MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA UCHUMBA NA NDOA πŸ™†

πŸ’« MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA UCHUMBA NA NDOA πŸ™†πŸ»‍♂*




Mwl.Peter Francis Masanja


0679392829


🌹SAUTI YA MUNGU MINISTRY 🌹



πŸ’» Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.

Yeremia 6:14



πŸ’« Kuna mambo wengi sana ya kujiuliza unapotaka kujiingiza katika Uchumba au ndoa .



πŸ’«mambo haya nataka niyaweke wazi kisayansi na kiroho pia .



πŸ’« Usiyachukulie mahusiano ( Urafiki , Uchumba au Ndoa ) kuwa ni jambo la kuamkia tu na kusema unamuoa au unaolewa na fulani .



πŸ’« Uchumba au Ndoa umebeba magonjwa mengi mno endapo utakosea mwenzi wa kuwa naye .



πŸ’« Moja ya magonjwa yanayosababishwa na Uchumba na ndoa ni Ugonjwa wa hisia.

πŸ‘‰πŸ»Tatizo hili huwapata wale walioumizwa , huwa hawajihisi tena kupendwa.




πŸ’« Kunawengine baada ya kuumizwa walijikatia tamaa kabisa na kusema yeyote atakayekuja mimi ananioa tu


Hawa wamejikuta wanaingia kwenye hatari sana na kujipa msongo wa mawazo .



πŸ’« Msongo wa mawazo


πŸ‘‰πŸ» Huu pia ni ugonjwa unaoweza kusababishwa na Uchumba au Ndoa .

πŸ‘‰πŸ» Usishangae kumwona binti alikuwa bonge lakini alipoolewa akakonda na kuchakaa .Hali hii inaletwa na mitihani mizito anayoipitia kwenye ndoa ikiwemo kupishana na mwenzi wake .

Msongo wa mawazo unakondesha .



πŸ’« Hasira

πŸ‘‰πŸ»Hili pia ni gonjwa linalosababishwa na uchumba na ndoa .



πŸ’» Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?

Amosi 3:3




πŸ’«Uchumba ambao kila siku makwazo unasababisha hasira sana hasa kwa yule anayekwazika na mtu wake .



πŸ’«Mizaha na makwazo katika Uchumba ni hatari kwa maisha ya mtu
Maana huzaa hasira na kumfanya mtu amsahau Mungu .




πŸ’« Ugonjwa wa kusahau .


πŸ‘‰πŸ» Huu pia ni ugonjwa unaotafuna wachumba au ndoa za watu ,



πŸ’« Uchumba wenu ukizidi makwazo huo haufai na kama mmoja wenu hataki kubadilika ni matatizo hapo .



πŸ’« Unajua kuwa kunawatu wamekuwa wepesi kukasirika kwa sababu wamezoezwa kuchokozwa na wachumba zao au wenzi wao na hasira imekuwa sehemu ya maisha yao .



πŸ‘‰πŸ» Epukeni kuleteana mambo ya makwazo katika uchumba au ndoa .



πŸ’» 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Zaburi 1:1

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

Zaburi 1:2



πŸ’« Ukimchumbia mtu anayejiona yeye yupo sahihi kila wakati hataki kukubali kosa hata umwelezaje , utahangaika sana kukua kiuchumi , kiafya na kiroho pia .

Aina ya mtu huyo dawa yake ni kumkimbia πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



πŸ’« Gonjwa linalosababishwa na mahusiano ni ugonjwa wa moyo ( presha ) .


πŸ‘‰πŸ» ugonjwa huu unaweza kumpata mtu baada ya mda fulani .

πŸ‘‰πŸ» Mtu anapokwazika mishipa ya moyo hutanuka sana hii ikiendelea mda mrefu huleta madhara makubwa sana ndani ya moyo .



 πŸ’« Unaweza kumkuta mtu anahuzuni amekonda sana kumbe haumwi lakini mawazo yamemnyonya mwili wake .



πŸ’« Hello , vijana msilazimishe Uchumba , mkilazimisha kuingia agano la ndoa na mtu asiyesahihi mmekwisha .



 πŸ’« Ndoa za kikristo mkifunga hakuna kuachana , mkipeana talaka hakuna kuolewa wala kuoa tena .



πŸ’« Sasa ni jukumu lako kuchagua , kuoa au kuolewa baada ya talaka uikose mbingu au usioe au kuolewa ili uurithi ufalme wa mbinguni .


 πŸ’« Ni jukumu lako kuamua kumuasi Mungu kwa kujua kabisa au kumtii .


πŸ’« Itakuwa ni heri usiolewe kuliko kusema ukajaribu kuolewa mkizinguana mpeane talaka , tambua mkipeana talaka hamruhusiwi kuoa au kuolewa.

Ndoa siyo nguo kwamba ujaribishie .



Jaribishieni nguo na siyo ndoa .

πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



 πŸ’« Helloo , nimefundisha kama roho wa Mungu alivyoniongoza

Sasa chagua yafuatayo


πŸ’» Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;

Kumbukumbu la Torati 30:19




1⃣ Ng'ang'ana na mtu ambaye siyo sahihi ukidai utaenda kumsamehe na kumvumilia ili ukafe kiroho na kiuchumi.


2⃣ Kila siku wewe anakuletea makwazo hujui kuwa huyo siyo wako ❓Piga chini tafta mtu sahihi ukaishi kwa amani .



3⃣ Chagua kutoa talaka uoe / uolewe uikose mbingu



4⃣ Chagua kupeana talaka usioe / usiolewe maisha yako yote ili uurithi ufalme wa mbinguni .



HITIMISHO


πŸ’« Mwenzi sahihi ni yule utakayemfurahia kipindi cha Uchumba na Ndoa pia πŸ’«



πŸ’« Hatuoani tukisema tukavumiliane tunaoana ili tukafrahiane πŸ’«


πŸ’« Furaha ikikosekana katika Uchumba kwenye ndoa itakuwa kilio πŸ’«



πŸ’«. Kujali simu au messages za mwenzako na kuzijibu hukimbiza dharau na hali ya kujihisi kutokupendwa .Hii huimarisha Uchumba au Ndoa πŸ’«



Mungu akubariki sana



https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*