GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA
🌐GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA 🌐
SIKU YA TANO
Mwlm. Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
💫Bwana Yesu asifiwe .
Karibu sana katika mwendelezo wa somo letu nakukaribisha tuendelee kujifunza katika jina la Baba , mwana na Roho Mtakatifu .Amen
💫 Lifuatalo ni giza lingine linalomzuia mtu kupata baraka kutoka kwa Mungu .
🌐 KUTOKUKAA NDANI YA YESU 💫
💻 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
Yohana 8:31
➡ Ukikaa ndani ya Yesu kunafaida kubwa sana .
➡ Maana kuu ya kukaa ndani ya Yesu ni kuyavaa matendo yake na kutii neno la Mungu kwa uaminifu huku ukilifanyia kazi .
💻 22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
Yakobo 1 :22
23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
Yakobo 1 :23
➡ Neno la Kristo likikaa ndani yako utapokea mambo mengi sana kutoka kwa Mungu .
➡. Siyo tu neno likae kwa wingi pia inabidi neno lilokaa ndani yako ulifanyie kazi ili lilete mabadiliko .
💻 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
Yohana 15 :4
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Yohana 15 :5
6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
Yohana 15 :6
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Yohana 15 :7
➡ Ili Mungu akustawishe katika huduma yako au utumishi wako pamoja na mambo yako yote , anakutaka ukae ndani ya Yesu kwanza .
➡ Ukikaa ndani ya Yesu umekaa katika neno na hilo neno litakaa ndani yako na neno hilohilo litaruhusu baraka za Mungu kukufikia kwa wingi.
💻 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Wakolosai 3 :16
17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Wakolosai 3 :17
➡ Kukaa ndani ya Yesu pia inamaanisha kuishi maisha matakatifu .
💻 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
1 Petro 1:15
➡ Maisha ambayo Mungu anamtaka mkristo aishi ni maisha matakatifu maana yeye ni mtakatifu .
➡. Na utakatifu ni kudhirisha kuwa Kristo anakaa ndani yako.
➡Tukikaa ndani ya Yesu tutakuwa tumekaa nuruni na siyo gizani tena.
💻 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
1 Yohana 1:7
➡. Tukikaa nuruni yaani ndani ya Yesu tutakuwa tumeliondoa giza linalotuzuia kupata baraka za Mungu .
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni