IJUE NGUVU YA KUTUMIA NENO KATIKA KILA HITAJI UNALOMWOMBA MUNG

πŸ’«IJUE NGUVU YA KUTUMIA NENO KATIKA KILA HITAJI UNALOMWOMBA MUNGU πŸ’»*



Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


🎀SAUTI YA MUNGU MINISTRYπŸ’’



πŸ’« _BWANA YESU ASIFIWE_ 🎀



✍🏻 Mtu wa Mungu , kunafaida kubwa sana ya kutumia neno la Mungu katika kila jambo unalomwomba Mungu .



πŸ’« Maombi yako yajikite ndani ya neno la Mungu ili liwe ushuhuda mbele za Mungu .



πŸ’» 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

Ufunuo wa Yohana 12:11



πŸ’« Ukitumia neno katika maombi unajihakikishia ushindi zaidi , kwasababu nguvu ya kumshinda shetani imo ndani ya neno .



✍🏻 ZINGATIA HUU MFANO




πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’




πŸ’« Unataka Mungu akutendee nini ❓



Mungu anauliza unataka akutendee nini



πŸ’» Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema.

Hosea 6:4



πŸ’«Mungu anauliza nini akutendee maishani mwako




 Kama Bwana alivyosema


πŸ’» 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

Marko 16:17

18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Marko 16:18


Pokea uzima katika jina la Yesu .



πŸ’« Katika jina la Yesu ninaamuru kila roho ya magonjwa na roho ya mauti iachie maisha yako popote ulipo .


πŸ’» Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.

Luka 7:21





 Sikiliza



✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻


Ivi unajua nguvu ya neno la Mungu ukilitumia kwenye maombi ❓


πŸ’« Leo nataka tujifunze kutumia neno la Mungu katika kila tuombalo .



πŸ’«Ukiwa unamshukuru Mungu


Sema hivi


πŸ’« Mungu nakushukuru kwakuwa unasema


πŸ’» Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 107:1


Ninakushukuru kwa kuwa wewe ni mwema , wewe ni Mungu mweza wa yote , ninakila sabanu ya kusema asante kwa kunipa uzima , asante kwa kunipa afya , wastahili sifa , heshima , na utukufu , nakuita maishani mwangu uniongoze sasa na hata milele .Amen



 πŸ’« Ukiwa unaomba maombi ya toba .

Tumia maandiko yafuatayo :

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻


πŸ’» 18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Isaya 1:18





πŸ’» 1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.

Zaburi 51:1

2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.

Zaburi 51:2

3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Zaburi 51:3

4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.

Zaburi 51:4

5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.

Zaburi 51:5

6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,

Zaburi 51:6

7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji

Zaburi 51:7

8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.

Zaburi 51:8

9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.

Zaburi 51:9

10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu

Zaburi 51:10

11 Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

Zaburi 51:11

12 Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.

Zaburi 51:12

13 Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.

Zaburi 51:13



 πŸ’» 8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.

1 Yohana 1:8

9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

1 Yohana 1:9




πŸ’«Huzuni ni ishara ya kuwa unafuatiliwa na roho ya mauti


πŸ’» 14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,

Waebrania 2:14

15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.

Waebrania 2:15



Huzuni isiyokuwa na sababu ikuachie katika jina la Yesu .

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Ukiwa unaombea uchumi ( biashara ) au ajira yako .


Mungu ulisema kwamba :

πŸ’» 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Kumbukumbu la Torati 28:3

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Kumbukumbu la Torati 28:4

5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
Kumbukumbu la Torati 28:5

6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
Kumbukumbu la Torati 28:6



πŸ›Nakuomba bariki biashara yangu , bariki watoto wangu    , bariki miradi yangu ya biashara sawasawa na mapenz yake



πŸ’« Unaombea milango yako  ya uchumi ifunguliwe

Tumia neno hili :


πŸ’» 11 Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.

Isaya 60:11



Mwambie Mungu afungue milango yako ya uchumi sema :

Eeh Mungu  , ni wewe unasema malango yangu yatakuwa wazi mchana na usiku .

Ninakuomba ufungue milango yangu ya biashara na kazi yoyote niifanyayo katika jina la Yesu.Amen


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻

Unaweza ukaongeza maneno yako kwa kadri roho wa Mungu atakavyokuongoza .



Mungu akubariki sana

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*