GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA
*🌐GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA 🌐*
SIKU YA NNE
Mwlm.Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
💫BWANA YESU ASIFIWE
Karibu tena tuendelee kujifunza kuhusu somo hili ambalo linalenga kuangalia mambo ambayo yamekuwa giza linalozuia watu wasifikiwe na baraka za Mungu .
➡Jambo la nne ambalo ni giza linalomfanya mtu asione baraka za Mungu hili
_4⃣ KUFANYA KAZI YA MUNGU KWA ULEGEVU_ 💫
💻 Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.
Yeremia 48:10
➡ Kuna hasara kubwa sana kwa mtu amtaftaye Mungu kwa mazoea .
➡ kutokumtafta Mungu kwa bidii kunamfanya mtu akose baraka ambazo anasitahili kupata .
💫Bidii yako katika kumtafuta Mungu ndiyo wingi wa baraka kutoka kwa Mungu .
➡ Usimtafute Mungu katika tatizo tu mtafute Mungu kila wakati.
💻 34 Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta; Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.
Zaburi 78 :34
35 Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao.
Zaburi 78 :35
💫 Mtafute Mungu kwa bidii sana ili aachilie baraka zake juu yako .
💻 1 Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake?
Mithali 8 :1
17 Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
Mithali 8 :17
💫Bidii yako ni ya thamani sana mbele za Mungu .
💻 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Waebrania 12 :14
💫Dumu sana katika neno usilegee soma neno kila siku .
➡ Weka bidii yako katika maombi ili Mungu akujaze baraka ( akujibu maombi ) .
➡ Udhaifu katika maombi ni giza linalomzuia mtu asipate baraka za Mungu .
💻 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
Yakobo 5 :15
16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Yakobo 5 :16
17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Yakobo 5 :17
18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
Yakobo 5 :18
💫Mwangalie Eliya alivyoomba kwa bidii tunaona maombi yake yalileta matokeo mazuri .
💫 Yakobo aling'ang'ana katika kuomba mpaka akabarikiwa , iangalie bidii yake.
💻 24 Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
Mwanzo 32 :24
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
Mwanzo 32 :25
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
Mwanzo 32 :26
27 Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo.
Mwanzo 32 :27
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Mwanzo 32 :28
29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
Mwanzo 32 :29
💫Hakikisha unamtafta Mungu kwa moyo wako wote ili utaona baraka zake
💻 29 Lakini huko, kama mkimtafuta Bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.
Kumbukumbu la Torati 4 :29
➡Ukimtafuta Mungu kwa bidii utapokea kibali cha kumiliki na kitawala.
💻 4 ili Bwana afanye imara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.
1 Wafalme 2 :4
💫weka bidii katika kuwsjulisha watoto wako kumjua Mungu ili wafanikiwe sana .
💻 9 Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
Kumbukumbu la Torati 4 :9
💫Kwahiyo kutokufanya kazi ya Mungu kwa bidii ni giza linalozuia baraka za Mungu kumfikia MTU .
Mungu akubariki sana
Karibu tena siku inayofuata tuendelee
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni