URAFIKI πŸ’UCHUMBA na NDOA πŸ‘ͺ

πŸ‘« URAFIKI πŸ’UCHUMBA na NDOA πŸ‘ͺ





SIKU YA TATU

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829/ 0744056901



SAUTI YA MUNGU MINISTRY



 *πŸ’« KUFANYIKA KUWA MKE MWEMA* πŸ‘«




πŸ’» Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana mji wote pia wa watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.

Ruthu 3:11




πŸ’« Kuitwa mke mwema siyo kazi rahisi kama unavyofikiria binti yangu .



πŸ’« Kuitwa mke mwema ni kazi ya Mungu na wazazi .



πŸ’« Wazazi ndyo chanzo kikubwa cha wewe kuitwa mke mwema .


πŸ’« Jinsi walivyokulea ndivyo itakavyokuwa na kwenye ndoa yako binti yangu

Hata kama utabadili mfumo wa kuishi bado kunamfumo wa maisha ya wazazi wako utauishi tu .



πŸ’« Ukiona binti yupo vizuri kitabia na anawajibu watu vizuri jua mama yake ni mstaarabu sana .


Alimlea malezi ya adabu .


πŸ’» Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Mithali 22:6



 πŸ’« Malezi ( makuzi ) yako yanaweza kuamua uwe mke mwema au mke jina tu πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂




πŸ’« Leo Mungu anataka ujifunze jambo zuri binti ambaye bado hujaolewa na wewe uliyeolewa .






πŸ’« Ili uitwe mke mwema au ufanyike kuwa mke mwema lazima msaada wako mkubwa wa kufanyika mke mwema unatokana na Mungu na wazazi .

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Familia ni shule ya kumwandaa binti kuwa mke asiyefaa au kumfanya ataftwe na kila kijana kwasababu amefanyika kuwa  mke mwema .




πŸ’« Wazazi wapo hapo kukufundisha wajibu wako ukiwa ndani ya ndoa ni nini ❓




πŸ’« Tuangalie wajibu wanaotakiwa wazazi wakufundishe ili uwe mke mwema .





1⃣ Kumtii na kumlinda mume


πŸ’» 1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

1 Petro 3:1

2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.

1 Petro 3:2




πŸ’« Ukiona binti anapiganiwa na kila kijana anataka amuoe ujue kafundishwa utii na ndyo maana anavutia wanaume wengi wanamhitaji wamuoe.Mwenendo aliofundishwa na wazazi ni mzuri mpaka majirani wanaona wivu .

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’» 22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

Waefeso 5:22

23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

Waefeso 5:23

24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Waefeso 5:24





πŸ’« Kazi ya mama ni katika familia ni kumfundisha binti utii na utii huu uwe ndani ya Kristo ( neno la Mungu ).




πŸ’« Binti anaiga kutoka kwa mama yake , kama mama hamtii mumewe atawaharibia binti zake .

πŸ’« Ndiyo maana mama akizaa binti mwenye utii utasikia binti anamwambia

Oooh mama jamani mbona humtii baba πŸ™†πŸ»‍♂

Binti huyo ameteuliwa na Mungu kuwa mke mwema .




πŸ’« Binti yangu mwanaume hakoromewi hata kama ni mchumba ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻





2⃣ Kumthamini na Kumhudumia mume

πŸ’« Ili binti uitwe mke mwema lazima ujue thamani ya huyo uliyenaye maishani mwako



 πŸ’« Yapo mengi ya kumkatisha tamaa au kumfanya achoke kama vile wingi wa kazi  , au kakwazwa huko kazini .


Wewe ndiye wa kumfariji na kumpa pole

Mthamini , amechoka mwekee maji bafuni akaoge siyo mpaka aseme .

Mchemshie chai au mletee juisi kama unafriji kwako na kama huna mletee maji anywe .



πŸ’« Hii ndiyo maana ya kumthamini na kumhudumia mume ambayo binti hujifunza kutoka kwa mama zao .




πŸ’» 2 Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai;

Wimbo Ulio Bora 1:2




 πŸ’« Mume anatoka kazini hata busu hakuna unafikiri unamthamini kweli πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂



πŸ’» 5 Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.

