π« ROHO YA UASI π*
π« ROHO YA UASI π*
Mwl. Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
roho ya uasi ni roho isiyotaka toba
π«mtu mwenye roho ya uasi hataki kukemewa .
π«mtu mwenye roho ya uasi ukimkemea umemtukana .
π« mtu mwenye roho ya uasi anapinga kweli ya Mungu anahalalisha dhambi.
π« Imekuwa kawaida kwa vijana wa kike kuvaa mavazi ya aibu wakiita fasheni bila kujua kuwa wanamwasi Mwenyezi Mungu .
π« Imekuwa jambo la kawaida kwa Vijana wa kike wakiwa na kazi basi hawatii waume zao tena wala kuomba samahani kwao hakuna kabisa .
Hii ni roho ya uasi
π« Hii roho ya uasi iliyoingia kwa vijana wa kike inawafanya wengi wao kuzeekea makanisani bila kuolewa kabisa .
π« Imekuwa ni desturi ya kawaida hata kwa vijana wa kiume kubebesha mimba na kutelekeza wanawake
Hii ni roho ya uasi .
π« Hii roho ya uasi inaukataa ukweli inafuata tamaa za mwili ikisingizia kufanya mapenzi kabla ya ndoa ni burudani .
π« Hii roho ya uasi inawafanya wakristo wafungishe ndoa huku wanamimba
π» 13 Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani;
Tito 1:13
14 wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli.
Tito 1:14
15 Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.
Tito 1:15
16 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
Tito 1:16
π« mtu mwenye roho ya uasi hataki kuthamini mawazo ya wenzake .
π« mtu mwenye roho ya uasi hawezi kujishusha hata kama kakosea
π«mtu mwenye roho ya uasi anakufanya wewe wa ziada kwenye mahusiano hana mda na wewe .
π» 2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
2 Timotheo 3:2
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
2 Timotheo 3:3
4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
2 Timotheo 3:4
π« mtu mwenye roho ya uasi anakiburi .
π« mtu mwenye roho ya uasi anapenda maisha ya anasa kuliko kumpenda Mungu .
Ukimwambia twende kwenye mkesha wa maombi hataki lakini anaenda kuangalia mechi za mpira usiku au anaangalia filamu akidai anajifunza kumbe ajitengenezea njia ya kwenda kuzimu .
π« mtu mwenye roho ya uasi hataki kuchangamana na wanaishika kweli ya Mungu
Yeye marafiki zake wengi hawajaokoka yaani watenda dhambi
π«Mkemee hata kama hataki kukemewa mkemee
π» 1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 Timotheo 4:1
2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
2 Timotheo 4:2
π«Nimeagizwa kukaripia na kukemea kwa mafundisho ya uzima sitaki mzaha
π« nichukie nichukie nitukane lakini ukweli umeupata
π« upo kanisani unasema Mungu haangalii mavazi wewe unaroho ya uasi .
π« Leo tunasafisha kanisa , tunatoa uchafu kanisani
π« wamekaa kanisani huku ni waasi wanaikataa kweli kwa kuhalalisha ujinga ( maovu).
π» Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
1 Yohana 2:19
π«Anajiita mpendwa lakini matendo yake hayanatofauti na wasioamini .
π« Wakristo feki ,Wakristo photocopy .
π« wanapenda nyimbo za dunia kuliko nyimbo zinazomtukuza Mungu , yaani ni waasi .
π« Hawasomi hata neno kazi kukaa yao ni kuleta mizaha kwenye neno la Mungu kwa kutaka kuingiza habari za dunia .
π« Waache kiburi watubu wamrudie Mungu
: π» 1 Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
Isaya 58:1
Mungu akubariki sana
Nakutakia siku njema
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni