TAFAKARI YA LEO

_🌐TAFAKARI YA LEO 🌐_




Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


The Voice of God Ministry


Somo:


πŸ’«MATENDO YAKO MEMA YANAMFANYA MUNGU AKUOKOE SIKU YA DHIKI πŸ’«




πŸ’» 36 Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 

Matendo ya Mitume 9 :36

37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. 
Matendo ya Mitume 9 :37

38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. 
Matendo ya Mitume 9 :38

39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 

Matendo ya Mitume 9 :39

40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. 

Matendo ya Mitume 9 :40

41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai. 

Matendo ya Mitume 9 :41

42 Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana. 

Matendo ya Mitume 9 :42

43 Basi Petro akakaa siku kadha wa kadha huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi. 

Matendo ya Mitume 9 :43


πŸ’«. Ni jambo la wewe kujifikiria umemfanyia jambo gani Mungu la kumfurahisha ili akukumbuke katika shida yako ❓


πŸ’« Je umejitoa kwake kwa bidii katika kuifanya kazi yake kwa uaminifu ❓


πŸ’« Jiulize je , hivi leo Mungu nikiomba anibariki au aniinue ataangalia nini kwangu ili anibariki ❓


πŸ’« Ili Mungu akukumbuke ni lazima ufanye kazi yake kwa bidii .

1⃣ Mtolee Mungu sadaka

πŸ‘‰πŸ»Kumtolea Mungu sadaka siyo mali ulizonazo tu ,

Hata wewe kujitoa katika kufanya yale Mungu anataka uyatende ni sadaka pia .

Mwili wako utoe kwa BWANA uwe chombo kitakatifu mbele zake ili utumike kwake .


2⃣ Tenda mema , usilipe kisasi kisasi ni cha BWANA .



πŸ’« Dorcas ( Tabitha ) anakumbukwa na Mungu kwa kuwa alijaa matendo mema na kudumu katika kumtolea Mungu .

πŸ’« Katika tafakari ya leo ninataka umwangalie Dorcas awe mfano wa kuiga kwako ukatende mema mbele za watu na mbele za Mungu ili Mungu akukumbuke katika shida zako kama vile ndoa , uchumba , biashara, elimu, n.k

Katika kutenda mema kunamfanya Mungu akufungulie mlango wa mafanikio ya kiroho na kimwili ( utajiri).


Matendo yako mema yanamfanya Mungu akuokoe katika shida inayokupata kwa haraka sana .


Mungu akubariki sana


https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*