YESU NI MPATANISHI

*๐ŸŒนYESU NI MPATANISHI ๐ŸŒน*

18 March 2018




๐Ÿ“–๐Ÿ’ป 17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
Waebrania 2 :17

18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia watu wanaojaribiwa.
Waebrania 2 :18



๐Ÿ‘‰Mpatanishi ni yule anayesimama katikati ya watu wawili waliogombana.


๐Ÿ‘‰Ili uwepo lazima kuwe na msamaha kati ya pande mbili

๐Ÿ’ซKwanini Yesu awe mpatanishi ❓


๐Ÿ‘‰Tunakumbuka mwanadamu alifarakana na Mungu kwa kutenda dhambi .


๐Ÿ“–๐Ÿ’ป 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Mwanzo 3 :18

19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mwanzo 3 :19

๐Ÿ‘‰Mwanadamu alikuwa katika mafarakano na Mungu .


๐Ÿ‘‰Lakini Yesu alijitoa kama kuhani ili alete upatanisho kati ya Mungu na mwanadamu.


๐Ÿ‘‰Yesu alisimama katikati ya mwanadamu ili kuleta upatanisho.


๐Ÿ’ซIli upatane na Mungu lazima usamehe.


๐Ÿ’ป๐Ÿ“– 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

Mathayo 6 :12


๐Ÿ’ซBaada ya kusamehe patana .


๐Ÿ’ซOndoa habari mbaya ndani ya moyo wako ili upatane na Mungu.


๐Ÿ‘‰Maneno mabaya yanakutenga mbali na Mungu.


๐Ÿ’ซWaheshimu wanaokuongoza .

๐Ÿ“–๐Ÿ’ป Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

Waebrania 13:17



๐Ÿ’ซwaheshimu wazazi wako

1⃣Wazazi wa mwili
2⃣wazazi wa kiroho .
๐Ÿ’ป๐Ÿ“– Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

Kutoka 20:12




๐Ÿ’ซAcha manung'uniko.


๐Ÿ“–๐Ÿ’ป 1 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

Hesabu-Numbers 12 :1


๐Ÿ’ป๐Ÿ“– 2 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.

Hesabu-Numbers 14 :2


๐Ÿ’ซTupendane


๐Ÿ’ป๐Ÿ“– 1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

1 Wakorintho 13 :1

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

1 Wakorintho 13 :2

3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

1 Wakorintho 13 :3

4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

1 Wakorintho 13 :4

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
1 Wakorintho 13 :5

6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

1 Wakorintho 13 :6

7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

1 Wakorintho 13 :7

8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

1 Wakorintho 13 :8


๐Ÿ‘‰Upendo ukikosekana Mungu anakuwa mbali nasi .


Mungu akubariki



https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

๐Ÿ”ฐ MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA ๐Ÿ›*