URAFIKI πUCHUMBA na NDOA πͺ
π«URAFIKI πUCHUMBA na NDOA πͺ
SIKU YA PILI
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
*π« IMARISHA UCHUMBA AU NDOA YAKO KWA MAWASILIANO MAZURI π*
π« Siyo kwamba huyo uliyenaye ametulia kwako kwasababu ya uzuri wako au haoni wengine wazuri kuliko wewe.
ππ» Ametulia kwa sababu unaongea naye vizuri .
ππ» Kama utabisha jaribu kuongea naye kwa ukali uone kama atabaki kwako .
Nakuhakikishia hatatamani tena kuwa nawewe na kama ndye ni mchumba ataanza kuandaa mazingira ya kukuacha kabisa I'll asije kufunga nawewe ndoa ukampeleka jehanamu .
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
π« Unaweza kujiona unamikosi na kwamba umelaaniwa kisa kila mwanaume au mwanamke anaye kuja kwako anakukimbia kumbe uongeaji wako unawafanya wachumba wakukimbie kabisa
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
π« Uchumba mwingi unavunjika kwa sababu ya mazungumzo mabaya , ( majibizano ya kiburi ).
π«Embu tuangalie namna unavyotakiwa kuongea na mtu wako ili mfikie malengo yenu .
1⃣ Utulivu na busara.
π» 1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Mithali 15:1
2 Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
Mithali 15:2
π« Busara katika mazungumzo huleta amani , furaha na kuongeza upendo zaidi .
ππ» Majibu ya upole na busara yanamfanya mtu wako awe wako peke yako
Atatulia kwako hatatamani kupenda kwingine .
ππ» Siku zote biblia imeweka wazi kabisa kuwa mwanamke ndiye kila kitu katika familia
Mke akikujibu majibu mabaya kipindi cha uchumba tu kwenye ndoa ni kilio
π« Mwanaume hujenga nyumba tu zikaonekana kwa watu lakini ni kazi ya mwanamke kuzifanya nyumba zilizojengwa au walizojenga na mumewe kuzifanya paitwe nyumbani .
ππ» Maana yake ni kwamba ili paitwe nyumbani lazima mke awe na busara na upole kwa mumewe na watu wengine pia .
ππ» Hapo atawafanya watu watamani kurudi tena .
ππ» Unafukiri kwanini marafiki za mume wako wanawasimulia watu kuwa fulani kaoa mke kweli kweli ?
Ni kwa sababu nyumba hupendezeshwa na kuvutiwa na mke mwenye busara na upole .
π« wewe binti uliye kwenye uchumba usiseme kwamba yule uliyenaye humheshimu unamjibu utakavyo kisa hajakuoa .
ππ» Majibu yako kabla ya ndoa ni majibu yako ndani ya ndoa .
π« Uwe na busara kabla ya ndoa na ndani ya ndoa pia hapo utaitwa mke mwema .
ππ» Angalia wanawake kama Debora nabii mke alikuwa mwanamke mwenye busara sana .
Waamuzi 4:4
Mwenendo huo ufuate uimarishe Uchumba au ndoa yako .
2⃣ Lugha nzuri
π» 18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
Mithali 15:18
π« Lugha mbaya huvunja mahusiano ya vijana wengi , hasa wengine wamejikuta wanajuta kuwapoteza watu wao kwa sababu ya majibu mabaya .
Majibu ya hasira ,na kujikuta wanaambizana mimi nawewe basi tena .
π« Dumisha Uchumba wako au ndoa yako kwa mazungumzo mazuri epuka hasira .Hasira hupelekea maamuzi feki .
3⃣ Uwazi
π« Uchumba mwingi na ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya kuwekana wazi.
π« Taarifa ni muhimu sana katika Uchumba au ndoa taarifa huondoa kutokuaminiana .
Taarifa huondoa mashaka
π« Taarifa huuzima uongo
π» 7 Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.
