KWANINI ZAMANI WAKIKOSEA WALIKUWA WANADHIBIWA NA KUTUNDIKWA JUU YA MTI ❓

🌐 KWANINI ZAMANI WAKIKOSEA WALIKUWA WANADHIBIWA NA KUTUNDIKWA JUU YA MTI ❓





Mwlm.Peter Francis Masanja

0679392829

The Voice of God Ministry




πŸ‘‰πŸ»Harmani alitundikwa juu ya nguzo za miti .


πŸ‘‰πŸ» Yesu pia aliwekwa juu msalabani .

πŸ‘‰πŸ» Unatakiwa uelewe vitu hivi vitatu .

πŸ‘‰πŸ»Asili ya maovu ( dhambi ) ipo kwenye mti .

πŸ’» 16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,

Mwanzo 2 :16

17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Mwanzo 2 :17

πŸ‘‰πŸ»Tunaliona shina la dhambi lipo kwenye mti

πŸ’» 3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Mwanzo 3 :3

4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

Mwanzo 3 :4

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

Mwanzo 3 :5

6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Mwanzo 3 :6

πŸ‘‰πŸ» Dhambi iliingia duniani kupitia mti

πŸ‘‰πŸ» mti unachukuliwa kama shina la dhambi ndyo maana katika agano la kale utaona mtu akikosea akiadhibiwa anatundikwa juu ya mti .

πŸ’» Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti;

Kumbukumbu la Torati 21:22

πŸ‘‰πŸ» Yachunguze maandiko utaona habari za makosa yote yapo juu ya mti .

πŸ’» Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.

Esta 7:10

Mfalme Ahasuero akawaambia malkia Esta na Mordekai, Myahudi, kusema, Tazama, nimekwisha kumpa Esta nyumba yake Hamani, naye mwenyewe wamekwisha kumtundika juu ya mti, kwa sababu aliwatia mikono Wayahudi.

Esta 8:7

πŸ’« Kwahiyo makosa yote asili yake ni juu ya mti ndyo maana mtu akikosea alitundikwa juu ya mti kwa maana hiyo alirudishwa kwenye dhambi ilikotokea au kuanzia .

πŸ‘‰πŸ» Juu ya mti pia kuna mauti

πŸ’«Jiulize kwanini Musa alimtundika nyoka juu ya mti na aliyekuwa anamwangalia akiumwa na nyoka alipona ❓

πŸ‘‰πŸ» Yule nyoka aliyetundikwa alivunja mauti ( kifo)

πŸ’» Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Hesabu-Numbers 21:9

πŸ‘‰πŸ»Kwanini Yesu alitundikwa msalabani ❓

πŸ’«Kwanza tambua huo msalaba ni mti , na tafsiri ya mti kiroho ni shina la dhambi .

Kwahiyo dhambi iliingia ulimwenguni kupitia vitu vitatu .

1⃣ Nyoka

2⃣ Mti

3⃣ mtu

πŸ‘‰πŸ» mauti na uzima zipo kwenye mti

πŸ‘‰πŸ» Yesu alipotundikwa msalabani maana yake alirudishwa kule dhambi ilikoanzia ili aifute

πŸ’« Ukimtazama Yesu pale msalabani usimtazame tu ukaona msalaba hauna maana .

πŸ’«Msalaba huo maana yake ni shina la mauti , kwahiyo kufa kwake Yesu pale msalabani kulivunja nguvu zote za mauti , ( dhambi , kifo , magonjwa) n.k

πŸ’» 14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,

Waebrania 2 :14

15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.

Waebrania 2 :15

πŸ’«ile damu ya Yesu iliyomwagika msalabani ilifuta makosa yote na kuharibu kazi zote za shetani .

Mungu akubariki sana.

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*