URAFIKI,UCHUMBA NA NDOA
*🌹🌹MFANYE AWE WAKO PEKE YAKO TU👫😘*
Mwl.Peter Francis Masanja
The Voice of God Ministry
0679392829
🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹
Bwana Yesu asifiwe
🌹kuna mwimbaji aliimba tumeagizwa upendo
🌹mwimbaji huyo hajakosea kabisa.
🌹👫 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Waefeso 5 :25
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
Waefeso 5 :26
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Waefeso 5 :27
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Waefeso 5 :28
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
Waefeso 5 :29
🌹Mwanamke anahitaji kuonyeshwa upendo.
🌹Mwanamke anahitaji kusifiwa .
👉Msifu mkeo mwambie ni mzuri unafrahi ukimwona .
👉Mwambie yeye ni mzuri kuliko wanawake wote duniani .
🌹👫 29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
Mithali 31 :29
👉Msifu mkeo ili akufrahie.
🌹Mwite majina matamu huku ukimwambia unampenda sana na kumwaminisha kuwa yeye ni wa thamani sana maishani mwako.
Mfano :
Mpenzi , wewe ni wa thamani sana maishani mwangu , nikikukumbuka huko kazini natabasamu tu , uzuri wako wanifanya nizidi kukuona mpya kila iitwapo leo , nakupendaa baby .
🌹Mwanamke anapenda kiss ( busu )
👉Jitahidi kumpatia kiss mkeo siyo mpaka akwambie unaweza kumfanyia kama surprise huku unaonyesha tabasamu .
Hapo ndoa yako au uchumba wako utadumu sana.
🌹Kuwa na mazoea ya kukaa na mke wako siti moja au kaa karibu naye ongea naye na ikibidi mshike mkono , mtizame hata usoni.
Hii humfanya mwanamke akufrahie sana .
🌹Uwe na mazoea ya kumkumbatia mkeo huku ukisema wampenda .
🌹Mfanye mkeo acheke , mwanamke anahitaji kuchekeshwa , yaani utani huku ukimsifu ikibidi mshikeshike nywele zake.
🌹Cheza na mkeo , na wakati mwingine mbebe 👫
🌹👫 Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani,
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
*akamwona Isaka anacheza-cheza na Rebeka mkewe.*
Mwanzo 26:8
👉Shetani hupiga vita ndoa za waliookoka , kwahyo msipokaa vizuri kwenye maombi hayo hutokea .
✍🏻✍🏻 4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
Ufunuo wa Yohana 2 :4
5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
Ufunuo wa Yohana 2 :5
🌹Mke mjue anapendelea nini au anavaa size gani nguo za ndani 👙
Anavaa kiatu namba ngapi 👠
✍🏻hivyo vitu mletee hivi vitu kama surprise.
🌹Usisubiri eti akwambie , hata kama anauwezo wa kujinunulia nguo mletee atakuona wewe unampenda na kumjali sana.
👉Tatizo mnashindwa kuwasoma wake zenu wanapenda nini hii itawaumiza
👉Mwanaume hujui hata mkeo anavaa chupi namba ngapi kazi kumfunua tu 😨😨😨
✍🏻Unashindwa kujua mkeo anavaa size gani kiunoni mmmmh aiseeee ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
👉Umejua anapendelea rangi gani ❓👫🌹🌹
📖💻 2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao,
.✍🏻📖 *wasio na shukrani* ,
wasio safi,
2 Timotheo 3 :2
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
2 Timotheo 3 :3
4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
2 Timotheo 3 :4
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
2 Timotheo 3 :5
🌹mke asiye na shukurani huyo siyo mke anaweza kuwanyima chakula hata ndugu zako .
🌹Mwachie mkeo pesa ya matumizi
👉Hii pia humfanya mke atulie kwako daima
👉Haijalishi mkeo anakazi wewe acha hela ya matumizi
✍🏻kuna vitu vingne mletee bila yeye kumtaarifu ,
👉Af ndoa ni tamu mkiwa mnacheka na mkeo.
Ubarikiwe sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni