KUUSAFISHA MOYO

πŸ“’ KUUSAFISHA MOYO πŸ“™*



πŸ’» Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

Zaburi 119:11



πŸ’« Moyo hauwezi ukaliweka neno kama haujausafisha vizuri



 πŸ’» Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.

Hosea 10:12


πŸ’« Neno la Mungu haliwezi kukaa moyoni mwako likastawi kama kuna magugu yanayozuia lisiote .


πŸ’« Moyo ni shamba la kiroho

Sasa kama kuna magugu udogo hautakuwa mzuri kwa mbegu kuifanya mizizi ipate nafasi ya kuufanya mmea ukue vizuri .


πŸ’« Twende tuyaone haya magugu yanayozuia neno la Mungu lisikae moyoni mwa mtu .




πŸ’» 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

Mathayo 15:19



πŸ’« Magugu yanayozuia neno la Mungu lisizae matunda moyoni mwa mtu ni


πŸ“™ MAWAZO MABAYA


πŸ“™ UUAJI


πŸ“™UZINZI

πŸ“™ UASHERATI


πŸ“™ WIVI

πŸ“™ USHUHUDA WA UONGO


πŸ“™ MATUKANO


πŸ“™ WIVU


πŸ“™ KINYONGO


πŸ“™ KIBURI


πŸ“™ DHARAU


πŸ“™ KUTOKUSAMEHE


N.K




πŸ’« Usafishe moyo wako ili neno la Mungu likae ndani yake



πŸ’» 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Mathayo 5:8



πŸ’« Moyo ukiwa safi , huwezi kumtenda Mungu dhambi kwa sababu neno lake litastawi kwa wingi .



πŸ’» Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

Zaburi 119:11



πŸ’« Moyo ukiwa safi utakufanya uzitii sheria za Mungu



πŸ’» 1 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.

Mithali 7:1

2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.

Mithali 7:2

3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

Mithali 7:3



Mungu akubariki sana akupe wepesi wa kuyaelewa haya .



πŸ“™ *HITIMISHO* πŸ“’



Jifunze kuombea viungo vifuatavyo kwako .


πŸ“™ Ombea moyo wako


πŸ“™ Ombea macho yako maana kwa kuona wengi wanazini


πŸ“™ Ombea ulimi ( kinywa chako )

Usitukane , usinene mabaya .



πŸ“™ Ombea ufahamu wako


πŸ“™ Ombea miguu yako

Isikimbilie uovu .


πŸ“™ Ombea mikono yako .

Uipushe na umwagaji wa damu isiyokuwa na hatia .






πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›




https://peterfrancismasanja.blogspot.com




Mungu awabariki sana


Karibuni Mtwara Mjini



πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*