UCHUMI KIBIBLIA
UCHUMI KIBIBLIA
Mwl. Pastor Peter Sponga
from Bahi _ Dodoma
💻 17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
Kumbukumbu la Torati 8:17
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 8:18
Uchumi kibiblia ulijulikana kama utajiri au umiliki wa mali
Nikijaribu kutafsiri Uchumi naweza kusema ni hali bora ya umiliki wa mapato na mali na kumiliki vyanzo imara vya mapato
Tunaona katika mwanzo Mungu anamilikisha adamu Mali ili amiliki
Anampa Ardhi watataalamu wanaiita mali isiyoondosheka
8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
Mwanzo 2 :8
9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Mwanzo 2 :9
15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Mwanzo 2 :15
Kwahiyo unaweza ukaona kuwa asili ya uchumi ni Mungu mwwnyewe kwahiyo Bwana anaposema usijitape kuwa ni kwa akili zako anamanisha kuwa bila yeye hatuwezi
UCHUMI HAPO ZAMANI
Ulihesabiwa kwa kiasi cha mavuno na kiasi cha mifugo uliyo nayo
Tunaanza kuona Habili akifuga na kaini akilima mazao
Soma mwanzo 4:2,3
Unatakiwa kujua na kukumbuka siku zote kuwa wewe si wakwanza kumiliki mali na vyanzo vya mapato maana Mungu aliwahi kuifuta Dunia yote na akamuacha Nuhu tu na familia yake
Kwahiyo katika yote tuliyo nayo ni kwaneema tu ya Bwana
Angalia Bwana anaahidi kumuinua Ibarahimu na kumfanya baba wa mataifa
Utajiri na uchumi unahesabiwa kwa idadi ya watuulio
Ibrahimu pamoja na kuwa hakuwa na watoto lakini alikuwa na mifugo hadi malisho yakawa hayatoshi
Alikuwa na watumwa hadi akatengeneza jeshi
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Mwanzo 12 :2
16 Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda wake, na ngamia.
Mwanzo 12 :16
Tunapoona Marekani na China zinataka kutawala Dunia ni ahadi kibiblia Mwenye uchumi mkubwa ndiyo huwa Mkubw
Hapa uchumi wa Ibrahimu unahesabiwa kwa wingi wa kondoo,vijakazi,watumwa, ngombe,punda na ngamia
Tunaona Ibrahimu sasa baada ya kutoka Misri utajiri wake uNahesabika kwa fedha na dhahabu na mifugo
2 Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.
Mwanzo 13 :2
Waswahili wanasema ukitaka kujua tabia ya Mtu subiri apate mali au uchumi bora
Ukitaka kujua tabia ya mke filisika
Kumb 8:18 usisahau kuwa chanzo cha hayo yote ni Mungu wako aliyekuumba
Bwana anapenda
1. Watu wenye shukrani
2. Wanyenyekevu
3.watii
4. Wasio na tamaa
5. Watoaaji
Habili, Nuhu, Ibrahimu ,isaka kila baada ya muujiza na mafanikio walimtolea Mungu wao dhabihu
15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski.
Mwanzo 14 :15
18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
Mwanzo 14 :18
19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
Mwanzo 14 :19
20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Mwanzo 14 :20
Abrahamu anatoakikumi
Wewe unayetaka kufanikiwa kibiblia kwa mafanikio hayo kidogo uliyoyapata umemtolea nini Mungu
Umetoa nini katika madhabahu unayoshiriki ibada kila mara
Umefanya nini kwa makuhani wake
Ukisoma habari za watakatifu hawa utasikia akajenga madhabahu akatoa sadaka
BWANA NDIO ANAYETOA AKILI ZA KUPATA UTAJIRI
: 1 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.
Mwanzo 26 :1
2 Bwana akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.
Mwanzo 26 :2
3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.
Mwanzo 26 :3
4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
Huwezi kupata akili kutoka kwa Bwana kama humfuati umtafuti hutaki kutii
Huwezibkufanikiwa kibiblia kama unatamani mali za mataifa na kuishi kwa kukariri
Bwana anamweleza isaka baba yako alienda Misri wakati wa njaa wewe usiende huko naweka AGANO NAWE NA LILE LA BABA YAKO LITADUMU UKISHIKA MAAGIZO YANGU
nenda kwa abimeleki huko ndio kuna utajiri na uchumi wako kuboreka zaidi
ANGALIA AKILI ALIZOPEISA
12 Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki.
Mwanzo 26 :12
13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.
Mwanzo 26 :13
14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.
Mwanzo 26 :14
15 Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi.
Mwanzo 26 :15
16 Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi.
Mwanzo 26 :16
BWANA ANAMWAMBIA usitegemee urithi tengenezA pesa na mali zaidi akapanda mbegu
Kama si kutoka kwa Bwana kwanini wenyeji hawakupanda na sasa wanaona wivu
: Anakumbushwa visima vya baba yake anazidishwa na kuwa mkubwa hadi anafukuzwa
Ukisoma mbele abimeleki na watu wake wanapatana naye ili asije akawaua maana anauchumi mkubwa hadi anati
*PESA ZA WAPAGANI NA WAABUDU MASHETANI ZISIKUTAMANISHE NI ZA MUDA NA NI ZA MAZINGAOMBWE HAZIDUMU LEO ZIPO KESHO ZINATOWEKA NA WEWE UNATOWEKA NI ZA MAANGAMIZO YAO NA YA KUPROMOTE UOVU DUNIANI*
24 Bwana akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.
Mwanzo 26 :24
25 Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko.
