MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MAOMBI π
π« MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MAOMBI π
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
π» 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Waefeso 6:11
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 6:12
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Waefeso 6:13
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
Waefeso 6:14
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
Waefeso 6:15
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Waefeso 6:16
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Waefeso 6:17
π« Kama askari aendavyo vitani , vivyo hivyo na mtu aingiapo katika maombi anatakiwa kujua kuwa maombi ni vita.
π« Ili mtu aingie kwenye maombi anatakiwa ajipange kwanza , maana anakwenda vitani kupambana na shetani na jeshi lake .
π« Mtu aendapo vitani huchukua silaha yake na kuiweka tayari kwa kuanza vita .
Mfano , ataandaa bunduki na risasi nyingi kwaajili ya kumpiga adui.
π« Kwa mtu mwombaji , anapomwendea Mungu anatakiwa ajipange na kuhakikisha kuwa moyo wake wote upo kwa BWA
π« Baada ya kujipanga anatakiwa kujua kwamba kutangaza vita na shetani vita kwelikweli .
π« Unatakiwa kufahamu kwamba silaha kuu ya kumshinda shetani ni neno la Kristo pekee.
π« Shetani hupingwa kwa neno , bila neno huwezi kumshinda shetani na hila zake.
π« Neno la Kristo linamfanya shetani akimbie .
π» Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Yakobo 4:7
π«Shetani anapingwa kwa neno
π« Unasisitizwa sana kabla ya kuanza maombi hakikisha unaomba ulinzi.
π« Tubu pale uponkosea Mungu
π« Mkaribishe roho Mtakatifu awe mwalimu wako katika maombi yako .
π» 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Warumi 8:26
π« Lialike jeshi kutoka mbinguni likulinde
Pia jifunike na damu ya Yesu .
π» Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?
Kumbukumbu la Torati 32:30
π« Ni kazi ngumu kumfanya shetani akukimbie , mpaka uite msaada kutoka mbinguni.
π Ualike jeshi la malaika kutoka mbinguni liwe pamoja na wewe katika maombi .
π« Vita ya kiroho unayopigana siyo yako ni vita ya Mungu na adui zako
π« Mungu ni adui wa adui zako wanaokusumbua katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa macho .
π« Ili Mungu aingilie hiyo vita lazima umwite yeye maana ukinyamaza hawezi kuwaondosha adui zako.
π» 6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;
Isaya 62:6
π«Hutakiwi kunyamaza kimya wewe mwana wa Mungu maana Mungu mwenyewe anasisitiza usinyamaze mkumbushe mahitaji yako .
π« Maombi yako yatafaa zaidi ukianza na kumsifu Mungu .
π« Kumwimbia Mungu sifa na kuabudu kunamfanya Mungu aachilie nguvu ya ajabu ndani yako .
π« Maombi ya mtu anayeanza na kumsifu Mungu yana nguvu sana kuliko maombi makavu yaani maombi bila kumsifu Mungu .
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
Mungu akubariki sana nahitimisha kwa kuaema hivi.
π« Katika maombi zingatia
1⃣ Sifa na kuabudu ili maombi yako yawe ya ushindi .
2⃣ Hakikisha unamwalika Roho Mtakatifu akufundishe vita .
3⃣ Alika jeshi la malaika kutoka mbinguni likuzingire ili shetani asipate nafasi ya kukudhuru.
4⃣ Jifunike na damu ya YESU wewe na vitu vyote ulivyonavyo ili shetani asipate nafasi ya kukudhuru wewe na vitu vyako.
5⃣ Hakikisha unatumia neno la Mungu katika maombi yako maana neno ndyo silaha kuu ya kumharibu shetani .
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni