YUPO MUNGU , ADUI WA ADUI ZAKO ATAKUTETEA 💫*

*💫YUPO MUNGU , ADUI WA ADUI ZAKO ATAKUTETEA 💫*


Mwl.Peter Francis Masanja


0679392829


The Voice of God Ministry



💫Ijapokuwa adui ni wengi wamekukatisha tamaa katika maisha yako , usifadhaike wala usiogope maana yupo Mungu atawaondoa hao wanaokutisha.



💻 22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.

Kutoka 23:22

23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali.

Kutoka 23:23



💫Ijapokuwa hao adui ni wengi sana wewe msikilize Mungu akupe maelekezo ya kuwatawanya mbele zako .



💫 Inawezekana wamekutia katika magereza ya dhambi , magereza ya umaskini , magereza ya magonjwa , n.k
BWANA atauyonsha mkono wake kupitia malaika wake naye atakutoa huko .


💻 4 Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.

Matendo ya Mitume 12:4

5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.

Matendo ya Mitume 12:5

6 Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.

Matendo ya Mitume 12:6

7 Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.


Matendo ya Mitume 12:7

8 Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate.

Matendo ya Mitume 12:8

9 Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.

Matendo ya Mitume 12:9

10 Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.

Matendo ya Mitume 12:10

11 Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.

Matendo ya Mitume 12:11



💫 Angalia jinsi Petro alivyookolewa , utaona jinsi gani Mungu anawaokoa wampendao na kumcha yeye.


💫 Kwahiyo usiiangalie shida uliyonayo mwangalie Mungu katika shida uliyonayo ili aachilie njia ya kukutoa kwenye hiyo shida


Mungu akubariki sana


https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*