WITO NA UTUMISHI
SOMO: WITO NA UTUMISHI
ANDIKO KUU;-
MATENDO 13:2-3 “…..nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia”
🎤📖Maisha ya Binadamu hayatakuwa na matokeo makamilifu mpaka siku atayogundua Wito wake. Kwanini Mungu alikuumba ? Kwanini upo Duniani ?.
🎤📖Kuna aina nyingi za wito, lakini nataka nizungumzie Wito wa Utumishi. Wito hautegemei elimu, fedha, muonekano ,umasikini. Wito ni wewe
🎤👉Maana Ya Wito nini
🎤📖Wito ni kitendo cha KUMSIKIA Mungu akitoa majukumu ya utumishi wako
👉SomaYEREMIA 1:5, ISAYA 42:6-7
🎤👉Dhumuni la Wito nini?
🎤📖Dhumuni la kuitwa ni Mungu anataka jambo litendeke kwa kupitia wewe, kwahiyo wewe unakuwa ni chombo, kazi yako ni kutii na kutenda.
👉SomaYEREMIA 51:20-23
👉) Naanzanje safari yangu ya wito au utumishi?
👉Mambo mawili ya msingi katika mwanzo wa mchakato huu
(1) Amini injili (2) Pokea zawadi( Roho Mt)
🎤📖INJILI- Ni habari njema za Yesu kuhusu msamaha kamili wa dhambi zote, injili ina habari nne kuu;- Maji, Damu, Mwili na Msalaba.
👉Soma RUMI 1:1
👉Unaiamini Injili kwa kuliamini JINA LA YESU
👉Soma Mdo 4:12, 16:31
🎤📖ROHO MTAKATIFU – Ni zawadi pekee, ni ahadi pekee ya Mungu kwa anaeiamini injili. Huwa anatoa hii zawadi kwa kupitia watumishi aliowatia muhuri. Hakikisha unakuwa na Roho Mt, sio hisia-hisia.
👉Soma vifungu hivi MATENDO 2:38-39,5:32, YOEL 2:32, ISAYA 44:3, YEREMIA 36:27
👉Mungu anamuitaje mtu kuwa mtumishi.
👉Ingawa Mungu huwa anaita watu kwa namna tofauti lakini anatumia njia moja ya mawasiliano kwa kila muitwaji.
👉🎤Mungu huwasiliana na mwanadamu kwa njia ya sita ya ufahamu ya mtu(fourth dimension), namaanisha Mungu hutumia MAONO, NDOTO, MASIKIO YA NDANI, MACHO YA NDANI.
🎤Mungu ni Roho, huwa anapenda kuongea na roho aliyompa mwanadamu kwa njia ya Yesu na kupita Roho Mt.
👉SomaWAEBRANIA 1:1-2, na YOHANA 10:4,16,27.
👉Naomba nikwambie kwamba Mungu anataka kila mtu aweze kumsikia.
👉Utajuaje Wito wako ?
👉Wito wako ni lazima uanzie ndani, Mungu atakuambia wito wako kwa kupitia MAONO
👉MDO 18:9), NDOTO(1Falme 3:5), KUSIKIA(1 Falme 19:13) NA KUONA KWA UTU WA NDANI(Ufu 1:12), hizi njia nne za mawasilia ninaziita kwa jina moja KUSIKIA au KUWA ROHONI(Ufu 1:10). Kwahiyo ili ujue wito wako utatakiwa USIKIE KWA BIDII. TORATI 28:1, YEREMIA 1:7,9-10.soma vzr hapa upaelewa.
👉🎤Baada ya kuwa UMESIKIA KWA BIDII wito wako, usikulupuke, subiri uthibitisho, Mungu atamtumia Mtumishi wake ( aliyeamini injili na kupokea Roho Mt)aje akuthibitishie huo wito wako, au ataongea na wewe kwa mara ya pili, mpaka mara ya tatu.
👉SomaMATENDO 9:17-18, na 1 SAM 3:8-9
🎤👉Kutokana na ulivyosikia, Mungu atatimiza kile alichokwambia, huwa analiangalia Neno lake, we anza huduma usiogope.
👉Soma ISAYA 55:11.
👉Mungu atatuma watumishi kwa ajili yako
👉Soma Mdo 18:26.
