π« URAFIKI πUCHUMBA na NDOA
π« URAFIKI πUCHUMBA na NDOA πͺ
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
*π« KUFANYIKA KUWA MUME MWEMA* π·
π«. Ili uwe mume wa kumfurahisha mkewako lazima ujue wajibu wako kabla ya ndoa na ndani ya ndoa pia .
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
π« Ipo faida kubwa sana kwa mwanaume kutambua wajibu wake katika Uchumba au ndoa .
π« Hakuna kitu kizuri kama kuwa mume wa kuigwa katika jamii inayokuzunguka
π« Sasa tuangalie mambo yanayomfanya mwanaume aitwe mume mwema .
1⃣ Kumpenda mke wake
π« Jambo la kumpenda mke wako linaanzia kwenye kipindi cha Uchumba .
Usisubirie uonyeshe upendo ndani ya ndoa utafeli
π« Wanaowapenda wake zao na kuishi kwa furaha waliwapendea kwenye urafiki na uchumba kisha kwenye ndoa ni maboresho ya kuupalilia upendo .
π» 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Waefeso 5:25
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
Waefeso 5:26
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Waefeso 5:27
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Waefeso 5:28
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
Waefeso 5:29
π« Kumpenda mke ni agizo kutoka kwa Mungu
π« Usipoonesha upendo kwake watakuja wanaojua kupenda utashangaa mchumba kakuacha .
π« Furaha ya mke hapa duniani ni kupendwa , ukimwonyesha upendo atakuona mpya kila saa
π« Ukisafiri hizo simu oooh jamani nimekuwa mpweke .ππ
π« Mpende umfurahie naye atakufurahia .
π» 9 Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.
Mhubiri 9:9
π«Inasemekana kwamba wanawake wengi hutoka nje ya ndoa kwasababu wamekosa upendo yaani wananjaa ya kuambiwa maneno matamu ππππ
π« Mwanamke usipomwonyesha unampenda anarubuniwa mapema sana na kwenda kwa wengine
Hali hii ya kutokuonyesha kumpenda mwanamke ni hatari hasa kipindi cha urafiki na Uchumba .
π« Hakuna gharama yoyote kumwambia nakupenda.
Au kumjulia hali ya mchana , au asbhi au kumwambia usiku mwema .
π» 15 Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.
Mithali 5:15
16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?
Mithali 5:16
17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.
Mithali 5:17
18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.
Mithali 5:18
19 Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.
π« Mithali 5:15 _ 19
Inasema mke ni wa kumfurahia na kumfanya yeye wa kipekee sana
Msifu kwa uzuri wake .
π« Mwanamke anahitaji sifa ndugu yangu .
2⃣ Kumheshimu mke
π« mke naye ni binadamu siyo kiumbe cha kunyanyaswa na kumchezea hisia zake .
✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»✍π»
π« Kuna baadhi ya wanaume wanawaona wake zao si kitu kabisa wanawafanyia watakavyo .
π« Baadhi ya vijana wanawasahau kabsa wake zao na kuwatelekeza .
π« Wanasifu wake za wengine kuwa wamependeza kuliko kuwasifia wake zao
π« Wanachati na michepuko muda mwingi sana kuliko kuwakumbuka wake zao hii ni kutokuwaheshimu wake zao .
Wanawaona kama dust bin fulani πππππ
π« Pia hawawashirikishi wake zao katika kazi zao wanafanya kimya kimya , hii ni kutokujua thamani ya mke .
π» 7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
1 Petro 3:7
π« Ukimdharau mke wako uliyepewa na Mungu huwezi kufanikiwa hata sala zako hazijibiwi .πππ
π« Kukikosekana mahusiano mazuri kati ya mume na mke Mungu haibariki hiyo familia kila siku kilio tu .
π« Hata kwa wachumba ikitokea mmoja hamjali mwenzake amemfanya kuwa wa ziada tu huo Uchumba nawaambia hauwezi kudumu lazima utakuwa na migogoro mingi .
