ROHO YA KUKATAA MAFUNDISHO YA UZIMA

πŸ’« ROHO YA KUKATAA MAFUNDISHO YA UZIMA 



Mwl.Peter Francis Masanja .

0679392829


From :


SAUTI YA MUNGU MINISTRY




πŸ’» Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

Wakolosai 2:8


πŸ’« Kumezuka upinzani mkubwa sana katika kanisa kati ya wale wanaoitaka kweli na wale wanaotaka kupewa mafundisho ya uongo .



πŸ’« Watumishi wa Mungu tuna kazi kubwa sana tukikemea tumetukana watu wakati umetumia neno baadhi ya Wakristo ni wazinzi halafu ukitaka wakuchukie sema inawezekana na humu wamo 🀣🀣🀣🀣🀣



πŸ’« Kwanini ukasirike kama hufanyi na sijakutaja , au nilikuona πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’« Leo hii kanisani mtu akisikia masomo ya kukemea uovu anachukia .


Oooh ' Anajifanya mtakatifu


Oooh anajifanya ameokoka kuliko Roho Mtakatifu .

🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂



πŸ’» 9 Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;

Isaya 30:9

10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;

Isaya 30:10

11 tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu.

Isaya 30:11

12 Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo;

Isaya 30:12


πŸ’« Ikisemwa kweli watu hunyamaza kimya kanisani na utaona nyuso za wengine zimebadilika sasa wakitoka wanaanza vikao .🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂



πŸ’«Ukiona Amen zimepungua ujue umepiga mioyo ya watu πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’« Ndyo wakitoka pale wanakusema Oooh mchungaji hana hekima katutukana yaani wamezoea masomo laini


Masomo ya faraja na kuwaambia watabarikiwa , mwaka huu wataolewa , watapata magari ,

πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’« Washarika hao , wakipigiwa simu na watumishi waongo mfano :


Wewe ni fulani ❓

Utasikia ndiyo baba


Halafu akiambiwa uchumi wako umeyumba sana kwa sababu jirani yako anakuroga

Sasa nitumie laki 3 nije tutengeneze kwa maombi .πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂

Hata kama hana atakopa kwa jirani 🀣🀣🀣🀣🀣🀣


πŸ’« Watu wanafikiria baraka tu hawaangalii uhusiano wao na Mungu ni mzuri au la !



πŸ’« Moyo uliofarakana na Mungu hautaki kuambiwa kweli ya Mungu .


πŸ’« Ivi unapigiwa simu utume kiasi fulani cha pesa uombewe baraka milango yako ya biashara ifunguke

Je si sawa na kwa waganga ❓

Hayo ni mafundisho ya mashetani yanataka kutawala mioyo ya watu


πŸ’» Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

1 Timotheo 4:1



πŸ’« Kanisa la Mungu tusome biblia kila siku bila kusoma neno na kuijua kweli tuyayumbishwa sana .



πŸ’« Nakumbuka siku moja nafundisha kuhusu dhambi ya uzinzi na uasherati watu wakawa hawaitikii , Amen 🀣🀣🀣 kanisa lilikuwa na huzuni sana siku hiyo na ningekuwa Stephano ningepigwa mawe maana ibada ilikuwa chungu sana kwa wapendwa
πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’» 13 Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;

Isaya 29:13



πŸ’« Watu ambao mioyo yao imefarakana na Mungu hupenda mafundisho mapotovu .



Ukiwaambia mwaka huu mtapata gari ungurumeni kama gari wataunguruma kanisa zima πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’« Imani yako isiyumbishwe yumbishwe simama imara katika imani yako .


πŸ’« Ndyo hawa wanavutwa kirahisi na kupotezwa .



