GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA π
πGIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA π
SIKU YA SABA
Mwl. Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
π» 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
Mwanzo 4 :9
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
Mwanzo 4 :10
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
Mwanzo 4 :11
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Mwanzo 4 :12
Bwana Yesu apewe sifa.
π« Kumekuwa na mambo mengi yanayomfanya mtu asifikie maisha ambayo Mungu anataka aishi .
π« Katika siku ya kwanza mpaka ya sita tumejifunza mambo mengi ambayo yamekuwa ni giza linalomzuia mtu asione baraka za Mungu .
π« Katika siku hii ya saba na ya kuhitimisha somo hili tutaangalia jambo lingine linalomzuia mtu asione baraka za Mungu .
_π UMWAGAJI WA DAMU ISIYOKUWA NA HATIA_
π« Hakuna jambo linalomfanya mtu asifanikiwe kama kumwaga damu isiyokuwa na hatia .
π» 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
Mwanzo 4 :9
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
Mwanzo 4 :10
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
Mwanzo 4 :11
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Mwanzo 4 :12
π«. Tukimwangalia Kaini alivyomwua ndugu yake , tunaona jinsi damu ya ndugu yake ilivyokuwa ikidai haki kutoka kwenye ardhi .
π« Ardhi inaweza kufunga maisha ya mtu asifanikiwe , hii ni kwasababu ardhi ni lango linalopitisha laana au baraka kwa mtu .
π«Kaini alipomwaga damu ya ndugu yake tunaona ardhi haikumzalia matunda ( kumletea mafanikio) .
➡ Jambo lingine ni utoaji wa mimba
ππ» kutoa mimba pia ni umwagaji wa damu isiyokuwa na hatia na pia ni uuaji wa kiumbe cha Mungu kisichokuwa na hatia .
π« Umwagaji wa damu unamfanya mtu asiuone ufalme wa Mungu ( uzima wa milele ) .
π« Ukitoa mimba na ukanyamazia hiyo hali uendelee nayo bila kuitubia inatakuletea shida sana katika maisha yako .
ππ»Ukitoa mimba unaweza kusababisha yafuatayo maishani mwako na kizazi chako
1⃣ roho ya kuharibu mimba
2⃣ roho ya utasa
3⃣ roho ya kutokuolewa.
ππ» utashangaa binti zako hawaolewi kumbe damu uliyoimwaga imewafunga wanao .
4⃣ Kushindwa kuurithi ufalme wa mbinguni .
ππ» Usipotubu utawekwa hukumuni kutolea hesabu ya damu ya mtoto uliyoimwaga siku ulipotoa mimba .
π« Damu pekee iliyona kibali cha kumwagika ni damu ya Yesu pekee ndyo iliyopata kibali iyafuye makosa yetu.
Lakini kumwaga damu ya mtu ni kujiandalia makao ya jehanamu.
➡ Lakini usiogope maana Mungu anasamehe kila dhambi isipokuwa ya kumkufuru roho Mtakatifu .
π» 28 Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;
Marko 3 :28
29 bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
Marko 3 :29
π« Umeua au umetoa mimba usikae na hiyo dhambi itakuzuia kufanikiwa tubu .
π» Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Mithali 28:13
π«.Kwahiyo bado kuna nafasi ya kufanya toba mbele za Mungu na kurudisha uhusiano wako na Mungu kupitia damu ya Yesu .
ππ» usiiangalie hiyo dhambi ukakosa amani mwangalie Mungu afutaye dhambi .
π» 18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Isaya 1 :18
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
Isaya 1 :19
π« Mungu ni mwenye rehema kubali kutubia dhambi ya umwagaji wa damu isiyokuwa na hatia ili ufanikiwe .
π» 1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
Zaburi 51 :1
2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
Zaburi 51 :2
3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Zaburi 51 :3
4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Zaburi 51 :4
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
Zaburi 51 :5
6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
Zaburi 51 :6
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
Zaburi 51 :7
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
Zaburi 51 :8
➡ HITIMISHO
Umwagaji wa damu ni giza linaloweza likamfanya Mungu asifanikish
e njia zako .
Mungu akubariki sana
https:/peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni