ALIYE NA ROHO WA MUNGU HUKETISHWA PAMOJA NA WAKUU πŸ’’

πŸ’« ALIYE NA ROHO WA MUNGU  HUKETISHWA PAMOJA NA WAKUU πŸ’’*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


SAUTI YA MUNGU MINISTRY







πŸ’« Je unajua kuwa wewe ukiongozwa na roho wa Mungu utawatisha wakuu dunia?



πŸ’« Je , unajua kuwa ukiongozwa na roho wa Mungu unapata kibali ❓



 πŸ’« Maisha yako ya wokovu yategemee uongozi wa Roho Mtakatifu .




πŸ’» Mwanzo 41

38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?

39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.

40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.



πŸ’« Mwangalie Yusufu alipata kibali akawa mkuu katika utawala wa Farao.



πŸ’« Unaona hadi farao anashangaa akisema


🎀 Tupate wapi mtu kama huyu , mwenye roho ya Mungu ndani yake ❓



πŸ’« Alipomwangalia Yusufu aliona ukuu wa Mungu yaani Bwana wa majeshi .



πŸ’« Alishangaa ile ndoto amewezaje kuitafsiri , maana aliwakusanya waganga wote walishindwa kujua maana ya hiyo ndoto .



πŸ’« Je , Yusufu aliwezaje kuitafsiri ndoto ya farao ❓

Naam, ni kwasababu alikuwa na roho ya Mungu ndani yake .




 πŸ’« Utauliza , je kuwa na roho ya Mungu utawezaje kutafsiri ndoto ❓


Twende tuyachunguze maandiko




πŸ’» Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

1 Wakorintho 2:10



 πŸ’« Roho Mtakatifu alimfunulia Yusufu maana ya ndoto ya Farao .



πŸ’« Tunaona jinsi Roho Mtakatifu alivyomfunulia Yusufu maana ya ndoto ya Farao


Tuona hii ndoto aliotaje huyo farao ❓




πŸ’» 1 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto.

Mwanzo 41:1

2 Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini.

Mwanzo 41:2

3 Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto.

Mwanzo 41:3

4 Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka.

Mwanzo 41:4




πŸ’« Tunaona huyo farao aliona ng'ombe saba wenye sifa hizi

1⃣ Wazuri

2⃣ wanono


✍🏻 Walipanda kutoka mtoni


 ✍ Walikuwa wanakula nyasi kando ya mto



 πŸ’« Akaona tena ng'ombe saba


Embu tuyachunguze maandiko tuone hao wengine saba walimuwaje ❓



 πŸ’» 3 Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto.

Mwanzo 41:3

4 Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka.

Mwanzo 41:4




πŸ’« Ng'ombe hao walikuwa na sifa hizi

1⃣ wabaya

2⃣ wamekonda



✍🏻 Walifanyaje ❓


πŸ–Š wakawameza wale saba waliowazuri na wanono .



πŸ’« Ndoto ya pili aliyoota farao aliona masuke saba manene

Na masuke mengine membamba _mabaya .


Lakini katika hiyo ndoto akaona hayo masuke membamba yakayameza hayo masuke manene .



πŸ–Š Tuyachunguze maandiko




πŸ’» 5 Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema.

Mwanzo 41:5

6 Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.

Mwanzo 41:6

7 Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.

Mwanzo 41:7



πŸ’« Yusufu alipoelezwa hakupata tabu kabisa kuitafsiri ndoto hiyo ya farao kwa sababu alimtegemea Mungu sana



πŸ’« Ilibidi amwulize Roho wa Mungu kwanza kupata maana ya hizo ndoto mbili za farao kama ifuatavyo ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



 Wale ng'ombe saba na masuke saba wanono ( manene ) ni miaka saba ya shibe yaani ya chakula kingi sana .





πŸ–ŠWale ng'ombe saba wabaya waliokonda na masuke saba mabaya ni miaka saba ya njaa .



πŸ’» 25 Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.

Mwanzo 41:25

26 Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.

Mwanzo 41:26

27 Na wale ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa.

Mwanzo 41:27

29 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri.

Mwanzo 41:29

30 Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi.




πŸ’« Hiki ndicho kilimfanya Yusufu awe mkuu wa pili kutoka kwa farao .



 πŸ’« Kama somo linavyosema aongozwaye na Roho wa Mungu huketishwa pamoja na wakuu



πŸ–Š Angalia jinsi Mungu anavyowapa kibali wale wamtegemeao na kumtii.



 πŸ’« Mfano mwingine ni Danieli naye alipata kibali akawa mkuu katika ufalme wa Nebkadreza mfalme wa Babeli




πŸ’« Daneli naye alitafsiri ndoto ya mfalme Nebkadreza




πŸ’» 19 Ndipo Danielii alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danielii akamhimidi Mungu wa mbinguni.

Danieli 2:19

26 Mfalme akajibu, akamwambia Danielii, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake.

Danieli 2:26

27 Danielii akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu;

Danieli 2:27

48 Basi mfalme akamtukuza Danielii, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.

Danieli 2:48

49 Tena, Danielii akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme.

Danieli 2:49




 πŸ’« Tunamwona Danieli anafanyika kuwa mkuu juu ya maliwali wote Babeli

Hii ni kwasababu alimshangaza Nebkadreza kwa kuweza kutafsiri hiyo ndoto yake .



πŸ–Š Naomba nihitimishe kusema kwamba


πŸ’« Tafta uongozi wa roho Mtakatifu ilo Mungu akupe kibali kila uendako utakuwa mkuu  na watu wote watakuangalia wewe .




πŸ’« Mungu akibariki sana



https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*