KIJANA NA UKUAJI WA KIROHO
🌐KIJANA NA UKUAJI WA KIROHO 🌐
SIKU YA KWANZA
Mwlm.Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice God Ministry
Bwana Yesu asifiwe
Karibu katika somo hili ambalo limelenga kumfanya kila kijana alisomaye akue kiroho au ainuliwe kiimani .
💻 9 Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Mhubiri 11 :9
👉🏻 Katika utangulizi wa somo hili tutaangalia thamani ya maisha ya kijana katika dunia hii .
👉🏻Idadi kubwa ya waumini makanisani ni vijiana .
💫Kuna mambo ambayo yanamfrahisha sana kijana kuyafanya katika dunia hii mpaka yanamfanya amsahau Mungu lakini mwishoni yanampeleka humumuni .
💫 Uasherati na uzinzi na ulevi ni mambo ambayo yanawafrahisha vijana wengi na kumsahau Mungu lakini mwisho wa mambo haya mwisho wake ni uangamivu .
💻 12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Mithali 14 :12
👉🏻 Lazima kijana atambue kuwa kuna mambo mazuri sana yanayomfurahisha kuyafanya lakini mwisho wake ni kumpeleka hukumuni.
💫Mambo kama hayo yanazuia ukuaji wa kiroho wa kijana .
💫Mambo hayo yanamfanya kijana akose utii mbele za Mungu .
Kwanini kijana akose utii ❓Ni kwa sababu ya kugeukia njia mbaya .
💻 9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
Zaburi 119 :9
💫 Ukuaji wa kiroho wa kijana unahitaji kusafisha njia zake kwanza ili Mungu amuinie imani hadi imani.
➡ Kuna vitu vitatu vinavyoweza kubadilimaisha maisha ya kijana.
1⃣ Kanisa
2⃣ Umri na
3⃣ Dunia ( ulimwegu)
👉🏻 Ili kijana aache njia mbaya anahitaji vitu hivyo vitatu .
💫Kanisa likishindwa kumbadilisha umri utambadilisha .
👉🏻 Akishindwa kubadilika kutokana na kanisa au umri dunia itambadilisha kwa habari ya kukutana na wimbi kali litakalomfanya amkumbuke Mungu .
💫 Kunawakati utamwambia kijana mavazi fulani asivae lakini hawezi kukusikia mpaka atakapofikia umri fulani naye atayaacha.
💫 Katika utangulizi wa somo hili leo tutaegemea zaidi kwa upande wa kijana kubadilishwa na Mungu ili amtumikie na amkuze kiroho .
👉🏻Lazima kijana aitambue thamani ya kuletwa hapa duniani ili ajue faida ya kumtumikia Mungu .
💻 13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Zaburi 139 :13
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi 139 :14
15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Zaburi 139 :15
16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Zaburi 139 :16
💫. Kuna faida kubwa ya kijana kutambua jinsi ujana wake ulivyo wa thamani sana na jinsi Mungu alivyomleta hapa duniani .
💫. Lazima kijana atambue kuwa hakuletwa duniani kutumikishwa na shetani balu aliletwa duniani kufanya kazi ya Mungu .
💻 1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
Mhubiri 12 :1
Leo tutaishia hapa
Karibu katika somo linalofuata tuangalie mambo ambayo kijana anatakiwa ayazingatie ili akue kiroho .
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni