USIOGOPE WINGI WALA UKUBWA WA ADUI
💫USIOPE UKUBWA WALA WINGI WA ADUI ZAKO 🔥
Mlm.Peter Francis Masanja
francispeter424@gmail.com
0679392829
The Voice of God Ministry
Bwana Yesu asifiwe
✍🏻 Siku ya leo nataka tujifunze kuhusu kujiamini kuwa wewe ni mshindi ukiwa unamtegemea Mungu na kuamini kuwa yeye anamiliki na kutawala pia .
📖📖 Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.
Zaburi 6:10
Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.
Zaburi 18:3
👉 Japokuwa kuna adui wengi wanakufuatia ujue kuwa Mungu atawaaibisha mbele zako.
Usione ni wengi mbele za Mungu ni wachache sana .
👉 Kuna wakati ukiona adui wamekuandama unaogopa sana lakini nataka nikwambie kuwa usiogope mtukuze Mungu naye atasimama upande wako na atakupa namna ya kuwapiga adui zako .
📖📖 2 Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi).
2 Mambo ya Nyakati 20 :2
3 Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.
2 Mambo ya Nyakati 20 :3
4 Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute Bwana; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta Bwana.
2 Mambo ya Nyakati 20 :4
5 Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa Bwana, mbele ya ua mpya;
2 Mambo ya Nyakati 20 :5
6 akasema, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.
2 Mambo ya Nyakati 20 :6
7 Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele?
2 Mambo ya Nyakati 20 :7
12 Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yatazama kwako.
2 Mambo ya Nyakati 20 :12
13 Wakasimama Yuda wote mbele za Bwana, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.
2 Mambo ya Nyakati 20 :13
14 Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya Bwana, katikati ya kusanyiko;
2 Mambo ya Nyakati 20 :14
15 akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 20 :15
16 Kesho shukeni juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli.
2 Mambo ya Nyakati 20 :16
17 Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi.
2 Mambo ya Nyakati 20 :17
18 Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana.
2 Mambo ya Nyakati 20 :18
19 Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.
2 Mambo ya Nyakati 20 :19
20 Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
2 Mambo ya Nyakati 20 :20
21 Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Mambo ya Nyakati 20 :21
22 Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa.
2 Mambo ya Nyakati 20 :22
23 Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe.
2 Mambo ya Nyakati 20 :23
24 Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka.
2 Mambo ya Nyakati 20 :24
25 Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
2 Mambo ya Nyakati 20 :25
26 Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia Bwana; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
2 Mambo ya Nyakati 20 :26
27 Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya adui zao.
2 Mambo ya Nyakati 20 :27
👉Usiogope wingi wa adui mwite Mungu mtetezi wako aliye hai milele atakuokoa na adui zako atawakatilia mbali .
📖 4 Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja.
1 Samweli 17 :4
5 Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba.
1 Samweli 17 :5
6 Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake.
1 Samweli 17 :6
7 Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
1 Samweli 17 :7
8 Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
1 Samweli 17 :8
9 Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia.
1 Samweli 17 :9
37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe.
1 Samweli 17 :37
43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.
1 Samweli 17 :43
44 Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.
1 Samweli 17 :44
45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
1 Samweli 17 :45
💫Daudi alikuwa mdogo sana kwa Goliath lakini hakuangalia ukubwa na vitisho vyake bali alimwangalia Mungu .
Mungu alionyesha ukuu wake kwa Daudi kuwa yeye ni mweza wa mambo yote.
Adui zako ijapokuwa ni wengi mbele za Mungu ni wachache sana. Mwite Mungu atakupigania hyo vita uliyonayo ni vita ya Mungu maana yeye ni adui wa adui zako .
Unasemwa vibaya na watu yafute maneno yao songa mbele nao watakuona ukiwa viwango vya juu sana.
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni