GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA
🌐GIZA LINALOZUIA BARAKA ZA MUNGU KUKUFIKIA🌐
SIKU YA PILI
Mwlm.Peter Francis Masanja
The voice of God Ministry
0679392829
💻 10 Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti, Wamefungwa katika taabu na chuma,
Zaburi 107 :10
11 Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu, Wakalidharau shauri lake Aliye juu.
Zaburi 107 :11
12 Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa wala hakuna msaidizi.
Zaburi 107 :12
💫Bwana Yesu asifiwe .
👉 Nimatumaini yangu kuwa unaendelea kujifunza kupitia mwendelezo wa somo hili ikiwa leo ni siku ya pili tunaendelea na somo hili.
Leo tutaangalia giza lingine linaloweza kuzuia Mungu asikuletee baraka .
2⃣ KUTUMIKIA MIUNGU MINGINE
💫Kutumikia miungu mingine ni giza kubwa ambalo linamfanya mtu akose baraka za Mungu.
💻 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Kutoka 20 :4
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 :5
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kutoka 20 :6
💫 Kutumikia miungu mingine ni hasara kubwa sana katika maisha ya mtu.
💫 Kutumikia miungu mingine huleta uangamivu na mateso katika maisha ya mtu .
💻 11 Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
Waamuzi 2 :11
12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.
Waamuzi 2 :12
13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.
Waamuzi 2 :13
14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
Waamuzi 2 :14
15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.
Waamuzi 2 :15
💫Baada ya kufa Yoshua, Israeli waligeukia miungu mingine wakaacha kumtumikia Mungu aliye watoa utumwani Misri .
💫Angalia mateso waliyoyapata baada ya kumsahau Mungu , yaani Mungu aliwatia mikononi mwa adui .
💫Kwa maana hii Mungu aliwaacha hakuwalinda na adui nao wakaingia kwenye mateso makali sana .
💻 10 Ndipo wana wa Israeli wakamlilia Bwana, wakisema, Sisi tumekufanyia dhambi, kwa sababu tumemwacha Mungu wetu, na kuyatumikia Mabaali.
Waamuzi 10 :10
💫. Angalia jinsi walivyotumikishwa na adui mpaka wakaamua kumrudia Mungu .
💻 3 Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.
1 Samweli 7 :3
4 Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia Bwana peke yake.
1 Samweli 7 :4
💫Najua siku za leo ni vigumu kuona kuwa Mungu amekutia mikononi mwa adui pale unapomsahau na kutumikia miungu mingine .
💫 Ishara zifuatazo utaziona siku za leo
Kwa wale wanaotumikia miungu mingine.
1⃣ Katika uchumi utaona mtu hafanikiwi na hata akifanikiwa kwa baraka za kipepo bado uchumi wake hautadumu.
Uchumi bila baraka za Mungu haudumu .
2⃣ katika afya utaona mtu anamali lakini magonjwa kwake ni rafiki sana.Hii ni kwa sababu wamemsahau Mungu na kugeukia miungu mingine.
💻 25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Kutoka 23 :25
26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.
Kutoka 23 :26
💫Ukiona familia inatumikia miungu mingine ujue baraka za Mungu hazipo hapo na roho za magonjwa na vifo huibuka sana .
3⃣ Katika elimu utaona watoto wengi wanaotoka katika familia za wanaotumikia miungu mingine hawana akili darasani wao ni kufanya vibaya tu.
Hii ni kwa sababu ndani yao hakuna maarifa yatokayo kwa Mungu .
💻 7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Mithali 1 :7
💫. Kutokumtumikia Mungu ni giza linalozuia baraka za Mungu kumfikia mtu katika elimu .
💫Angalia mikoa ambayo kuna uganga na uchawi mwingi kiwango cha elimu kipo duni sana na waliosoma ni wachache sana.
Linganisha watoto wanaotoka katika familia za wachaMungu na za wanaoabudu miungu mingine utaona kuwa kuna wasomi wengi katika familia za wacha Mungu
Kwasababu Mungu kafungua milango ya baraka katika elimu na kuwapa watoto uwezo wa juu sana katika masomo.
💫Kutumikia miungu mingine kunamkosesha mtu amani kwakuwa Mungu hayupo pamoja naye .
💻 3 Naye Bwana alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute mabaali;
2 Mambo ya Nyakati 17 :3
4 lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli.
2 Mambo ya Nyakati 17 :4
5 Kwa hiyo Bwana akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele.
2 Mambo ya Nyakati 17 :5
💫Tunamtazama Yehoshafati katika utawala wake alifanya vizuri sana mpaka mataifa wakamletea zawadi hii ni kuashiria kuwa alikwenda katika njia za Mungu baraka za Mungu zikawa juu yake .
✍🏻Epuka kutumikia miungu mingine maana kuna baraka za kipepo ambazo ni za mda mfupi mtumikie Mungu peke yake ili baraka zinazodumu zikujilie .
Rejea Kumb 28:15 __
Kutumikia miungu mingine ni giza linalofanya baraka za Mungu zisikufikie.
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni