GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA
GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA
_SIKU YA KWANZA_
Mwlm.Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
💻 10 Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote.
Warumi 11 :10
💫 Bwana Yesu asifiwe
✍🏻 Mpendwa kuna giza zito ambalo linamzuia mtu asione baraka za Mungu maishani mwake.
💫 Giza hili tunalonizungumzia siku ya leo katika somo hili ni matendo ambayo mwanadamu anayafanya yasiyomletea Mungu utukufu .
💫 Giza la dhambi linamfanya mtu asione baraka zake na apoteze dira ya maisha yake .
💻 35 Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizanihajui aendako.
Yohana 12 :35
💫Giza linamfanya mtu akose kabisa uelekeo katika maisha yake.
💫 Giza linamfanya mtu awe mtumwa yaani anakuwa katika gereza la mauti ambalo linamzuia asione baraka za Mungu .
💻 Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti,Wamefungwa katika taabu na chuma,
Zaburi 107:10
💫 Giza la kwanza ambalo linazuia baraka za Mungu zisizikufilie ni ✍🏻
1⃣ *UASHERATI NA UZINZI* 🔥
✍🏻Uasherati na uzinzi ni giza linalozuia watu wengi wasione baraka za Mungu .
💫 Uasherati na uzinzi unamzuia mtu katika nyanja kuu tatu .
🛐@ _Kukosa ibada_
👉 uasherati unamfanya mtu akose muda mzuri wa kuwa karibu na Mungu hii inamaana kwamba uasherati na uzinzi ni giza linalomfanya mtu asimwone Mungu
.
👉Tafiti za kiroho zinaonyesha kuwa vijana wengi walioangukia kwenye uasherati na uzinzi wamepungukiwa uwezo wa kifikiri mambo ya Mungu yaani ufahamu wao juu ya sheria za Mungu umefinywa kwa sababu akili zao zimetiwa giza .
💻 Basi alifunua uzinzi wake, na kufunua uchi wake; ndipo roho yangu ikafarakananaye, kama ilivyofarakana na umbu lake.
Ezekieli 23:18
💫Uzinzi unamfanya Mungu afarakane na mtu na kumwacha atembee katika matendo yake ya giza ambayo mwisho wake ni uangamivu .
Kwahiyo uasherati na uzinzi ni giza limfanyalo mtu asiwe karibu na Mungu na mtu akiwa mbali na Mungu hawezi kuona baraka .
💫 Wengine watauliza mbona waasherati na wazinzi wanaongoza ibada kanisani ?
Mpendwa nataka ujue kuwa siyo kila umwonaye kanisani ni mwana wa nuru wengine ni wana wa giza ingali wanazijua sheria za Mungu lakini ni masinagogi ya shetani .
💫 Hukumu inakuja tena kali kwa wale wanaoijua sheria ya Mungu na kuivunja huku wakitembea gizani .
💻 47 Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, walakuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
Luka 12 :47
🌐Kupungukiwa muda wa kusoma neno laMungu
Hili pia ni giza linalokumba vijana wengi leo .
Wameshindwa kusoma neno na kutafakari mambo ya zinaa. Hili jambo lawafanya wakose baraka za Mungu.
🔥 Vifungo na maagano ya uasherati na uzinzi
👉Hili pia ni giza ambalo linazuia vijana wengi hata kwenye kuoa na kuolewa .
👉 Giza hili linazifunga ndoa za vijana wetu leo waishi maisha duni na kuingia kwenye mafarakano .
✍🏻 Vijana wengi husema ndoa ni ngumu kumbe wao ni wagumu lakini ndoa ni rahisi na inaraha sana .
👉Tatizo ni kwamba wanandoa mmeingia kwenye ndoa kila mtu kabeba roho chafu kutoka kwa wapenzi wake hizo roho zimezuia ndoa yenu Mungu asiibariki.
👉 Mungu hawezi kuwamwagia baraka kama hamjazivua roho za wapenzi wenu wa zamani roho hizo ni giza linalozuia ndoa yenu isibarikiwe .
💻 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwilimmoja.
1 Wakorintho 6 :16
👉.Pia kuoa na kucha mke au kuongeza wake wengine ni giza linaloua maisha ya mtu asifanikiwe katika viwango ambavyo Mungu anataka.
Itaendelea ....
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni