SIFA ZA KIONGOZI WA KIROHO

Kanisani Leo

Mahali: AICT _MTWARA

Tarehe 15 April 2018


Somo 1: 2 Timotheo 2:2

Somo 2: Kutoka 18:21_22


Neno kuu: ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻

🌐 SIFA ZA KIONGOZI WA KIROHO🌐


MWL.Christina Seleka

0684616320

UTANGULIZI

💫 Kanisa lolote la Mungu linapaswa kuchagua viongozi wa kiroho kwa kufuata sifa za kiblia.

💫 Kanisa linatakiwa lichakugue viongozi wa kiroho kwa kuangalia kwa macho ya kiroho na siyo ya mwili yaani mwonekano .

💫 Mtu anaweza kuwa na mwonekano mzuri sana na wa kuvutia lakini hafai kuwa kiongozi wa kiroho .

💫Israeli walijikuta katika taabu na mateso kwa sababu waliweka viongozi ambao waliwatumikisha sana na walilia sana hii ni kwa sababu hawakumsikiliza Mungu katika maamuzi ya kuchagua viongozi .

💫 Walijikuta katika mateso kwa makosa waliyoyafanya kuchagua viongozi kwa sababu ya mwonekano .

SIFA ZA KIONGOZI WA KIROHO


1⃣ Mwenye wito wa kazi ya Bwana .

2⃣ Mkweli

💻 2 Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.

2 Timotheo 2 :2



3⃣ Anayechukia mapato ya aibu .

💻 21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;

Kutoka 18 :21

22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.

Kutoka 18 :22



4⃣ Awe msomaji wa neno la Mungu na kulitendea kazi .

💻 8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Yoshua 1 :8

5⃣ Mwenye uwezo

💻 1 Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.
Matendo ya Mitume 6 :1

2 Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani.

Matendo ya Mitume 6 :2

3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;

Matendo ya Mitume 6 :3

4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.

Matendo ya Mitume 6 :4

5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;

Matendo ya Mitume 6 :5

6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.

Matendo ya Mitume 6 :6


🌐HASARA/HATARI ZA KUCHAGUA KIONGOZI/VIONAOZI WA KIROHO KWA MTAZAMO WA KIMWILI

1⃣Kupishana na makusudi ya Mungu.

💻 10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana.

1 Samweli 8 :10

11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.

1 Samweli 8 :11

12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.

1 Samweli 8 :12

13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.

1 Samweli 8 :13

14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.

1 Samweli 8 :14

15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.

1 Samweli 8 :15

16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe.

1 Samweli 8 :16

17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake.

1 Samweli 8 :17

18 Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile.

1 Samweli 8 :18

19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;

1 Samweli 8 :19

20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu.

1 Samweli 8 :20

21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana.

1 Samweli 8 :21

2⃣Kutanguliza mambo ya kimwili na kuacha mambo ya kiroho.

💻 4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;

1 Samweli 8 :4

5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.

1 Samweli 8 :5

6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.

1 Samweli 8 :6

7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.

1 Samweli 8 :7

8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.

1 Samweli 8 :8

9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.

1 Samweli 8:9

Mungu akubariki sana

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*