π« URAFIKIπ UCHUMBA na NDOAπͺ
π« URAFIKIπ UCHUMBA na NDOAπͺ*
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SIKU YA KWANZA
SOMO :
π« KANUNI ZA KUMPATA MWENZI SAHIHI WA MAISHA YAKO π
π« Kijana uliyeokoka na upo ndani ya Yesu sawawa πͺπ»
ππ» Tafuta kwanza kujijua wewe jinsi ulivyo
π« Angalia uhusiano wako na Mungu kisha uulingalishe uhusiano wako na Mungu na yule unayemtarajia .
π» 3 Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
Amosi 3:3
π« kama vitu vingi sana umepishana naye ahirisha mkataba wa mahusiano .
π« Ili uweze kufikia malengo ya urafiki au Uchumba ulionao usikubali kila mtu awe kampani yako .
π« Vijana wengi wamejikuta wanapoteza wachumba zao kwa kuwasikiliza watu kuliko kumsikiliza Mungu .
π« Kaa karibu na watu wanaokaa katika uwepo wa Mungu
π«Usikae na watu ambao wanakaa barazani wataua uchumba wako mapema sana .
π« Kijana hukuletwa duniani kuchaguliwa nani wa kumuoa , umeletwa duniani kumsikiliza Mungu anataka umuoe nani .
π« Kwanini mtu akwambie unataka kuolewa au kuoa mtu na sura mbaya ❓
Huyo anayekwambia mchumba wako mbaya huyo macho yake yameharibika akapimwe ✍π»✍π»✍π»✍π»
π« Ndoto zako za nani utamuoa au atakuoa zisikatishwe na marafiki zako .
π« Ukiona mwanamke au mwanaume anadai ngono kabla ya ndoa mkimbie huyo hakufai kabisa .
π« Binti yangu nataka nikupe siri hii hapa
ππ» Ukitaka kumshinda mwanaume mtizame usoni mwulize shida yake ukiwa umejiamini kabisa .Utamwona amekosa hata cha kuongea na kuanza hadithi zingine zisizoeleweka .
π« Urafiki na Uchumba unahitaji nguvu ili uweze kuujenga .
π» 29 Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
Mithali 20:29
π« Kijana lazima uwe na nguvu za kufikiri na kupambanua mambo na kumjua Mungu kama kina Yusufu., Timotheo , Shadrack , Meshaki , Abedinego , n.k
π«Ukiwa na mtu katika Urafiki au katika Uchumba uwe na nguvu au uwezo wa kupambanua mambo anayoyafanya mtu wako ukijiangalia wewe na Mungu unayemtumikia kisha jiulize huyo mtu anakufaa ❓
π«Vijana wengi wanajikuta wanakufa kiroho kabisa kwa kuwa na wachumba ambao hawafanani nao .
π«UNAPOMPATA MCHUMBA / RAFIKI JIULIZE MASWALI HAYA ❓
1⃣ Kuna faida yoyote nitakayoipata katika uhusiano huu ❓
ππ» Uchumba usiokuweka karibu na Mungu hauna faida kabisa .
2⃣ Ni marafiki wa aina gani alionao ❓
ππ» Kama hawamleti karibu na Mungu ( wapotoshaji ) .
Achana na mtu huyo.
3⃣ Anampenda Mungu kweli au anajifanya ameokoka ili akunase ❓
ππ» Mwulize kaokoka lini .
4⃣ Yupo tayari nifahamu yote juu yake ❓
ππ» Kama hayupo tayari huyo hakufai .
5⃣ Ananipenda kweli au anapenda kitu ( vitu ) fulani kutoka kwangu ❓
ππ» Maana unaweza ukadhani unapendwa kumbe unatakwa tu
π« Vijana wengi walioumia walitakwa hawakupendwa
ππ» Kutakwa maana yake ni mtu kuwa nawewe kwa sababu unavitu fulani anavitaka bila vitu hivyo asingekupenda kamwe .ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂
ππ» Binti za watu wamejikuta wanalizwa kwa kuanishwa kuwa wataolewa na kuwaruhusu wanaume wawaguse kabla ya ndoa , na matokeo yake kuchokwa na kuachika .
ππ» Mchumba siyo mume mpaka akuguse kabla ya ndoa ,
Tambua mwili wako ni kwaajili ya mumeo na siyo kwa ajili ya mchumba wala rafiki .
π«Mwili wako ni mali ya Kristo na kwaajili ya mumeo na siyo mchumba wako .
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
π» 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
1 Wakorintho 6:18
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
1 Wakorintho 6:19
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
1 Wakorintho 6:20
π« Kuna jambo pia naomba niliweke wazi kwa vijana wenzangu leo ambao hawajaoa au kuolewa .
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
π« Vijana msifanye maamuzi haraka sana na kuwaaminisha watu kwamba ndiyo wanawafaa kuwa ndyo wametoka kwa Mungu .
π« Vijana wengi leo wanaona kabisa Mungu anawaambia huyu hakufai lakini hawataki kumsikiliza kabisa .
π« Sikilizeni kwa makini vijana labda ufahamu wenu utafumbuka leo
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
π« Kitu cha msingi kabisa katika kumpata mwenzi sahihi wa maisha yako
ππ» Amjue Mungu na kuisimamia kweli ya Mungu
ππ» Awe ameokoka kiroho na kimwili ( uvaaji wake ).
ππ» Sikuhizi wokovu wa midomo bila matendo umejaa makanisani kwahiyo kijana akikuambia kaokoka siyo kwamba kaokoka kweli inabidi ufuatilie sana huo wokovu wake upo viwango gani .
π« Wokovu unavipimo vijana , usishangae kuja kumgundua mtu anamiaka mitano katika wokovu hajui kufungua biblia lakini magazeti ya udaku anayajua sana tu
ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂
π« Unaona mtu anajua waimbaji wengi wa nyimbo za kidunia kuliko wanaoimba nyimbo za Mungu halafu nawewe unajifariji umepata bwana bila kujua unaolewa ukaabudu sanamu .ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂
π« Simu yake imejaa video za bongo fleva , na siku nzima yeye kuzungumzia wasanii wa bongofleva aiseee huna mume au mke hapo atakuua kiroho .
π« Usishangae akikuta wewe umeweka wimbo wa kwaya kwenye runinga anakuja kuutoa na kuweka bongo fleva
π« Haya mambo vijana huonyesha mapema sana wanayapuuzia kabisa
π« Wanaonyeshwa kwenye
1⃣ Uvaaji
ππ» Vimini, Vijikaptura, Vijisuruali, milegezo na vijisuruali vya kuvulia sabuni kwa wanaume .
2⃣ Nyimbo na videos
ππ» Videos za nusu uchi ( bongo fleva )
3⃣ Mengineyo yasiyomtukuza Mungu
π« Mtu uliye naye wewe kijana uliyeokoka kama hataki kuyaacha haya huyo hakufai
Hapa vijana wengi waliookoka wamejikuta wanaingia motoni huku wanaona kabisa lakini wanajifanya hawaoni .
π« Oooh mtumishi jamani nina mtu wangu nampenda lakini hapendi mambo ya Mungu nifanyaje ❓
ππ» Huyo ni mpinga Kristo achana naye kabisa
Na aina ya watu huwaomba wadada wawatumie picha za kuonyesha miili yao
[π«Mungu akubariki sana
Tukutane siku nyingine
π«πππππππ
HITIMISHO
Usiamue kimwili katika Uchumba amua kiroho
Na ukiona mtu wako hapendi mambo ya Mungu na kuitii sheria za Mungu huyo siyo mwema kwako .
Maoni
Chapisha Maoni