UKWELI KUHUSU NDOA
UKWELI KUHUSU NDOA
SWALI: JE NI HALALI KUVUNJA NDOA IKIWA MUME HANA NGUVU ZA KIUME ?
Majibu :
Pastor Peter Sponga A.
From Bahi _ Dodoma
JESUS CO_WORKERS MINISTRY
Hiyo inavunjwa ndoa ni tendo kwanza mengine ni mbwembwe
Kanisa linakaa na kuvunja
Tatizo likimpata akiwa kwenye ndoa huo ni msalaba wako inabidi uubebe
Japo ni nguvu ya kanisa kuamua maana tokea zamani wasioweza tendo la ndoa walijulikana mapema na hawakuruhusiwa kuoa
Kwahiyo Biblia iko kimya sasa kama huwezi kumpa binti haki yake na ulizaliwa hivyo haiwezekani
Umeonja vya moto vyabaridi vyenye chachu vikavu vibichi halafu kisaikolojia uwe fiti labda uwe umepondwa pondwa na huyu Yesu vinginevyo utaona ndoa ni PINGU PINGUA NA WOKOVU JOKOFU
Kweli na shida leo madhehebu wachungaji vijana
Group wengi vijana
Mtu anazaliwa mpaka anakua anaishi na vijana
Mengi ya mambo ya chumbani nguvu za kiume yalimalizwa na mababu zamani
Mnafundishana kwa video za ngono
Unataka ujifunze mpira wa Miguu kwa kuangalia mechi Messi akiwa anawapita mabeki??
Unajua chenga hiyo kajifunza kwa miaka mingapi??
Vijana ukiwaambia unaswali hawana
Kuna tatizo wanakuambia pambana na hali yako
Binti anaingia kwenye ndoa anafikili ndoa ninvicheko tu akinuniwa siku moja anapost whataap jamani nisaidieni baby kanuna
Anapost video analia baby hajanichumu leo si nivituko hivi
Watu tunachati nanyi tunaomba tuna hudumu kumbe usiku nilipigwa kipepsi lakini tulifundwa
Tumebahatika wwnzenu kukaa na wazee vijijini na mijini wazee ndio rafiki zetu
Leo vijana wanaamini kila mzee ni mchawi
Leo mnaingia kwenye ndoa kila mtu anabullet proof kwenye akili ndoa umeambiwa ni uwanja wakujaribisha silaha ulizo nazo
Ndoa ni paradiso ndogo ndio maana ulipewa raha huwa unasahau shida zako na kupitiwa na usingizi mwororo
Kila kabila lina ubora mitindo na udhaifu katika mambo ya familia na katika ubora wa tendo la ndoa
Kuna makabila tendo ndio muhimili wa ndoa lakini makabila mengine ni kiburudisho tu sawa na juice baada ya kula hata kama hakuna ni sawa tu
Kuna kabila ukienda kuoa utaomba pooo lakini mengine kila ukitaka mpaka upige magoti au uandike barua ya maombi uambatanishe na zawadi na picha
Kunamakabila baba mkwe alitaka lazima umpe maana mke ni mali ya ukoo
Kuna makabila baba akioakabinti saizi yako unaruhusiwa kuingia mara moja moja na mtoto akizaliwa anakuwa mdogo wako
Sasa ktika mazingira haya ambayo watu tumekutana kanisani usione kila anayenena kwa lugha ni mkristo wengine bado mila hawajaacha
FANYA YAFUATAYO
1.Amin Mungu anaweza kukupatia mwenza mwema
2.omba Mungu akupe wa kwako , wamaisha yako, unayemmudu, atakaye kupa raha hadi uzee
3.tulia mngoje Bwana maana hakawii wala hawahi
4. Kuwa mtii kufuata maelekezo kuelekea kwenye ndoa
5. Kuwa tayari kurekebisha vigezo vya mwenza uliyemtaka linapokuja swala la kumsubiri Bwana
6. Kumbuka wakati wakuanza familia ulishapangwa ukifika usijizuie anza Bwana ameshaweka tayari unavyoviona na visivyoonekana kwajili ya familia hiyo.
Ukiwahi au ukichelewa utajipigania mwenyewe
7. Ndoa ni shule kamili hatakama ulikuwa mwalimu wa wanandoa kabla ya kuoa ulishaanza ndoa kubali kuanza CHEKECHEA
KUMBUKA NDOA
1+1=1 ni jibu linaloweza kutolewa na mwanafunzi wa chekechea pekee
Mwisho
KUMBUKA SIKU ZOTE KUJITOLEA KWAAJILI YA MWENZIO NA KUTAMANI KUJUA HISIA ZA MWENZA WAKO JUU YAKO
Kama huamini kuwa ndoa ni hatma yako usiolewe utajinajisi tu
Wanaume tujenge mazingira ya kusikiliza wachumba wetu na tuwatoe mashaka yote yanayowasibu kabla ya kuingia katika ndoa
Mwanamke ni ngumu kuishi mpk uzee bila kuolewa wala kupata mtoto kuliko mwanaume. Kwa nn.?
Tafadhali wakaka tuache tabia ya kuwateka wasichana
Unamkuta mkaka anatawala mawazo ya msichana na kumfanya zezeta unamfanya kama simu hutaki kusikia mawazo yake
Kumbuka unaweza kudanganya na kutawala kila mara lakini hutoweza kutawala na kudanganya siku zote
Wadada acheni mawazo hasi kuhusu ndoa bado mabikira wapo kuanzia wamwili hadi wa fikra
Mpokeee mtu ambaye unadhani anastahili kuwa mfalme wako ili akufanye kuwa malkia
Kumbuka ndoa inalenga kujenga himaya ukoo siyo eneo la pikiniki au kujirusha.
Usipowekeza vya kutosha katika ndoa yako hakuna atakaye kusaidia
Unaporuhusu mtu asiyehusika kuwa muhimili wa ndoa yenu hata kama unaona leo anawafaa sana au anakufaa sana tambua kuwa ndoa yako haitadumu
Jitahidi kuwa na muda wa kutosha wa mijadala na mwenza wako ili mjenge mifumo yenu katika mambo haya.
1. Mtafunga ndoa ya aina gani
2.mtaishi maisha kwa mfumo gani wa kiroho kimila au kisayansi
3.mtaishi wapi
4.mnawategemezi wangapi na mtawasaidiaje
5. Mtazaa watoto wangapi na majina yao yatapatikanaje
6. Ajira itakuwaje ,kiuchumi mtashirikianaje, uhifadhi wa mali.
7. Anataka zaidi ya kuwa mwenza uwe nani wake, mwalimu ,mzazi, mlezi ,mshauri nk
8.kubalianeni namna ya kupeana raha zenu. Mf. Ukinikwaza omba radhi .
Au usiku ukiona sina nguo ujue natakaππππ
Tutasali wapi??
Kumbuka mawazo na milengo tofauti katika ndoa ndio uharibifu wenu wamali na wawatoto
Mungu awabariki siwezi kumaliza
Nawapenda
Pastor Sponga Peter A.
Maoni
Chapisha Maoni