NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA MAOMBI π*
NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA MAOMBI π*
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
francispeter424@gmail.com
π» 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Ufunuo wa Yohana 12:11
π« Damu ya Yesu inanguvu sana ikitumika wakati wa maombi .
π«Damu ya Yesu inanguvu za kumshinda shetani .
π« Damu ya Yesu inatakasa ( inafuta makosa ) .
π» 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Waebrania 9:22
π«Damu ya Yesu inamnyang'anya shetani umiliki.
π» 9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Ufunuo wa Yohana 5:9
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Ufunuo wa Yohana 5:10
π« Damu ya Yesu inanguvu za uponyaji .
π«Damu ya Yesu inavunja nguvu za mauti .
π» 14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Waebrania 2:14
: π«Damu ya Yesu inafuta maneno mabaya
: π« Itumie damu ya Yesu kuvunja madhabahu ya ukoo inayokuunganisha kwenye ibada za mizimu , mashambulizi ya ndoto za wafu na ndoto za nyoka .
π: π«Kila kitu kinachokuhusu maishani mwako ambacho shetani amekishikilia au amekificha leo tunakidai , tunamnyang'anya kwa damu ya Yesu .
π: π«mpendwa , nikuibie siri kwamba shetani akimiliki malango yako ya kiroho anasumbua sana
.π« Shetani anatumia wachawi na waganga kufunga maisha ya mtu
π: π« Ardhi iliyofungwa na waganga kupitia matambiko na mazindiko inamadhara sana kiroho
π: π« Achilia damu ya Yesu iondoshe kila mambo ya matambiko na mazindiko yaliyofanyika katika ardhi ya familia , ardhi unayoikalia , na ardhi ya ukoo .
π: π« Peleka damu kwenye kwenye eneo ambalo unafanyia kazi yako au ofisini kwako .
π: π« mpendwa kunaofisi zingine hazikaliki yaani kuna madhabahu ya shetani imesimama kwa lengo la kutafuna wafanya kazi kwa kufukuzwa au kuugua au kufa kabisa .
π« Kuna kampuni kila meneja akiajiriwa anakimbia kazi , kumbe kuna madhabahu ya shetani imesimamishwa .
π« Mimina damu ya Yesu iondoshe ile madhabahu .
π: π« Kuna ofisi moja mameneja walikuwa hawadumu lakini kumbe maombi yalipofanyika roho wa Mungu akatuonyesha chini ya kiti kuna kitu kimechimbiwa
π: π« Tuliamkia kuchimba tukatoa hirizi tukaichoma , kuanzia siku hiyo wafanyakazi walikuwa hawasalimiani wakaanza kusalimiana .
.π: π«Damu ya Yesu inanena mema .
π: π« Mungu akubariki sana
π: ➡ God bless you
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni