UJINGA UNAOWAFUNGIA MABINTI WAPOTEZE SIFA ZA KUOLEWA

UJINGA UNAOWAFUNGIA MABINTI WAPOTEZE SIFA ZA KUOLEWA πŸ’«*

 _πŸ‘‰πŸ»THE IGNORANCE THAT CHAINS GIRLS TO BE UNMARRIED_ πŸ’«



Mwl. Peter Francis Masanja .


0679392829
The Voice of God Ministry .



πŸ’«The devil is using the girls to overthrow the God's plans concerning with marriage .

πŸ‘‰πŸ»Shetani anawatumia wanawake kuzuia mpango wa Mungu kuhusu ndoa.


πŸ’« Lucifer have planted the of spirit  wickedness to most of Christian girls and thus they are not walking in the light but their deeds are attached in the darkness.


Shetani amepandikiza roho ya uasi ndani ya binti za kikristo , wanatembea gizani wakiiache njia ambayo Mungu anataka waiendee.


😘😘: Nitachambua

Kuanzia


Kwenye eneo LA

1⃣ Kipato

πŸ‘‰πŸ» shetani katia roho gani kwa wasichana kuhusu kipato ❓


2⃣ Elimu


πŸ‘‰πŸ» Shetani kapandikiza roho gani kwa wasichana kwenye eneo la elimu


3⃣ Imani


πŸ‘‰πŸ»Shetani kapandikiza roho gani kwa mabinti kuhusu imani .


 πŸ˜˜πŸ˜˜: 1⃣ Katika eneo la kipato ( uchumi )

πŸ‘‰ Shetani ametia roho ya tamaa ya vitu ndani ya binti wengi .

πŸ‘‰ Wamekuwa wa kuangalia ni mwanaume gani aliye na kipato kati ya hawa ili nimkubalie .


πŸ’« Siyo jambo la kushangaa kuona binti anamdanganya kijana kuwa Mungu hajanionyesha kwako , kumbe amemwona huyo kijana anakipato kidogo na huku kuna  fulani anamwona kamzidi .


πŸ‘‰ Leo binti zetu waliookoka wanamdanganya roho wa Mungu kwa kusingizia kuwa kasema nao kumbe hata hawajaingia kwenye maombi wameangalia uchumi na kuamua kuwakataa vijana .

: πŸ’« Pia katika eneo hili la kipato , binti zetu walio na kazi  ajira au kazi zao zimewafunga wasiolewe .


 πŸ‘‰Ajira kwa binti wa kisasa imeleta kiburi na roho ya kutokujishusha hata kama kakosea .


πŸ’« Ajira / kazi imewafanya binti wengi wajione wamekamilika ( wanajiweza ) yaani hata bila mume wataishi.
Kwahiyo akikosolewa na mwanaume mtu mwenye fikra ya kwamba anajiweza lazima amjibu vibaya mwanaume .

 πŸ’« Unafikiri kwanini mabinti wengi wenye kazi wanaishia kuzaa tu na wanaume kabla ya ndoa ❓


 πŸ‘‰ Ni kwasababu ya kiburi na kutokujua nafasi ya mwanamke kibiblia ambayo ni kutii waume zao , sasa wao badala ya kutii wanawadharau na kuwaambia hata kama ukiniacha nitaishi na wanangu najiweza.

Na wanaongezea sitaki kusumbuliwa na mwanaume .


πŸ’« Hii ni kukosa utii na kumwasi Mungu .


πŸ’» Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

Waefeso 5:22


πŸ‘‰ Usimdharau mwanaume kwa sababu tu umeajiriwa na unaweza kujitunza .


Ukimdharau ujue kabisa utatolea hesabu mbinguni hicho kiburi chako .

Kumtii mume ni agizo toka kwa Mungu .


 πŸ‘‰ Usitegemee kijana aje kukuchumbia kama utatanguliza kauli za kwamba unajiweza hata peke yako waweza kuishi .


 πŸ’« Roho ya uasherati kwa binti zetu imeenea kwa kasi sana , hasa walio na kazi na tunao makanisani wengine wanaimba kwaya .

Kiburi cha kazi usikilete mbele za mwanaume  utafunga na kuomba usione wa kuja kukuchumbia kumbe hata Mungu kakukataa anataka uondoe kiburi kwanza ndiyo afungue mlango wa kumpata mume .


πŸ‘‰ Ndyo utashangaa binti kaajiriwa na anakazi na ameokoka lakini katika eneo la upole , unyenyekevu , na utii yeye sifuri .Mwisho wake umri ukienda wanamwasi Mungu na kuzaa na wanaume wajinga wa mtaani na tena wapinga Kristo .

πŸ’« Huwezi kusema unamwomba Mungu upate mume halafu huku huna unyenyekevu na upole na utii , utakuwa mwongo na utabadilisha watumishi wa Mungu wakuombee lakini kumbe wewe ndiye tatizo.


