BWANA AONGOZE HATUA ZAKO
🌐 BWANA AKUFUNDISHE NA AONGOZE HATUA ZAKO🌐
Mwlm.Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
💻 8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Zaburi 32 :8
💫 Uamkapo asbh hii kuelekea kazini , masomoni , na katika huduma , mwambie Mungu aongoze hatua zako
💫 Mwambie Mungu nifundishe na uniongoze katika kila jambo nilifanyalo kwa utukufu wako .
💫Mwambie Mungu aitazame kazi yako , ailinde na kupitia kazi hiyo ukuu wake ukaonekane.
💫Ahadi za Mungu ni za kweli akisema atafanya jambo maishani mwako anafanya kwelikweli.
*💒TUOMBE* 💒
Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu , baba wa mbinguni , Bwana wa majeshi , Mungu wa miungu .
Tunaliinua jina lako na kushukuru tukisema asante kwa kutujalia afya na uzima na kutupa zawadi kuu ya kuiona siku nyingine iitwayo leo .
Mungu ,ahadi zako ni za haki na kweli ukiahidi utatenda jambo maishani mwetu wewe unafanya .
Na sasa tunakuja mbele zako asbh hii tukikuomba utufundishe , utuongoze na ututazame katika kila jambo tutakalolifanya .Maana umeahidi utafanya .
Watazame wasafiri na watu wenye shida mbalimbali ukawaongoze ee Mungu .
Zitazame nchi mbalimbali katika dunia hii ukaachilie amani na kuondoa roho za madaraka na umwagaji wa damu zisizokuwa na hatia .
Katika jina lipitalo majina yote la Bwana Yesu Kristo tunaomba yote haya tukiamini utayafanya .
Amen
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni