TAFAKARI YA LEO ( ASBH )

*πŸ›TAFAKARI YA LEO* πŸ’’




MATENDO YA MITUME 8

MWL.Peter Francis Masanja

0679392829


The Voice God Ministry





1⃣ Tunamwona Stefano wanamzika baada ya kuuawa kwa kupigwa mawe kwa sababu ya kutangaza habari za Yesu .


2⃣ Tunamwona Filipo anahupiri injili ya Yesu na kufanya ishara na miujiza na watu wanamwamini na kubatizwa .


3⃣ Tunamwona Simoni mchawi naye anaamini na kubatizwa


πŸ’» 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

Matendo ya Mitume 8 :12

13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.

Matendo ya Mitume 8 :13



πŸ‘‰πŸ»Kwahiyo kubatizwa kunaanza na kuamini kwanza .



4⃣ Tunawaona mitume wengine wamekuja Samaria kuwawekea mikono walioamini na kubatizwa wampokee roho Mtakatifu.


πŸ’» 14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;

Matendo ya Mitume 8 :14

15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;

Matendo ya Mitume 8 :15

16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.

Matendo ya Mitume 8 :16

17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.

Matendo ya Mitume 8 :17


 5⃣ Tunajifunza kuwa karama ya Mungu haiuzwi


πŸ‘‰πŸ»Usitoe pesa ndyo uombewe na mtumishi .


πŸ’« Yachunguze maandiko

πŸ’» 18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,

Matendo ya Mitume 8 :18

19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.

Matendo ya Mitume 8 :19

20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.

Matendo ya Mitume 8 :20

21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.

Matendo ya Mitume 8 :21



 6⃣ Tunajifunza kuwa , uwezo wa kulisoma neno la Mungu na kulielewa mtu hupewa na Roho Mtakatifu .


πŸ’» 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.

Matendo ya Mitume 8 :31

32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.

Matendo ya Mitume 8 :32

33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.

Matendo ya Mitume 8 :33

34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?

Matendo ya Mitume 8 :34

35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.

Matendo ya Mitume 8 :35

36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?

Matendo ya Mitume 8 :36

37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]

Matendo ya Mitume 8 :37

38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.

Matendo ya Mitume 8 :38

39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.

Matendo ya Mitume 8 :39

40 Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.

Matendo ya Mitume 8 :40


 7⃣ Pia tunajifunza kuwa Injili ni nguzo kuu ya mtu kuamini na kubatizwa.



https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*