KIJANA IMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU UHESHIMIKE πŸ’’*

πŸ’«
KIJANA IMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU UHESHIMIKE πŸ’’*




Mwl.Peter Francis Masanja


0679392829


SAUTI YA MUNGU MINISTRY



πŸ’» vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.

Danieli 1:4



 πŸ’« Ujana wako usikubali uutie madoa  yaani sifa mbaya katika jamii .



πŸ’« Wewe kama kijana hupaswi kabisa kujichafua na kubandikwa majina ya aibu hapa duniani .



 πŸ’« Kuwa msafi kila wakati , ujana safi ni kutii na kulifuata neno la Mungu .



πŸ’» Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.

Zaburi 119:9


πŸ’« Nguvu zako kijana zimebebwa na neno la Mungu

Bila neno haiwezekani uwe na nguvu za kiroho za kumshinda shetani .



 πŸ’« Kijana utaiwa una nguvu pale utakapoliweka neno la Mungu moyoni mwako na kuliganyia kazi .


Hapo utamshinda shetani .


πŸ’» ........... Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

1 Yohana 2:14




πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻



πŸ’» Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

Mithali 28:1


 πŸ’« Akikujia mchumba mwovu atakukimbia tu hawezi kubaki kwako wewe ni shujaa πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻



✍🏻 Simama katika kweli kijana usiyumbishwe na marafiki



 πŸ’« Angalia Mungu anasema nini katika maisha yako na siyo marafiki wanasema nini ufanye .



πŸ’« Msikilize Mungu , tenda sawasawa na maagizo yake ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Punguza orodha ya marafiki wasio na manufaa kwako ondoa kabisa hao watakupoteza .

✍🏻✍πŸ»πŸ’«✍🏻✍🏻✍🏻


 πŸ’« Kaa na marafiki wenye maono , ili ufikie maisha ya viwango vya juu sana.


πŸ’« Haiwezekani unakaa na rafiki saa zote habari za wanawake tu au za wanaume tu huyo jitenge naye , mkimbie atakutia roho ya uasherati na uzinzi .

πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



 πŸ’« Haiwezekani uishi na rafiki yeye haamini kuwa zinaa inashindwa kwa neno la Kristo pekee

Hata kama anasema ameokoka mkimbie πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’« Ondoa marafiki wasiokufaa


Ukipata mshahara wao ndiyo wanaanza kupanga eti mnaenda bar fulani ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



✍🏻 Kijana futa namba za marafiki unaoona ukipata pesa wanakutafta mkastarehe hao hawakufai kijana kamwe .✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻


πŸ’« Leo hii ukifikiria kwa makini kabisa unitajie marafiki zako watatu waaminifu na ni msaada kwako utajifikiria sana na unaweza usiwe nao .


πŸ’« Marafiki ambao ukitembea nao watu hawawezi kukupakazia sifa mbaya .



πŸ’ͺ🏻 Itumie nguvu uliyopewa na Mungu yaani nguvu ya neno ikuoatie marafiki wazuri .



 πŸ’« Uwe na marafiki ambao ukiambatana nao watu hawatanung'unika juu yako .

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍πŸ»πŸ’«✍🏻


πŸ’» 17 Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.

Danieli 1:17



 πŸ’« Daniel alikuwa na marafiki watatu , Shadrach, Meshach na Abednego yaani alijivunivunia kuwa na hawa marafiki .


 πŸ’« Lazima unapomwonyesha mzazi wako marafiki zako afurahie kabisa asianze kuguna juu ya aina ya marafiki ulionao .✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Tenda sawasawa na neno la Mungu usiache kabisa


πŸ’« Wakitafuta kijana aliyeokoka mwaminifu na mwenye hekima wasisite kukutaja wewe .



πŸ’» 8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Yoshua 1:8



πŸ’« Ukitenda sawasawa na neno utapata kibali mbele za Mungu na wanadamu  , hekima ya Mungu itawale ndani yako .



πŸ’« Watakugombania kila mahali watakuhitaji ili utatue matatizo yao .✍🏻✍🏻✍πŸ»πŸ’«✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



 πŸ’« Haijalishi wewe unaonekana mdogo kwao lakini Yesu Kristo uliye naye amekukuza πŸ’«πŸ’«πŸ’«πŸ’«πŸ’«



πŸ’« Wewe ni kijana shupavu na Mungu ameahidi atakupa hekima na atakufundisha kuwaongoza hao watu ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’» 6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.

Yeremia 1:6

7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.

Yeremia 1:7



πŸ’« Watu huuliza je , inaewezekanaje huyu kijana mdogo anishauri kuhusu ndoa yangu ❓


Ni Roho ya hekima na ushauri imekaa ndani yake ndyo maana anakushauri usihoji kuwa hajaoa tambua asemayo yanatoka kwa Mungu kupitia yeye Mungu anakupa maelekezo uyatii .


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Kijana mwanifu mbele za Mungu hupata kibali cha kumiliki na kutawala .



πŸ’» 3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.

Yoshua 1:3



πŸ’« Kila sehemu utakayofika utakuwa mkuu



πŸ’« Kijana mwenye nguvu akiondoka watu wa eneo hilo hujihisi ukiwa hii ni kwa sababu wameona manufaa yake katika maisha yao .



 πŸ’«Hakikisha ukifika sehemu siku unatoka watambue mazuri unayowatendea wazee kwa vijana wakutakie safari njema



πŸ’« Siyo waanze heeee afadhali limetoka

Yaani unasafiri watu wanakusema afadhali umetoka kwamba walichoshwa na matendo yako mabaya .

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Hofu ya Mungu ikae ndani yako .




Mungu akubariki sana




πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*