SOMO: UFUNUO WA YESU KWA UTUME WA PAULO.π
π«SOMO: UFUNUO WA YESU KWA UTUME WA PAULO.π
Mwl. Magy Kazungu
JESUS CO_WORKERS MINISTRY
Kwa maana, ndugu zangu, injili hio niliyowahubiria , nawajulisha kuwa sio ya namna ya kibinadam, 12, Kwakuwa sikupokea kwa mwanadam wala sikufundishwa na mwanadam Bali kwa mfumo wa Yesu Kristo.
Injili aliyo ihubiri Paulo aliipokea kutoka kwa Mungu na alifundishwa na Mungu hivyo Mungu alijifunua kwake.
Tamani kupokea kutoka kwa Mungu ili uwafundishe watu , ukipokea kutoka kwa Mungu utapata vyote tena bila mashariti.
Mwanadam anaweza akakupa ila sio vyote, taMani kupokea kutoka kwa Mungu.
Unaweza ukajiuliza ilikuaje!!!!
Pamoja na Paulo kutenda uhalibifu Lakini Mungu alikua amemchagua kwa kazi yake, alimuita kwa NEEMA,
Sio kwa utashi wake waka kwa kutembea ktk mapokeo ya kibinadam na mapokeo ya baba zake
Usiiangalie historia ya nyuna na madhambi uliyowah kufanya Bali itazame NEEMA ya Kristo ktk maisha yako. NEEMA INA nguvu kuliko historia.
Ukiendelea mstari wa 16, utaona Mungu aliona vyema kumdhihirisha Kristo kwa Paulo ili Paulo amtumikie Mungu.
π Ili Paulo afanye kazi ya Mungu pasipo kushauliana na mwanadam
Paulo halufanya shauli na mwanadamu mwenye mwili na nyama ,
Kwasababu mwanadamu hakuwa na uwezo kwa kumshauli sawa na Mungu, ( ipasavyo).
Tamani Mungu akusaidie kuihubiri injili, akuelekeze yakupasayo kutenda.
Unapokwenda kwenye huduma usishauliane na mwanadam maana anaweza kukuvunja moyo au kukuzuia kulingana na mzingira
Utasikia huko wachawi wengi, mala nauli kubwa , utafikili umeitwa na yeye,
Kama utaogopa wachawi ni Mungu wa namna gani unayemtumikia,au ni Mungu yupi aliye kuita,
Tamani kusikia kutoka kwa Mungu, kama mtume Paulo
Kwa habari ya kazi ya Mungu simama pekeako usisimame na mtu maana mtu anaweza akaanguka mkaanguka wote.
Ukisoma mstari wa 17, Paulo hakwenda kule walikomitume wengine Bali alikwenda kule ambako Mungu alimuelekeza, alimsikiliza aliyemuita.
πTamani kuelekezwa na aliyekuita na kufanya vile anataka utafika mbali kwa habari ya huduma.
Mstari wa 21-,
Paulo alipokwenda shamu walisikia habari zake na kusema
Yule aliyetuudhi hapo mwanzo , sasa anaihubiri injili/Iman ile alioiharibu zamani
24,
Wakamtukuza Mungu kwaajir yake.
Mungu anapokuita na ukaachana na Matendo ya kale inatakiwa watu wakikuona wamuone Mungu uliyenae , wamtukuze Mungu kwaajir yako , Mungu ajitukuze ,
Wasiomlne uharibifu waione NEEMA ilioshushwa kwako.
Wagalatia 1:1-
Paulo, mtume, ( si mtume wa wanadamu Bali wa YESU Kristo na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu)
MATHAYO 16:17
Mwili na damu haviwezi kukufunulia siri za Mungu.
Bali Mungu ndiye awezaye kutufunulia siri zake.
Isaya 49:1,
Mungu ameku alikutambua na kukutenga kwa kazi yake toka tumboni kwa mama yako.
Mwanadamu ni nani hata azuie huduma yako,
πKama umeitwa na Mungu, kuna siri kubwa na mpango madhubuti kwa huduma yako.
Mungu alipokuchagua alikutenga kwa kazi yake
π usiruhusu mwanadamu akaingiza mpango wake katikati.
Tamani udhihirisho wa ki Mungu katika huduma na utumishi wako sio wa kibinadamu.
Yeremia 1:5
Mwanadamu anaweza kukuita majina mengi Lakini hakujui .
Mungu pekee ndiye akujuaye
Usitishwe na majina hayo liko jina moja ambalo Mungu hukuita
1Wakorintho 15:10
Paulo alitambua siri kubwa kwamba hivyo alivyo ni kwa NEEMA tu na maisha aliyonayo so hakuona haja ya kujivuna na kuona yeye ni wapekee sana pamoja na kua ni kweli Lakini aliiona NEEMA iliyomfunika.
Mitume waliotangulia walipita Lakini yeye alifanya kuwapita wote alifanya kazi sana Lakini sio kwa uweza wake Bali ni kwa NEEMA .
Tambua hilo adui asikuibie, tunatumika na kutenda kazi ya Mungu kwa NEEMA sio kwa akili na uweza wetu.
Matendo 9:3-6
Paulo alikutana na Mungu. Soma vizuri hapo
4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
Matendo ya Mitume 9 :4
5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
Matendo ya Mitume 9 :5
6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.
Matendo ya Mitume 9 :6
Tumuombe Mungu atupe nuru ya elimu kwa utukufu wake akang'ae ktk mioyo yetu
πTutembee na uwepo na nguvu zake
πTuwe na mamlaka ya ki Mungu katika huduma na utumishi aliotuitia
2wakorintho4:6
Kwakuwa Mungu aliyesema nuru itang'aa toka gizani ndiye aliyeng'aa mioyoni.....
Mungu alimpa maelekezo pauloya kwenda kuhubiri injili.
Paulo anapokea maagizo toka kwa Mungu sio mwanadamu
Matendo 22:21
Hivyo tutamani kristo ajifunue kwetu kama alivyojifunua kwa Paulo.
Tutamani kufundishwa na yeye na tusimame imara kwa kumtazama yeye aliyeiamzisha huduma ndani yetu.
Mungu awabariki sana kwa Leo tuishie hapo Mungu awabariki sana wapendwa.π€π€π€πππππͺπ½

Maoni
Chapisha Maoni