πŸ’’ KIJANA NA MAISHA YA KIROHO ✍🏻*

πŸ’’ KIJANA NA MAISHA YA KIROHO ✍🏻*




Mwl.Peter Francis Masanja .

0679392829

Sauti Ya Mungu Ministry




Swali : NIFANYE NINI ILI NIKUE KIROHO ❓


πŸ’» 22 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.

Matendo ya Mitume 14:22



πŸ’« Inawezekana kuna watu huwa wanajiuliza hawapati majibu kuhusu nini wafanye ili wawe imara kiroho .


πŸ’« Lakini leo Mungu anakuonyesha mambo ya kufanya ili mtu fulani ambaye wa kwanza ni mimi , wewe na yule .



πŸ’« Kuna kila sababu ya kujifunza mbinu zitakazokusaidia kiroho .



πŸ’« Katika kujifunza mbinu za kiroho , kuna mambo mawili ya kuzingatia .

1⃣ Kuachana na mambo fulani ili ukue kiroho .



✍🏻 Kuna baadhi ya mambo lazima kijana ayaache ili akue kiroho .



πŸ’« Baadhi ya mambo hayo ni kama vile ; mambo ya mizaha, tamaa za dunia kama vile ulevi , uzinzi, uasherati , n.k

Kuacha kutumikia miungu ya kigeni ,



πŸ’« Acha kutumia mda mwingi kwenye mambo yasiyo na maana tafta kujadili mambo ya kiMungu .



πŸ’« Acha kupoteza muda wako kwenye movie ( filamu ) masaa mengi



2⃣ FANYA YAFUATAYO ILI UKUE KIROHO


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« DUMU KATIKA KUSOMA NENO




✍🏻 Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya usomaji wa neno na ukuaji wa kiroho wa kijana .



 πŸ’» 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Wakolosai 3:16



πŸ’« Kadri unavyozidi kusoma neno na kulifanyia kazi ndivyo unazidi kukua kiroho.



πŸ’« Neno la Mungu likikaa kwa wingi ndani ya moyo wako linahalalisha ukuaji wa kiroho .


πŸ’» Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;

Yohana 8:31



πŸ’« Baada ya kumwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako unakazi ya kusoma neno



 πŸ’«Ndyo maana utaona anawaambia wale Wayahudi waliomwamini wakae katika neno .

Kukaa katika neno maana yake ni kulisoma neno na kulitendea kazi .



πŸ’« Mtu asomaye neno ni mwanafunzi wa Yesu kwelikweli

πŸ‘‰πŸ» Kwa maana hiyo mtu ambaye hasomi neno bado hajakuwa mwanafunzi wa Yesu kweli kweli ( hajakua kiroho ) .




πŸ’« KAA KARIBU NA MLEZI WAKO WA KIROHO


πŸ‘‰πŸ» Vijana wengi wakiokoka wanajisahau kukaa karibu na walezi wao wa kiroho kitu ambacho kinawafanya wapoteze dira ya kiroho .



✍🏻 baba yako wa kiroho ni mtu muhimu wa kukufanya wewe ukue kiroho ,


 Ukiwa karibu naye utajifunza mbinu nyingi za kiroho



πŸ’« TAFTA MARAFIKI WA IMANI



Haruni alijifunzia utumishi kwa Musa



πŸ‘‰πŸ»Je wewe unarafiki gani ambaye anakufanya ukue kiroho ( anakuweka karibu na Mungu )


 πŸ‘‰πŸ» usikubali kuwa na marafiki ambao watakufanya ufe kiroho .


πŸ‘‰πŸ» Petro alikuwa karibu sana na Yesu ndyo maana alimpenda .



 πŸ‘‰πŸ»Je rafiki yako wa karibu sana anakufanya umtafakari Mungu ❓

Kama ni hapana huo urafiki unafaida gani ❓



πŸ’« Rafiki uliye naye anaweza akaawa mchango kwa wewe kuanguka au kukua kiroho



πŸ’« waangalie wa kina Shadrak , Meshack na Abedinego hawa vijana waliimarishana kiroho .Nawewe tafta watu ambao watakufanya ukue kiroho


 Naomba niishie hapo kwa leo


Mungu akubariki sana

https://peterfrancismasanja.blogspot.com


Karibu siki nyingine tuendelee na somo letu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*