πŸ’« Siku unakemea dhambi ukiona praise team kimya , wazee wa kanisa kimya ujue kanisa lipo vuguvugu .
πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’« Utasikia Bwana YESU asifiwe kumbe kinafiki anamitandao humo kanisani na baadhi yao wake za watu πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂na ni mwimbishaji mzuri sana kumbe



Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻


πŸ’« Ndiyo maana tunaona huko Afrika  Kusini kulizuka kanisa mnaenda kunywa pombe na mnayasoma na maandiko kabisa eti Mungu vyote kavibariki πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


πŸ’« Kwanini achukie kuonywa ❓ ni kwa sababu anamkiri Mungu kwa midomo yake lakini moyo wake upo mbali na Mungu .


 πŸ’» Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida.

Waebrania 13:9



πŸ’« Leo watu wanachukuliwa kirahisi na mafundisho ya uongo sijui wanatumia biblia ipi .πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



πŸ’« Ukifuatilia vizuri Mtu wa Mungu utagundua kwanini ukikemea watu wasijuane kabla ya ndoa vijana wanasema haiwezekani

Ni kwa sababu mioyo yao imefarakana na Mungu hawataki kuitii kweli ya Mungu .
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’» 28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Matendo ya Mitume 20:28

29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
Matendo ya Mitume 20:29

30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.

Matendo ya Mitume 20:30


πŸ’« Mtu wa Mungu tumekabidhiwa kundi la Kristo tuliongoze lisipotee lakini kulichunga hili kundi ni kazi inayohitaji uvumilivu maana ndani ya kanisa kuna wapinzani pia.


πŸ’« Ndiyo maana leo kijana anaibuka kidogo tu katika utumishi anakuwa na kiburi anajidai kakomaa kiroho na kumdharau mlezi wake wa kiroho
Anaenda kuanzisha kanisa lake .πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»


πŸ’« Tajiri hakemewi kisa anazo maana yake kanisa litakosa sadaka πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



 πŸ’« Makanisa kama hayo huwa na matatizo sana , hayakemei kisa watapunguza waumini .



πŸ’« Utasikia  , Ooh mwenye haki ajapo anguka mara saba atasimama tena , anguka tu hata mara miamoja maana Mungu ni mwenye rehema husamehe kabisa πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



πŸ’« Sasa haya mafundisho ya kuambizana kuanguka utainuka tena siyo kuchochea uovu ❓

Maana anaweza akadhamiria kutenda jambo lisilompendeza Mungu akidai atatubu akaja kufa kabla ya kutubu utakuwa umempalia moto wa jehanamu .



 πŸ’« Mtu wa Mungu labda tufundishe na masomo yanayohusu hatma ya mtu baada ya kifo .



πŸ’« Pale mtu anapokufa roho yake inaenda wapi ❓πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂

Kuzimu

Au Paradiso

πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



πŸ’« Kuzimu ni mahabusu ya roho za waovu ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Kuna mateso makali sana na ni pachafu hakufai huko .



πŸ’« Mtu anapokufa tu sekunde moja yupo kuzimu kama ni mwovu .



πŸ’» 9 Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.

Isaya 14:9

10 Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi!

Isaya 14:10

11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.
Isaya 14:11



 Kuzimu huko kuna funza na vidudu vikali na mateso

Sasa tunapowahuburi baraka tu bila kuwabia wajue kabisa


Yaan tunawafariji waendelee kuanguka watapotea sana .πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



πŸ’« Mwenye moyo wa kiburi mwambie kweli aijue , akishupaza shingo ni juu yake wewe umenawa mikono mbele za Mungu huna hatia .


πŸ’« Kuna kauli ambazo Mtu wa Mungu utazisikia kutoka kwa watu ambao mioyo yao imefarakana na Mungu .


✍🏻 Ina maana wewe ni Mtakatifu ❓


Hii kauli nzuri sana



Maana mbinguni wanaingia watakatifu na siyo wenye dhambi na kama hutaki kutubu na kuacha dhambi sahau kuhusu mbinguni .

🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂



 Mungu akubariki sana wewe uliye mtakatifu mwenzangu ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻


πŸ’« Nakutakia mchana mwema


Popote ulipo Mungu akuinue zaidi katika huduma yako .



🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*