KULITUNZA KUNDI LA MUNGU LISIPOTEE 💒*
💫 KULITUNZA KUNDI LA MUNGU LISIPOTEE 💒*
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
💻 28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Matendo ya Mitume 20:28
29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
Matendo ya Mitume 20:29
30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.
Matendo ya Mitume 20:30
💫 Leo kumezuka mapotovu mengi katika kanisa la Mungu .
💫 Watu wa Mungu wanaangamia kwa kufuata mafundisho yapotoshayo .
💫 Kuna makanisa leo yameibuka yaani wanasali ibadani huku wanakunywa pombe.
💫 Kuna baadhi ya makanisa leo yanahubiri kubarikiwa eti watu wapate magari na majumba kuliko kuwaambia watubu maana dhambi imewazingira na kuwaharibu wamekuwa watumwa wa dhambi .
💫 Kanisa la Mungu haliwezi kupona bila kuwaambia watu kutubu .
💫 Kundi la Mungu lililopotea halipendi mafundisho ya kukemea dhambi bali linapenda mafundisho mapotovu .
💻 9 Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;
Isaya 30:9
10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Isaya 30:10
11 tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu.
Isaya 30:11
12 Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo;
Isaya 30:12
💫 Mtume Paulo alionya watumishi wa Mungu walitunze kundi la Mungu lisipotee .
💫 Lakini bado neno la Mungu linaonya kuwa kuna mbwa mwitu wameingia kanisani kulipotosha kanisa.
💫 Nguvu ya watakatifu imedhoofishwa leo kanisani , watakatifu nao wamepotezwa .
💻 11 Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini.
Danieli 12:11
💫Mtu wa Mungu dumu sana katika kuyachunguza maandiko na kuyahakiki yale wakuambiayo watumishi wa Mungu .
💫 Soma maandiko , tafuta kuyajua ili usipotezwe.
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni