TAFAKARI YA LEO

*πŸ’«TAFAKARI YA LEO πŸ’«*

26 April 2018.


Mwl.Peter Francis Masanja

The Voice of God Ministry

067392829



Somo : *UKISIMAMA MBELE ZA ADUI KWA JINA LA BWANA ADUI UTAWATIA HOFU* πŸ”₯

πŸ’» 1 Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng'ambo ya Yordani pande za magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari, waliposikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa Israeli, hata tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli.

Yoshua 5 :1







Bwana Yesu asifiwe sana .


πŸ’«Leo nataka tutafakari jinsi Mungu anavyowatia hofu adui zako ukimtegemea yeye  katika safari ya maisha yako .



πŸ’« Inawezekana ulitiwa hofu na adui zako siku nyingi sana katika maisha yako ya wokovu .

πŸ’« Inawezekana adui walikuandama kwa kukuletea mashambulizi makali ya ndoto lakini mtegemee Mungu aliyekausha mto Yordani mbele ya Israeli.



πŸ’« Adui yako ataona ishara na maajabu ambayo Mungu anakutendea maishani mwako naye atakuogopa sana na hataweza kujihami kupigana na wewe.


πŸ’« Mungu anakupa uwezo , nguvu , na mamlaka ya kuwang'oa , kuwasambaratisha,kuwaangamiza, na kuwafukuza adui zako .


πŸ’«Mtegemee Mungu aliye adui wa adui zako katika vita uliyonayo katika uchumi , ndoa, uchumba , na afya yako .


πŸ’» 22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.

Kutoka 23 :22

23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali.

Kutoka 23 :
23


πŸ’« Mpe Mungu nafasi kubwa maishani mwako ili adui zako wayeyuke mioyo yao  ( wakuogope ) kwa sababu jina la BWANA litawafanya wauone wewe ni tishio kwao .


Mungu akubariki sana



https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*