GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA
🌐GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA 🌐
SIKU YA SITA
Mwlm. Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
Bwana Yesu asifiwe.
Karibu tena katika mwendelezo wa somo letu .
💫kama tulivyotangulia kusema kuna mambo ambayo yanamfanya mtu asione matokeo ya kile ambacho Mungu kakusaidia ndani yake.
➡Giza lingine linalomzuia mtu asione baraka za Mungu maishani mwake ni ;
🌐KUJITAMKIA AU KUTAMKIWA MANENO MABAYA
💻 2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
Mithali 6 :2
👉🏻 kujitamkia maneno ya kushindwa jambo fulani kulifanya kunamfanya mtu aishi maisha ya kushindwa kufanikiwa kwa sababu amejifungia kufanikiwa .
👉🏻 Maneno mabaya yanakamata mfumo wa maisha ya mtu na kumfanya aishi kulingana na alivyotamka.
💫 Leo kuna changamoto nyingi sana na matatizo mengi kwenye ndoa kwa sababu vijana wengi wamejitamkia maneno mabaya kabla ya ndoa.
👉🏻 Utasikia kijana anasema naolewa tu ili nitoe aibu lakini ndoa ni ngumu sana , mpendwa kama unaingia kwenye ndoa na wazo la kuwa ndoa ni ngumu ndoa yako itakuwa ngumu .
👉🏻 Neno lolote unalojinenea ni mbegu inayoota maishani mwako na mwisho wake utakuja uvune ulichokipanda
Ukipanda kushindwa utavuna kushindwa .
💫 Wengine walijitamkia sitakaa niolewe lakini wakaolewa ,na sasa ndoa zao zipo kwenye hatari ya kuvunjika kwa sababu ya maneno mabaya waliyojitamkia .
💻 20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.
Mithali 18 :20
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.
Mithali 18 :21
👉🏻 Unaona jinsi gani maisha ya mtu yanabebwa na neno analojitamkia .
💫Vijana wengi walishindwa kufanikiwa kwa sababu ya maneno yao mabaya
Anajitamkia Mimi ni maskini , mimi siwezi , mimi wa hivyohivyo , n.k
Sasa haya matamko yanamzuia Mungu kumbariki kwasababu tayari huyu mtu amejitia vifungoni mwenyewe na roho ya kushindwa .
💻 4 Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?
Ayubu 26 :4
👉🏻 neno ni roho , na mtu akijitamkia kushindwa atakuwa amekamatwa na roho ya kushindwa .
👉🏻 Ukumbuke kuwa vitu vyote viliumbwa kwa neno ,.
💻 1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1 :1
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
Yohana 1 :2
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Yohana 1 :3
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Yohana 1 :4
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
Yohana 1 :5
👉🏻 Kwahiyo epuka kujitamkia maneno mabaya ili Mungu akufungulie milango ya baraka.
💻 29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana.
Yeremia 22 :29
30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Yeremia 22 :30
👉🏻 Pia tunaona mtu anaweza kutamkiwa maneno ya kutokufanikiwa ikawa ni chanzo cha mateso maishani mwake .
💫. Kupitia kutamkiwa maneno mabaya watu wengi wamejikuta wanakwama katika maisha yao .
👉🏻 Futa maneno yote mabaya uliyojitamkia au kutamkiwa
💻 10 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
Isaya 8 :10
👉🏻 maneno yote uliyotamkiwa hayatasimama yafute maishani mwako .
💻. 7 Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa.
Isaya 7 :7
Neno lolote baya haliwezi kusimama katika maisha yako ukilifuta.
💫maneno mabaya ni giza linalozuia baraka za Mungu kukufikia .
Popote ulipojitamkia kushindwa au ulitamkiwa kushindwa tamka kufanikiwa .
💻 9 Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama.
Zaburi 33 :9
10 Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.
Zaburi 33 :10
👉🏻Futa maneno ya kushindwa na uweke neno la kufanikiwa lisimamie maisha yako ili Mungu akubariki .
Mungu akubariki sana.
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni