IJUE NGUVU YA KUMSIFU MUNGU KATIKA MAOMBI π€π₯
π€πΊ IJUE NGUVU YA KUMSIFU MUNGU KATIKA MAOMBI π€π₯
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
π« Fahamu kwamba unapomsifu Mungu kwa nyimbo unazidi kumfukuza shetani .
π« Ivi unajua kuwa ukimsifu Mungu mapepo hukimbia ❓
π« Mpendwa maombi yako yanategemea kumsifu Mungu maana Mungu anaketi mahali pa sifa .
π» 25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
Matendo ya Mitume 16:25
26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.
Matendo ya Mitume 16:26
27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.
Matendo ya Mitume 16:27
28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.
Matendo ya Mitume 16:28
29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;
Matendo ya Mitume 16:29
π« Maombi yako yaambatane na nyimbo za kumsifu Mungu ili ujihakikishie ushindi .
π« Kumwimbia Mungu sifa huvunja kazi zote za ibilisi
Sifa zinawatia hofu maadui na kuyeyuka mioyo yao .
π€ Unaona Paulo na Sila walipoimba sifa milango ya gereza ikafunguka ππππ
π€ Yule mlinzi aliyekuwa anawalinda ( askari magereza ) alitaka kujiua kanisa π€£π€£π€£π€£ kumsifu Mungu kuna nguvu kubwa sana .
π€ Kupitia kumsifu Mungu mashetani hutetemeka na kuamini
Ona huyo askari magereza aliamini na kubatizwa kabisa yeye na familia yake .
Halleluya π€π€π€πΊπΊπΊ
Nawaza tu hizo nyimbo za kina Paulo na Sila zilivyokuwa nziri mpaka Mungu kashuka kuwashughulikia maadui π€£π€£π€£
Oooh Halleluya πΊπΊπΊπΉπΉπ₯π₯π€π€
π» Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
Zaburi 33:3
π€ Paulo na Sila waliimba kwa ustadi kabisa π€π€πΊπ₯π₯
π« Yaani ndani ya gereza kulikuwa na shangwe huo usiku wa manane , mpaka wafungwa wengine nao waliungana na Paulo na Sila kuimba .
π€π€πΊπ₯πΊπΉ
Halleluya .
π» Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.
Zaburi 43:4
π€πΊ Paulo na Sila hawakukumbuka kufungwa kwao walimsifu Mungu kwa furaha walijua kabisa wakiwa na huzuni Mungu asingetenda miujiza angewaacha wasote kwanza sasa walijiongeza wenyewe wakaona hapa ni kusifu tu mpaka kieleweke π€π€π€πΊπ₯π₯πΉπΉ
Halleluya
π€πΊ Nikitafakari nabaki najiuliza tu inamaana hawakuogopa wafungwa wengine ❓
Nikakumbuka neno
Usiogope maana mimi ni pamoja nawe
π€£π€£ Hakika Bwana alikuwa pamoja na Paulo na Sila
π€π€π€π₯π₯πΊπΊπΊπ»π»π§πΈ
Halleluya
π€ Nakumbuka tena Yoshua aliambiwa auzunguke ukuta wa Yeriko mara saba akawaambia watu wauzunguke kwa shangwe na nderemo na nyimbo
Wee Ukuta wa Yeriko ulianguka
π€π€π€πΊπΊπ₯π»πΈπ»
Halleluya
π» 4 Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao.
Yoshua 6:4
5 Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili.
Yoshua 6:5
π€ Sifa ina nguvu sana inabomoa kuta na kufungua njia ambapo shetani amezuia watu wa Mungu wasipite .
π€π€π»π»π»π₯πΊπΊ
Halleluya
π« Nakuomba leo uwe na desturi ya kumsifu Mungu katika maombi yako katika jina la Yesu .Amen
Nitaendelea siku nyingine
Karibu sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni