ITUMIE NGUVU YA IMANI KUBADILI MABAYA KUWA MEMA π*
π«ITUMIE NGUVU YA IMANI KUBADILI MABAYA KUWA MEMA π*
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
π» 32 Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;
Waebrania 11:32
33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,
Waebrania 11:33
34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.
Waebrania 11:34
π« Ndani ya imani kuna nguvu mbalimbali .
π« Unatakiwa kujua kuwa imani inanguvu tofauti na kila nguvu inaleta matokeo fulani katika maisha yako.
_πNGUVU ZILIZOPO NDANI YA IMANI_ π
1⃣ Uponyaji
2⃣ Utajiri
3⃣ Urejesho
4⃣ Ushindi
π« Je , wewe unajua kuwa unanguvu ya kubadili mabaya kuwa mema ❓
π« Usiyaone mabaya ukafikiri yamebeba mabaya bali kuna mema yamejificha ndani yake.
π« Daniel alipandishwa cheo kwa sababu kwa sababu alisimamia imani katika kiwango cha juu sana .
π« Itumie nguvu ya imani kuwashangaza maadui wanaokuzunguka .
ππ» Mwangalie nabii Eliya , aliomba kwa imani moto ukashuka kutoka mbinguni mpaka manabii wa baali walistaajabu .
ππ» Pia angalia Eliya aliomba kwa imani moto ukamshukia na kumteketeza yule akida .
π» Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.
2 Wafalme 1:10
ππ» Eliya huyohuyo aliomba kwa imani mvua zikaacha kunyesha .
Hii ni nguvu ya imani .
π» Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Yakobo 5:17
π« Imani inavifanya vitu visivyoonekana vije kufanya kazi pamoja na wewe.
π« Nguvu ya kubadilisha mabaya kuwa mema inawafanya adui zako wakutumimie .
ππ» Danieli alikuwa mkuu kwa Nebkadreza kwa sababu ya ile nguvu ya imani aliyokuwa nayo .Mpaka Nebkadreza aliomwogopa Mungu wa Daniel akakiri kuwa Mungu wa Daniel ni Mungu wa kuabudiwa .
ππ»Mwangalie Yususu alikuwa mfungwa lakini alikuja kuwa waziri mkuu katika utawala wa farao .
ππ» Nguvu ya kubadili ubaya kuwa wema inamfanya mtu atumikiwe na adui zake.
π» 39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.
Mwanzo 41:39
40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.
Mwanzo 41:40
41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.
Mwanzo 41:41
42 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Mwanzo 41:42
43 Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
Mwanzo 41:43
44 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.
Mwanzo 41:44
ππ» Katika mstari wa 44 hapo juu utaona Yusufu anatumimiwa na adui zake sasa
π« Inawezekana wewe unaishi kwa mama wa kambo au kwa ndugu zako wamekugeuza kuwa mfanyakazi wao wa ndani wakidhani wanakukomesha kumbe wanakufanya siku moja waje wakutumikie .
π« Unapokuwa unaishi kwa ndugu unabebeshwa kazi zote wewe furahi ipo siku hao watoto wao watakuja wakutumikie , Mungu hadhihakiwi .
π« Mtegemee Mungu amini kuwa Mungu aliyewaokoa wana wa Israeli na mikono ya farao yupo atakutetea .
π« Bwana ataweka adui zako chini ya miguu yako
ππ» Wewe utakuja kuwatawala na kuwa na amri juu yao .
π« Anayekutaftia sababu huko ulipoajiriwa mwambie huwezi kuacha kazi kwa sababu yake mpaka BWANA atakapokuambia umetosha .
π« Huwezi kusemwa mabaya bila kuwa na jema linaloonekana ndani yako .
π« Mabaya ndiyo yanayosababisha mema yaonekane .
ππ»Mwangalie Yesu alitendwa mabaya kupitia mabaya aliyotendewa pamoja na kusulubiwa na kufa kwake sisi tumepata uzima wa milele .
ππ» Kama Yesu alitendwa yote hayo akafa pale msalabani na Mungu akamfufua
Amimi kuwa katika maisha yako pia Mungu anaweza kukufanya mkuu sana.
π« Imani inaamua nini Mungu akutendee
Neema ya Mungu na iwe pamoja nawe
https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni
Chapisha Maoni