GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA
🌐 GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA 🌐
SIKU YA TATU
Mwlm.Peter Francis Masanja
The Voice of God Ministry
Bwana Yesu asifiwe
Karibu tuendelee tena na somo letu hili ikiwa leo ni siku ya tatu .
👉 Kuna mambo ambayo waliookoka yamekuwa giza kwao hata yamewafanya wasione baraka za Mungu maishani mwao .
👉 Matendo yanayokuzuia Mungu asikujibu maombi au asikubariki ni giza kwako linalokuzuia usipokee baraka kwa Mungu .
✍🏻Leo tuangalie giza lingine linalowazuia watu kuzipata baraka za Mungu .
*KUTOKUSAMEHE
💻 25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11 :25
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
Marko 11 :26
💫 Naomba nikukumbushe kuwa msamaha ni jambo kuu sana ambalo Mungu analiangalia katika maisha ya mwanadamu.
💫Kama yeye Mungu alivyo na tabia ya kusamehe na kusahau ndivyo ilivyo na kwa mtu
💫 Kutokusamehe ni dhambi mbele za Mungu dhambi hii inakufanya wewe ukose baraka za Mungu maishani mwako .
💫 Hata hivyo napenda kugusia juu ya sala ambayo wakristo wengi tunakiri tukisema .
" utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea "
Jiulize mpendwa je , nimesamehe walionikosea ❓
Ndipo mwambie Mungu , " unisamehe makosa yangu kama ninavyowasamehe wanaonikosea "
💻 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo 6 :12
💫Katika huu mstari tunajifunza kusamehe kwanza ili Mungu atusamehe .
💻 14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Mathayo 6 :14
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Mathayo 6 :15
💫 Ni nini basi leo nataka ujifunze , nataka ujifunze kuwa usiposamehe Mungu hawezi kukubariki kirahisi rahisi .
💻 4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].
Luka 11 :4
💫 Tujifunze kwamba mtu yeyote asiyesamehe bado yupo mikononi mwa shetani kwahyo inabidi aing'oe roho ya kutokusamehe ili Mungu amsamehe na kumrejesha kwake .
💫 Imekuwaje basi kutokusamehe liwe ni Giza linalozuia baraka za Mungu kukufikia ❓
Jibu ni kwamba kazi ya giza ni kumzuia mtu asione anachokitafta .Au ni nani aliyewahi kutafta sindano gizani akaiona ?
Kwahiyo kutokusamehe kunamfanya mtu asione baraka za Mungu .Hii ni kwa sababu kutokusamehe ni dhambi na dhambi ndiyo giza .
💻 3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.
Luka 17 :3
4 Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Luka 17 :4
💫. Jifunze kusamehe na kusahau ili Mungu akubariki .
✍🏻 Msamaha ni jambo la msingi sana maishani mwako na kama uliapa kutokumsamehe mtu basi futa maneno yako na uachilie msamaha ili Mungu akusamehe pia .
💫 Kusamehe ni njia inayomfanya mtu aone baraka za Mungu haraka sana .
💫 Anayesamehe ana furaha , amani na upendo moyoni mwake .Na ijulikane kuwa Mungu anapenda moyo wenye furaha .
💫Wengine ni wapendwa wanasali kanisa moja lakini walikwazana na hawataki kusalimiana kabisa na ibadani hushikana mikono kwa unafiki , watu kama hao hawawezi kuona baraka za Mungu maishani mwao mpaka wasameheane .Na hata hivyo ijapokuwa wanatoa sadaka sadaka yao ni uchafu mbele za Mungu maana inanena dhambi .
💻 23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
Mathayo 5 :23
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
Mathayo 5 :24
25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
Mathayo 5 :25
💫Liondoe giza la kutokusamehe ili uone baraka za Mungu .
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni