TAFAKARI YA LEO

TAFAKARI YA ASBHI

30 April 2018

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


SAUTI YA MUNGU MINISTRY





πŸ’« JINA LA BWANA LINAKUFANYA UWE IMARA KIROHO NA KIMWILI πŸ’«*

πŸ’» 1 Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.

Zaburi 125:1


πŸ’« Mungu anasema wewe umtumikiaye hutatikisika , hutaona hofu ya adui .

 πŸ’« Atakufanya imara , atakutia nguvu na uwezo mkubwa .

πŸ’« Atakufanya kichwa na siyo mkia tena .

πŸ’«Ameahidi atakubariki mjini na mashambani .

3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.

Kumbukumbu la Torati 28:3

πŸ’« Amekuahidi atawatawanya adui zako wanaokufuatia .


7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

Kumbukumbu la Torati 28:7





πŸ’«Anasema yeye ni adui wa adui zako .

πŸ’«Anasema kwamba wewe ni silaha yake ya vita

πŸ’«Anasema kwa wewe atavunjavunja falme na majeshi ya shetani .

πŸ’«Kwa wewe atafukuza wachawi na waganga .

πŸ’» 20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;
Yeremia 51:20

21 na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;

Yeremia 51:21

22 na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;

Yeremia 51:22

23 na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.

Yeremia 51:23

πŸ’« Mungu anazidi kusema na wewe kwamba usiogope yupo pamoja na we we.

πŸ’» usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Isaya 41:10

πŸ’« Anaongezea kusema kwamba atakusaidia katika shida zako .

πŸ’« Najua unajiuliza swali ? Mungu atanisaidiaje ❓

🌐Atakuandalia watu wake wakusaidie asipotumia watu atatumia hata mnyama .🀝🀝🀝

Ahadi za Mungu ziambatane na wewe

Mungu akubariki sana.


https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*