👉Unajiuliza Sina Pesa,nitaanzaje huduma ? –
👉Soma WALAWI 10:13
👉Wito ni tofauti kwa watumishi lakini misingi ya utumishi ni sawa.
a)Misingi Miwili ya Utumishi sahihi;--
👉Soma MDO 2:3
👉Misingi hii ni (1) Injili na (2) Kutoa vipawa.
👉Soma WAEBRANIA 8:3
👉Kila mtumishi wa kweli lazima awe nahii misingi, hii misingi ndiyo itakayokupa uelekeo wa wito wako ambao ni tofauti na mwingine.
👉Makuhani Agano la kale walikuwa na kazi kuu mbili, kufanya upatanisho na kutoa vipawa –
👉Soma WAEBRANIA 8:3.
👉Mtumishi wa Agano jipya anatakiwa kuhubiri ondoleo la dhambi kwa njia ya Yesu(Injili)
👉Soma MARKO 16:15
👉Na kuwezesha watu kupokea Roho Mt
👉Soma YOHANA 20:22
👉Tofauti za Utumishi
👉Kama uliamini Injili kwa usahihi, ukapokea zawadi kwa usahihi, Mungu hana ujanja, lazima akwambie kwa kupitia Simu yake Roho Mt eneo alilokuitia. Hapa sitaweza kueleza sana kwasababu hii ni siri kati yako na Roho wa Mungu.
👉Soma 1 KORINTHO 12:4-6, na WAKOLOSAI 1:26-27
👉Kipi Cha Kuzingatia
- Kama utumishi wako ulianza kwa KUSIKIA Roho Mt, utatakiwa kuendelea kusikia na kutii 100% unachoelekezwa na Roho Mt, hii ndio inaitwa Sabato. Mungu hataki wanaojitolea kumtumikia
👉Soma1 SAMWEL 16:1,
👉Anataka wanaoisikia sauti yake siku zote
👉Soma YEREMIA 18:1-2,
👉Kama Baba yako alikuteua au Jopo la maaskofu waliona unafaa – badili mtazamo.
🎤Nitamjuaje Mtumishi wa Kweli na Mshirika wa kweli? ,Rahisi mnoo
👉MTUMISHI ---
(1) Anahubiri Injili
.(2) Anatoa vipawa
👉MSHIRIKA ---
(1)Anaamini Injili
(2) Anapokea Vipawa
👉Kigezo cha VIPAWA kinasaidia kuvumbua wale waliojiita, wanaosema watatumia elimu zao, kuna walioona maisha magumu wakaona utumishi unalipa. Mtu ambaye Mungu hajamuita hata afanyaje hawezi kuwapa watu zawadi au vipawa ( Roho Mt)
👉Kuna Watumishi feki ?
- Ndiyo.
👉Ufeki wa watumishi upo wa aina mbili;
👉1) Mawakala wa shetani— siku zote wanaipinga Injili – wanapinga maji ya Yesu,damu ya Yesu,mwili wa Yesu na msalaba wa Yesu.
👉2) Watafuta pesa – Wanaikubali injili na wanaiamini, tatizo hawajaitwa, matokeo yake wanashindwa kutoa vipawa, mafundisho yao ni pesa, zaka ni amri, wanataka sana heshima, waitwe majina makubwa- baba askofu, watafanya juu chini waonekane njema, wao huwa hawatoi vipawa ni kupokea tu zaka na sadaka.-
👉Soma MATENDO 19:1-3,
👉Watumishi hawa mara nyingi wanatumia moto wa kigeni… sijui siku ya hukumu itakuwaje !!!!
👉Nimalizie kwa kusema
👉Kuna watu wengi walioanza utumishi bila kujua hizi kanuni, usijali, anza upya kwa kufuata utaratibu hapa chini ;
👉a) Tamani/omba Mungu akupe NENO-Isa 44:3, Math 7:11
👉 b) Tarajia KUSIKIA —Danieli 2:17-19, Habakuki 2:1-2
👉c) Amini(believe) utakayo YASIKIA —Mwanzo 15:6
👉d) Fanya(Faith)uliyo YASIKIA —Yohana 14:12
👉e) Kiri/tamka Imani yako —Warumi 10:10b
👉 f) Mungu atakutumia —Yeremia 1:12, Isaya 55:11
👉Mungu awabariki
Mtumishi
Elias Y.Mgallah.(0787402828)
Maoni
Chapisha Maoni