π« Msimruhusu shetani kuharibu ndoto za Uchumba wenu kwa kuwafanya wachumba zenu ni ziada
Unatuniwa sms unajibu usiku bila hata samahani .Hizo ni dharau ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂
3⃣ Kujitoa kwa mchumba / mke wake
π« Jitoe atambue kuwa wewe ni wa thamani sana maishani mwake .
π« Jitoe atambue kuwa wewe ni furaha ya moyo wake na unayempunguzia mawazo na kumfariji anapokwazwa na mambo fulani .
π« Jitoe katika mda na katika mambo ambayo unaweza kuyafanya ili atulie kwako daima.
π« Mjali , msikilize , mthamini ajisikie amani kila wakati atamani muwe pamoja ππππ
π« Maneno matamu yatie na asali kama hupendi asali ongeza sukari maneno yako ili akuoende na kujivunia kuwa na wewe .
π» 31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
Waefeso 5:31
π« mwaume lazima uwathamini ndugu wa upande wa mke wako kama unavyowathamini wa upande wako .
π« Hii ndiyo kujitoa kwaajili ya mke wako na yeye kujitoa kwako .
4⃣ Kumlinda mke
π« mwanamke analindwa na upendo bila upendo huwezi kumlinda .Usipoonyesha upendo wa hali ya juu utamfanya amezwe na simba wenye njaa.
π« Usimchafue mke wako mbele za marafiki yako usiyaseme madhaifu yake hadharani yahifadhi mtunze .
π« Siku mojamoja tokeni out na mkewako ππππ
π« msifie basi namna alivyopendeza hata kwa chakula alichokupikia .ππππ
π« Kuwa karibu naye utamlinda na atakuwa mwaminifu kwako
π» 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Waefeso 5:28
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
Waefeso 5:29
π« Mke utamlinda kwa upendo
5⃣ Utoaji
π« Utoaji pia ni sehemu ya kuonyesha upendo kwa mchumba au mke wako .
π« Zawadi ni sehemu ya kumfanya mwanamke ajisikie furaha ya kumjali na kumthamini.
π« Usisubiri mpaka uambiwe zawadi
Mfanyie Surprise πππ
π« Zawadi ni dawa ya upendo pia na inaonyesha mapenzi ya dhati .
6⃣ Kuwa kiongozi wa Kiroho .
π« Baba ndiye kiongozi wa kiroho katika familia .
π« Kijana kabla hujaoa simama kiroho uwe imara kwelikweli .
π» 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Zaburi 1:1
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
Zaburi 1:2
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Zaburi 1:3
π« Kijana ili uwe mume mwema imarika kiroho maana wewe ni kiongozi wa kiroho.
π« Ndoa siyo kwenda kuikalia tu upo vibaya kiroho ikija dhoruba unaweza kukimbia ndoa kwa sababu hujaiva .
π« Iva kiimani kijana uone Mungu atakavyokuletea mke mwema .πππ
7⃣ Kumtunza mke na watoto
π» 8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
1 Timotheo 5:8
π« Hakikisha unatunza mke wako na watoto wako pia .
π« Unataka kuoa unapesa za kuhudumia familia ❓
π« Uanaume ni majukumu lazima mume mwema awe na vision ( maono ) .
8⃣ Kuonya
π« Sifa ya mume mwema ni kuonya na kuhakikisha baadhi ya tabia zisizofaa anazikomesha .
π« Jukumu la mume ni kuonya na kutahadharisha kwa mafundisho ya uzima .
π« Siyo unakuwa na mwanaume anaruhusu tu kila aina ya uongo na kusema yaishe .
π« Mwonye mchumba wako au mkewako asiiache njia ya BWANA.
9⃣ Ukweli
π« Mume mwema ni mkweli hadanganyi .
π« Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye Uchumba au ndoa .
π« Uongo unaharibu kila kitu katika mahusiano
π« Unawatoto sema unawatoto acha kukumbatia uongo .
πMungu akubariki sana
Tutakutana siku nyingine .
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
ππππππππ
Maoni
Chapisha Maoni