URAFIKI , UCHUMBA NA NDOA

*๐ŸŒURAFIKI , UCHUMBA NA NDOA ๐Ÿ’ซ*

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

The Voice of God Ministry

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

*๐Ÿ’ซMAHUSIANO NI UGOJWA WA KIMWILI NA KIROHO* ๐Ÿ’ซ

๐Ÿ’ซNi jambo la kushangaza kumwona mtu anamsahau Mungu kisa simu yake haijapokelewa na mchumba wake .

๐Ÿ’ซUnanuna siku nzima yanini kununa โ“

โžกHuwezi kushindana na mwanadamu mwenye kinywa .

๐Ÿ’ป Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

Danieli 6:10

๐Ÿ’ซMahusiano yasikufanye uhame njia uelekee njia ya mauti .

๐Ÿ’ซPresha za nini โ“

๐Ÿ’ซ Hasira za nini โ“

๐Ÿ’ซ Mashaka ya nini โ“

๐Ÿ’ซUnatakiwa ujue kuwa mbinguni hawaoi wala kuolewa .

๐Ÿ’ป Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.

Marko 12:25

๐Ÿ’ซ Yanini kujitaabisha na kujitafutia magonjwa ya moyo uzeeni โ“

๐Ÿ’ป Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.

Mathayo 22:30

๐Ÿ’ซLabda nikwambie wewe ambaye hujaoa

Mungu alikuleta duniani uwe na mtu atakayekufanya uwe na furaha na siyo huzuni .

๐Ÿ’ซ Ukiona uchumba tu mikwaruzano mingi ujue ndani ya ndoa ni maratatu ya hapo .

๐Ÿ’ซPresha za mahusiano weka pembeni mtafte Mungu

๐Ÿ’ซUna mtu ndyo unatarajia umuoe lakini kabla ya ndoa tu mmeanza kujibizana vibaya  na bahati mbaya umeharibu siku nzima kwa mambo ya kipumbavu .

๐Ÿ’ป 15 Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.

Mithali 5 :15

16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?

Mithali 5 :16

17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.

Mithali 5 :17

18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.

Mithali 5 :18

19 Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.

Mithali 5 :19

๐Ÿ’ซKama unabiblia pigia mstari neno

Umfurahie mke wa ujana wako

Mithali 5:18b

Biblia haijasema umvumilie mke wa ujana wako .โŒโŒ

๐Ÿ’ซUnaona hupendwi unalazimisha kupendwa embu mkimbie shetani ๐Ÿƒ๐Ÿปโ€โ™‚๐Ÿƒ๐Ÿปโ€โ™‚๐Ÿƒ๐Ÿปโ€โ™‚

Tafta amani ya moyo wako acha kuwa na shingo ngumu .

๐Ÿ’ซYule uliyenaye na unamtarajia awe mke wako au mume wako lazima umfurahie

Usipomfurahia tambua Mungu kakataa hayo mahusiano na anakuonyesha viashiria unajifanya huoni .

๐Ÿ’ซPalipo na huzuni hakuna mda wa ibada hata kidogo .

๐Ÿ’ซsiku mbili mmepatana , ya tatu mnagombana tena , hivi mnafikiri huo ni uchumba ni mpango wa Mungu โ“

๐Ÿ’ซPalipo na amani ya moyo katika mahusiano kuna ibada na kuna mkono wa Mungu .

๐Ÿ’ซ Najua anakusumbua sana unajifukiria kumwacha huwezi lakini ni heri ukachukua maamuzi magumu maana ukimuoa itakuwa hasara kwako .

๐Ÿ’ซ Utakwazwa kila saa na utakosa mda mzuri wa kumtafakari Mungu .

๐Ÿ’ซMahusiano yasiyokuwa na faida , yasiyokuwa na amani yanatia ganzi moyoni mwako usisikie neno la Mungu .

๐Ÿ’ซKingine msiwe romantic sana kwenye mahusiano msiwe kila saa mkipigiana simu nyie mahaba tu .

Ongeeni pia mambo ya Mungu .

๐Ÿ’ซ Katika uchumba wenu tengeni muda wa kumtafakari Mungu

๐Ÿ’ซMshirikishe mwenzako mambo ya kiroho ili mkija kuoana utukufu wa Mungu ukae kwenye ndoa yenu .

๐Ÿ’ซ Msiwekeze mda wenu wote kwenye mahaba ( romance )

Ooh ! I love you โ—

Kila saa maongezi hayo hamna mengine ya kuongea โ“

: ๐Ÿ’ซ Badilikeni tafteni mda wa kuombea uchumba wenu na ikibidi mfunge pamoja
Mkifanya hivyo mtabarikiwa sana

Maana Mungu atawasikia na kuwabariki atasema kwamba watu hawa wapo kwenye uchumba lakini wamenikumbuka pia hawakuangalia uchumba wao tu .

: Hitimisho

โžก Jiepushe na mahusiano ya ugomvi maana yatakufanya ushindwe kumwona Mungu .

โžก Jiepushe na mahaba ( romance ) kila wakati

Kumbukeni Mungu ndiye mlizi wa mahusiano yenu , hivyo tengeni mda wa kumtafakari pamoja na kuombeana .

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

๐Ÿ”ฐ MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA ๐Ÿ›*