachezea na kuacha
💫ni kweli kuna vijana wanachezea na kuacha
💫Na kama wanachezea na kuacha mchezewa kwanini uruhusu kuchezewa ❓
💫Huwezi kusema umechezewa kama ulilazimishwa wakati ulikubali mwenyewe kabisa
💫Naomba niseme hivi usiingie kwenye mahusiano ukisema ikitokea tumeachana itakuwaje
💫Kuachana ni matokeo kwahiyo usiyatazamie ya kuachana mtazame Mungu asimame juu ya uhusiano wenu
💫Kuna wakati umeachika katika uchumba kumbe Mungu amekuepusha na shida katika maisha yako.
💫Usiingie kwenye mahusiano kama unamashaka Mungu hatasimama katika uhusiano wenu .
💻📖 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka.
Mathayo 21:21
💫Kuingia kwenye mahusiano na mashaka ni sumu kali sana inayoweza kuvunja uchumba au ndoa
Itaendelea
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni