UKWELI KUHUSU ROHO MTAKATIFU

πŸ’’ UKWELI KUHUSU ROHO MTAKATIFU πŸ’’*





Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

SAUTI YA MUNGU MINISTRY




πŸ’« Roho Mtakatifu ni nani ❓


πŸ‘‰πŸ» Ni Mungu katika nafsi ya tatu ambaye anafanya ushirika na mtu amwaminiye Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake ili afanyike kuwa raia wa ufalme wa mbinguni ( mrithi wa uzima wa milele ).



πŸ’« Roho Mtakatifu kwa aliyeokoka ni wamuhimu sana kumjua



πŸ’» Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

Isaya 6:3



πŸ’«Roho Mtakatifu ni mtakatifu maana yake hachangamani na uchafu wowote .



 πŸ’« Katika kitabu cha Isaya 6:3  tunaona neno Mtakatifu limerudiwa mara tatu .yaani



πŸ‘‰πŸ» Mtakatifu , Mtakatifu , Mtakatifu


✍🏻 Maana yake ni


1⃣ Mtakatifu -Mungu baba

2⃣ Mtakatifu - Mungu mwana

na


3⃣ Mtakatifu - Roho Mtakatifu .



 πŸ’« Roho Mtakatifu akikaa ndani ya mtu , hubadilisha mfumo mzima wa maisha yake .



 πŸ’«Roho Mtakatifu hubadilisha mfumo wa imani .


πŸ’«Roho Mtakatifu akifanya makao ndani ya mtu humpa nguvu ya kushinda dhambi ( tamaa za mwili ).



πŸ’» Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

Wagalatia 5:16



πŸ’« Roho Mtakatifu akitulia ndani ya mtu humpa maarifa na hekima .



πŸ’» 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;

1 Wakorintho 12:8



πŸ’« Roho Mtakatifu ni maji ya uzima wa milele



πŸ’» 13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

Yohana 4:13

14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

Yohana 4:14



πŸ’«Yesu alikuwa akizungumza kwa habari ya Roho Mtakatifu



 πŸ’«Roho Mtakatifu anatutua nguvu za kumshinda shetani ( upako wa kumshinda shetani ).


πŸ’» 1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

Isaya 61:1

2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;

Isaya 61:2

3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.

Isaya 61:3



πŸ’« Upako wa Roho Mtakatifu unatupa nguvu ya kuamuru watu wawekwe huru kutoka kwenye vifungo vya ibilisi .



πŸ’» 38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

Matendo ya Mitume 10:38
 Mungu akubariki sana
[5/11, 08:34] Rev.Peter Francis Masanja: https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*