Mwanzo 26 :25
26 Ndipo Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli, jemadari wa jeshi lake.
Mwanzo 26 :26
27 Isaka akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi mmenichukia, mkanifukuza kwenu?
Mwanzo 26 :27
28 Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba Bwana alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya mapatano nawe
Mwanzo 26 :28
29 ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u mbarikiwa wa Bwana.
Mwanzo 26 :29
ANGALIA MALI ZA AYOUB ZILIONDOKA NA ZIKARUDI DOUBLE DOUBLE
1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
Ayubu 1 :1
2 Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu.
Ayubu 1 :2
3 Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
Ayubu 1 :3
Kwaajili ya kuiga mataifa ndio maana mtu akifanikiwa kidogo anaona FAMILIA YAKE WATU WA KANISANI WASHAMBA ANAAPUUZA MAOMBI KANISA NA WATUMISHI
*HILI NI PEPO LA KISASA
Ayubu alimpendeza Mungu kwa sababu kuu mbili
1 alikuwa na sifa zote nilizosema hapo juu
2. Alitumia malizake kujipatanisha yeye na familia yake na huyu Mungu mtakatifu
HUWEZI KUDUMU KATIKA UCHUMI BORA KAMA UNACHUKULIWA NA MALI KIASI CHA KUMUACHA MUNGU
Pamoja na majanga yote hayo na shutuma za marafiki aliendelea kuamini
ULISHAWAHI KUTULIA NA KUHESABU HELA ZILIZOPITA MIKONONI MWAKO NI NGAPI??
HUJIULIZI KWANINI WENYEKIPATO KIDOGO KULIKO WEWE WANAENDELEA KWA KASI??
*SHIDA NI KUWA KILA UKIPATA MALI NA TABIA YAKO INABADILIKA KUHUSU HUYU MUNGU
Badilika leo na Mungu atakusaidia
Kuyumba kibiashara na liuchumi ni jambo la kawaida . Hakikisha kiimani huteteleki ndipo baada ya dhaluba hiyo utaimarika zaidi ya mwanzo
5 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.
Ayubu 42 :5
6 Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu.
Ayubu 42 :6
7 Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
Ayubu 42 :7
10 Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.
Ayubu 42 :10
11 Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.
Ayubu 42 :11
12 Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu, na punda wake elfu.
Ayubu 42 :12
13 Tena alikuwa na wana waume saba, na binti watatu.
Ayubu 42 :13
*USIGOMBANE NA BWANA KISA GARI MOJA WAKATI AMEPANGA KUKUPATIA MAGARI 20*
Usigombanena mwalimu kisa katunga mtihani mgumu
*USIGOMBANE NA BWANA KISA JARIBU UNALOPITIA*
ENDELEA KUMSIKILIZA BWANA DAIMA
1. ATAKUSAMEHE NA KUKURUDISHA KWENYE KITI NA UCHUMI WAKO NA KUZIDI
2. ATAONDOKA UTEKA WAKO
3.ATAKUREJESHEA MALI ZAIDI
4. ATAREJESHA FAMILIA YAKO
5.ATAREJESHA MARAFIKI NA NDUGU
6.ATAREJESHA YOTE
💻 17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
Kumbukumbu la Torati 8:17
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 8:18
Tafuta AKILI NA NGUVU kutoka kwa Bwana naye atakufanikisha .
Kama umekosema tumia elimu hii kurejea kwa Bwana yasije yakakukuta ya TAJIRI MPUMBAVU, ANANIA NA SAFIRA NA YA HERODE
16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
Luka 12 :16
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
Luka 12 :17
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
Luka 12 :18
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
Luka 12 :19
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Luka 12 :20
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.
Luka 12 :21
22 Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini.
Luka 12 :22
23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
Luka 12 :23
*KABLA YA KITU CHOCHOTE UCHUMI UKIIMARIKA MPE BWANA HESHIMA UTUKUFU NA SHUKRANI KISHA ENDELEA NA RAHA ZAKO*
2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
Matendo ya Mitume 5 :2
3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Matendo ya Mitume 5 :3
4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.
Matendo ya Mitume 5 :4
5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.
Matendo ya Mitume 5 :5
*ANNANIA ANAPOZWA NA HELA YA KIWANJA WATU WANAACHA YESU KWAAJIRI YA SMARTPHONE AJIRA KAZINI MWISHO WANAKUFA KIBUDU*
21 Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao.
Matendo ya Mitume 12 :21
22 Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu.
Matendo ya Mitume 12 :22
23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho.
Matendo ya Mitume 12 :23
*KIBIBLIA MUNGU AKITAKA UFANIKIWE KIUCHUMI ANAWEZA KUKUINUA KUPITIA CHEO. HATA UNAPOPATA CHEO USIMKUFURU WALA KUMSAHAU MUNGU
MUNGU AWABARIKI SANA KWA SOMO HILI
NAWAPENDA NI MIMI KIBARUA WA BWANA
Pastor Peter Sponga
Maoni
Chapisha Maoni