Mithali 15:7
π« kuna wachumba wengi na wanandoa utamkuta yupo busy siku tatu haongei na mtu wake wala sms hakuna na akija kuwa huru majibu ya mikato
Nilikuwa busy π¨π¨π¨π¨ hakuna cha samahani
Watu wa aina hii hujikuta wanaharibu bila kujua .
π« kunawengine siyo wawazi kwa maana ya kwamba wanawatu wengine pembeni licha ya kuwa na mchumba au mwenzi wa ndoa .
Hii husababisha kudharauliana kwa wachumba au wanandoa .
π» 32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Mithali 6:32
33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
Mithali 6:33
π« Mtu asipokuweka wazi ni mbaya sana maishani mwako hasa ukija kugundua aliyokuficha .
Heshima ya mtu humwondoka siku moja tu na ndiyo maana utasikia anaulizwa ,
Kumbe ndiyo maisha tabia yako hii , mbona ulinificha ?
π« Kuwa mwazi kwenye uchumba au ndoa acha kuwa kigeugeu , mara unamtoto , mara huna kuwa mwazi .
4⃣ Kusikilizana
π« Katika Uchumba au ndoa lazima msikilizane , msiposikilizana amani hupotea na upendo hupotea kabsa .
π» 38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Luka 6:38
π« Msikilize mwenzako ili ajione wa thamani kwako na ajivunie kuwa na wewe
π«Usitake kila mda usikilizwe wewe tu mwache na mwenzako aongee umsikie anajua nini kuhusu mada mnayozungumzia .
Usimwone kuwa hajui kitu kama utamwona hajui kitu maana yake nawewe hujui kwanini unaye .
π«Sasa usipomruhusu nayeye aongee maana yake hutambui thamani yake kwako na hii itapelekea kuharibu mahusiano kwa sababu atajihisi unamdharau .
π« Ulishawahi kuona familia baba ndiye mwongeaji hataki ushauri wa mkewake hata kama ni wa maana ❓
Utamsikia mama anasema
Mmmmh waacheni wajuaji waongee π€£π€£
Hapa mama amekata tamaa na ndoa mpaka anatamani Mungu ashuke atangaze kuanzia leo Ruksa kuachana na kuolewa kwingine
ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂
5⃣ Ukweli
π«Katika Uchumba na ndoa ukweli ni jambo la maana sana.
π« Epukeni uongo na visingizio
π«Utakuta mchumba wako anakwambia baby leo naomba usinipigie simu ninaenda mjini kunakazi fulani naenda kuifanya
ππ»♂ Kumbe anaenda kukutana na bwana wake mwingine
Na kunasiku utashangaa anamimba na cha ajabu zaidi akigundua anamimba ndogo anakuchoresha akunase mzini asingizie yako .
π« Mume naye anaaga anaenda semina wiki moja kumbe ameenda kutulia gest na hawara yake .ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂
Kuwa mkweli utaponya Uchumba au ndoa yako .
π» 17 Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya.
Mithali 13:17
π« Hakikisha unakuwa mkweli epuka uongo uongo wako utakuumbua siku za mbele .
π» 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.
Waefeso 4:15
16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Waefeso 4:16
17 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao;
Waefeso 4:17
π« Ukweli unaokoa
π« Uchumba wako au ndoa yako huimarishwa kwa kuwa mkweli .
6⃣ Kuomba msamaha ( Kujishusha )
π« Umeenda kinyume kubali kosa lako na kusema samahani mpenzi naomba unisamehe .
Acha kuja juu kujifanya hutambui kosa lako utaharibu
π«Vijana wengi wamejikuta waneharibu k
π«Hakuna mwanaume anayeoa mwanamke mkali asiyejishusha
HITIMISHO
Jenga Urafiki , Uchumba au ndoa yako kwa mazungumzo mazuri
Ili umfanye mwenzi wako akutulie kwako na kukuamini
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni