USHUHUDA
*TUJIFUNZE KUHUSU USHUHUDA*
Na, Peter Francis
🌐 *USHUHUDA* 💫
*➡Ushuhuda ni nini.??*
➡Ushuhuda ni ushahidi au uthibitisho wa jambo fulani lililotokea au kufanyika ( kufanywa / kutendwa) .
➡ Tunaposhuhudia jambo tunashudia utendaji wa jambo katika ulimwengu wa roho na ulimwengu unaoonekana .
➡ Ili ushuhuda uwe ushuhuda lazima kuwe na mtu anayeshuhudia yaani shahidi aliyeona tukio likitendeka kwake .
➡ Huwezi kushuhudia kama hujaona kilichotendeka utakuwa mwongo .
💻 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Ufunuo wa Yohana 12 :11
➡ katika maisha yako unatakiwa uelewe kuwa ushuhuda umebeba neno au andiko linalothibitisha tukio
➡ nguvu ya kumshinda shetani imebebwa na neno la Mungu
➡ neno la Mungu ni ushuhuda ambao mkristo anautumia kuutangaza uweza wa Mungu
💫 Ili ushuhuda wako uitwe ushuhuda lazima useme nini ambacho Mungu amekutendea
➡lazima ujue ulipitia jaribu gani ambalo ulifikia wakati huwezi kabisa na ulikata tamaa lakini Mungu akakuokoa .
➡Ushuhuda wako unaoutoa lazima utoe fundisho kwa wengine
➡ushuhuda lazima uongeze viwango vya imani katika maisha ya wengine
➡ uliugua sana kiasi kwamba madaktari walishindwa mpaka wakawa wanasema wewe utakufa kulingana na hali uliyo kuwa nayo lakini Mungu alinyosha mkono wake akaachilia uponyaji .
Huu ni ushuhuda
➡ Ulihamia kwenye eneo ukakutana na vita kali sana ya kiroho eneo halijatulia ukafanya maombi pakawa na amani Mungu katenda makuu
Huu ni ushuhuda
➡ Umefikia wakati ulikata tamaa baada ya kupigwa vita vya maneno na hila za kufukuzwa kazi na wachonganishi
Lakini waliokuwa wanakutaftia sababu za kufukuzwa wao ndio wakafukuzwa kulingana na nguvu ya maombi uliyoyafanya
Huu ni ushuhuda
🤝🤝🤝🤝🤝
➡ Ushuhuda unaoutoa lazima watu wakisikia wajisikie umewagusa mioyo yao na kuamini kwamba Mungu anaweza.
➡ Ukitembea makanisani ukiwa unasikiliza shuhuda za watu utaona wengine wanatania kweli 😀😀😀😀
➡ Kusimama mbele ya madhabahu kusema
Namshukuru Mungu nimeamka salama huu siyo ushuhuda mpendwa 😀😀😀
Ushuhuda hutoa fundisho kwa watu na kupitia ushuhuda wengine huokoka .
➡ Ushuhuda unaonyesha vita ambayo mtu ilimpata na Mungu akaingilia kati
➡ Maombi ya Yehoshafati yamebeba ushuhuda ndani yake yanaonyesha mambo makuu aliyoyatenda Mungu
Yaani jinsi alivyowapiga adui
➡ Kwahiyo uingiapo kwenye maombi mkumbushe Mungu makuu aliyoyatenda kupitia neno
➡ Ndyo maana aombaye kwa kuhusisha neno la Mungu ni tishio sana katika ulimwengu wa roho
Yaani akiingia eneo fulani kuna wakuu wa giza watahama.
➡ Ukiingia mtaa fulani kuna wachawi watahama kwa jina la Yesu. Lakini yakupasa utumie neno la Mungu kuizima mishale yao na vikao vyao
ISAYA 54:15, 17
➡ Mungu analiangalia neno ili akutendee jambo
➡ Mwambie kwamba Mungu ulisema hivi na ikawa sasa leo nakuomba fanya sawasawa na ulivyosema na ikawa
Zaburi 33: 9
➡ ndyo maana shetani anaogopa sana watu wanaomkataa kwa kutumia maandiko
Maandiko ni ushuhuda unaomfanya shetani akose cha kumfanya mtu .
➡ mwangalie Yesu pale nyikani alivyojibizana na shetani
Kila alivyojaribu kumdanganya alimwambia *IMEANDIKWA*
➡ Jifunze ,
1⃣ ushuhuda lazima uwafanye watu waamini kuwa Mungu yupo na anaweza kuokoa
2⃣ Ushuhuda lazima uguse maisha ya watu
3⃣Ushuhuda lazima umfanye mtu amtegemee Mungu na siyo wanadamu
Msaada wa wanadamu ni mfupi lakini msaada wa Mungu ni wa milele
Mwanadamu unayemtegemea akusaidie anaweza kufariki akakuacha lakini Mungu hawezi kukuacha .
➡ wengine watakukataa lakini Mungu atakuletea watu ambao siyo ndugu zako kabisa watakusaidia
➡ Wanaokucheka waache wakucheke sana lakini ipo siku ya kuinuliwa kwako watakuja kukuomba msaada .
Mungu akubariki sana
Maoni
Chapisha Maoni