 ✍ Tii maandiko matakatifu yanavyosema kuwa mtii mume ili Mungu apitishe baraka kwako wewe na watoto wako .


2⃣ Jambo la pili ni elimu .


Katika eneo la elimu kuna wanaume wengi wanalalamika kuwa hawawezi kuoa mwanamke msomi .

Kwa sababu mwanamke msomi anaasili ya dharau na ujuaji  , na majivuno na ubishi .


 πŸ’« Usijivunie na elimu ya dunia hii jivunie elimu ya Mungu ambayo inakupa karama ya kumtii mumeo mtarajiwa.


πŸ’« Wewe binti uliyeokoka tambua kuwa ndoa haina PhD ,Masters , au degree , Usimdharau mume wako kwa sababu umesoma acha kiburi

Tambua kwamba uchumba au ndoa unajengwa na upendo wa dhati kutoka kwa Mungu na siyo elimu yako .


Ukiona mwanamke amesoma na anasema ameokoka huku anamdharau mumewe ujue huyo hamjui Mungu ,( ni mpinga Kristo )


πŸ’» 4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;

Tito 2 :4

5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.

Tito 2 :5


✍ Binti zetu kwa sababu ya kujivunia elimu wamelifanya jina la Mungu litukanwe.

Wameokoka kwa nje lakini ndani hakuna roho wa Mungu aitwaye utii



3⃣ Katika eneo la imani


πŸ’» Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Warumi 14:23


 πŸ’« Nitazungumzia hilisuala la imani kwa pande za kuanzisha mahusiano .

πŸ‘‰ Binti yangu usianzishe mahusiano huku unasema akikuzingua tu unampiga chini .

Hii ni mbegu utakayoivuna katika mahusiano yako .


πŸ’« Binti zetu hawana matumaini katika mahusiano kila siku wanawaza kuachika .


πŸ‘‰ Sikia wewe binti , usianzishe mahusiano huku unaamini kuwa wanaume ni waongo wote , kupitia kutamka kwako unaruhusu roho ya uharibifu .


 πŸ’« Ukiwa na mashaka katika mahusiano usitegemee Mungu kuyalinda mahusiano yenu .


 πŸ’» Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

Waebrania 10:38


πŸ’« Mungu hayafurahii mahusiano ya mashaka,

Ooh ninamchumba wangu ila siamini kama tutaoana .

Msemo huu ni hatari sana na unatakiwa kuepukwa kwenye mahusiano


Ukiona huna amani sitisha mahusiano usije ukaendelea mbele ukajiletea matatizo



πŸ’« Uchumba wowote wenye neno unamchumba lakini , huo huwa na mwisho mbaya sana.


4⃣ Kiroho .



πŸ‘‰ Kuna baadhi ya binti zetu wamefungishwa ndoa za kupepo katika ulimwengu wa roho.


πŸ’« Kupitia ndoto za mapenzi ( kuota wanazini na wanaume ) binti zetu wamepandikizwa roho chafu kama vile  : hasira , matukano, kiburi, kujiinua, n.k


✍ Sababu hii ya kiroho ni pana sana   lakini nataka niseme hivi

Jinsi unavyoona mke wa mtu anavyotaka asifuatiliwe na wanaume tena ndivyo ilivyo na binti aliyeolewa katika ulimwengu wa roho huchukia wanaume wote na kumtii mume wake anayemjia ndotoni usiku .


 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

1 Wakorintho 6 :16

17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.

1 Wakorintho 6 :17


πŸ‘‰ binti akiwa amefungwa kiroho ni kizuizi kikubwa sana kinachomfanya asiolewe.


πŸ‘‰Hii ni kwasababu ataona ni kawaida sana kuishi bila ndoa kwasababu hajui kama anamilikiwa na pepo/jini .



πŸ’« ndyo maana utaona anajiremba na kutia wanja na kila aina ya vitu bandia ili kumfurahisha mume wake wa kiriho ( pepo/jini ).



πŸ’«Utasikia watu wanaulizana kuwa binti huyu ni mzuri sana lakini kwanini haolewi ❓

Jibu ni kwamba ameolewa bila ninyi kujua , sasa fanyeni maombi ya ukombozi mtaijua kweli yote


 ✍ Sababu nyingine ya kiroho ni dhambi ya ukoo , au familia ( wazazi ) ambayo haijapitishwa kwenye toba na bado inatafuna maisha ya binti pia


Yeremia 22:29_30


πŸ‘‰Hakuna kitu kibaya kama pigo ambalo limeletwa kwenye ukoo au familia ili kuharibu

Uchumba au ndoa .



πŸ’« Shangazi aliolewa akaachana na mumewe.

πŸ’«Fulani alitoa mimba.

πŸ’« mama alizaa nje ya ndoa kwa siri.



πŸ‘‰ Haya kama hayajafanyiwa toba ni kizuizi kikubwa kwa binti .
[4/21, 17:39] Living Sucrifice 😘😘: Mungu akubariki sana nakutakia siku njema

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*