THAMANI YA UJANA WAKO 🌐

*🌐 THAMATHAMANI YA UJANA WAKO 🌐


SEHEMU YA KWANZA

Mwl. Peter Francis Masanja

francispeter424@gmail.com

067392829

πŸ’«The Vioce of God Ministry πŸ’«

UTANGULIZI
.

πŸ’» Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

1 Timotheo 4:12



πŸ’«Bwana Yesu asifiwe ,


πŸ‘‰πŸ» Karibu katika somo hili namwomba Mungu.afungue macho yako ya kiroho na masikio yako ya kiroho ili uweze kwenda pamoja nami katika somo hili .
..

Mungu afungue moyo wako upate kupokea kile ambacho Mungu amekusudia ukipokee ili upige viwango vya juu sana kupitia jina la Yesu .Amen

πŸ’«Ujana ni nini ❓

πŸ‘‰πŸ» Ujana ni kipindi ambacho mtu anakuwa na umri kati ya miaka 18 mpaka 45 ..

πŸ‘‰πŸ»Kipindi hiki ni cha thamani sana katika maisha ya MTU.

πŸ‘‰πŸ» kwanini hiki kipindi ni cha thamani ❓

➡ Ni kwasababu mtu katika kipindi hiki anatakiwa asikichezee na kukiacha kipite bila kufanikiwa kiroho na kimwili.

➡ Katika kipindi hiki kijana anatakiwa ajitambue yeye yupo hapa duniani kwa kutimiza kusudi fulani

➡ Katika kipindi cha ujana , kijana anatakiwa atambue kuwa kudharauliwa na wanadamu hakuepukiki lakini yeye haimpasi kujidharau.Anatakiwa aijue thamani ya ujana wake.

πŸ’« Kijana anatakiwa awe kielelezo katika mambo yafuatayo:


1⃣ Usemi

πŸ‘‰πŸ» Maneno ya kijana yanatakiwa yawe mazuri na ya hekima siku zote na amjibu kila mtu vizuri .


πŸ’» Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Wakolosai 4:6

2⃣ Mwenendo

πŸ‘‰πŸ» mwenendo hauwezi kutenganishwi na tabia ya mtu .

πŸ‘‰πŸ» Kijana anatakiwa aenende kwa roho ili aweze kuwa mfano wa kuigwa katika matendo yake .

πŸ’» Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

Wagalatia 5:16

πŸ‘‰πŸ» kijana aenendaye kwa roho hawezi kutimiza tamaa za mwili na huyo atakuwa kielelezo .

3⃣ Upendo

πŸ‘‰πŸ» Ili kijana awe kielelezo lazima awe mwenye upendo .

Upendo unamfanya kijana awe kioo cha jamii

πŸ’» Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.

1 Yohana 4:2.

4⃣ Imani

πŸ‘‰πŸ» Kijana anatakiwa asimame Imara katika imani.

πŸ’» 5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;

Matendo ya Mitume 6 :5

➡ Haitoshi tu kuwa na imani bali hiyo imani ijae matendo.

: 5⃣ Usafi

➡ Ili kijana awe kielelezo lazima awe na moyo safi

πŸ’» 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Mathayo 5 :8

πŸ’« Hizi ni sifa ambazo zinafanya kijana amchaye Mungu awe kielelezo .

Mungu akubariki sana

Karibu sehemu ya pili

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*