Wimbo Ulio Bora 2:5



πŸ’« Baba anatoka kazini mama anampokea kwa shangwe na furaha .

Na kumwambia poleee na uchovu mume wangu


πŸ’« Haya yote binti ambaye anataka kuwa mke mwema huiga kwa mama yake .




πŸ’» 7 Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila.

Wimbo Ulio Bora 4:7




πŸ’« Mke mtii hachakai kwa mumewe kila siku atakuwa mzuri tu .



3⃣ Kumsaidia mume baadhi ya majukumu .


πŸ’« Baadhi ya majukumu pia mke unatakiwa kumsaidia mume wako




πŸ’» 1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Mithali 14:1




πŸ’« Wamekuja wageni nyumbani siyo lazima wakae kuongea na mumeo tu





πŸ’« Jukumu la kukaa na wageni wa upande wa mume siyo la mume tu nawewe mke unahusika kwa sehemu kubwa sana.





πŸ’« Unaona baadhi ya miradi ya mume wako inataka kufa na wewe upo msaidie kuisimamia .




πŸ’» 22 Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Mithali 18:22




 πŸ’« Sifa ya mke mwema ni kumsaidia mume baadhi ya majukumu .



πŸ’» Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Mwanzo 2:18




4⃣ Kujiheshimu


πŸ’« Ukijiheshimu na kujitambua utalinda heshima ya mumeo


πŸ’« Siyo mume anatoka nawewe unaenda kuzurura na kutafuta umbeya kwa majirani .

Huko ni kumwaibisha mume wako .



πŸ’« Mwanamke hutakiwi kufanya mambo yasiyopendeza mbele za Mungu na katika jamii inayokuzunguka .




πŸ’» 11 Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.

1 Timotheo 3:11




πŸ’«Kuwa mwaminifu katika Uchumba kunakufanya uwe mwaminifu katika ndoa yako asilimia mia moja ( 100%) .




πŸ’« Usisubiri ujiheshimu baada ya kuolewa , jiheshimu kabla ya ndoa ili uwe mke mwema , mwaminifu anayejitambua .


Ukifanya hivo huwezi kumwaibisha mumeo kwa majirani , hawawezi kunung'unika

Oooh jamani fulani kaoa mke gani huyu akiondoka analeta wanaume πŸ™†πŸ»‍♂πŸ™†πŸ»‍♂

Mambo ya aibu .



πŸ’« Mume wako ameenda kazini endelea kumwombea na kumkumbuka hata kumtumia sms inafaa sana .



πŸ’« Hii siyo kwa mume tu hata kwa mchumba pia




5⃣ Kumpenda mume


Mke mwema lazima ampende mume wake




πŸ’« kama nilivyosema awali kuwa familia ni shule ya maadili basi binti hujifunza namna ya kumpenda mume kutoka kwa mama yake .




πŸ’« Mama akiwa anamnyanyasa baba na kumjibu kwa ukali anawafundisha binti zake kutokuwapenda waume zao .




πŸ’» 4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;

Tito 2:4




 πŸ’« Lazima ujue kupenda ili uitwe mke mwema



πŸ’« Uwapende na ndugu za mume wako pia .



πŸ’« Haya yote binti hujifunza kutoka kwa wazazi



πŸ’» 3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;
Tito 2:3

4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;

Tito 2:4



6⃣ Kufanya kazi za nyumbani


πŸ’» 3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;
Tito 2:3

4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;

Tito 2:4

5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.

Tito 2:5


✍🏻 Nanukuu mstari wa tano hapo juu unasema

" KUFANYA KAZI NYUMBANI MWAO "



✍🏻 Binti ili uwe mke mwema jua kupika na kufua pia .

πŸ’« Siyo mume anakwambia nahitaji pilau leo unapika pilau liliounguza vitunguu πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂




πŸ’« kunabaadhi ya wazazi hawataki binti zao wapike eti watateseka bila kujua wanawafanya kuwa aibu kwa waume zao .




πŸ’« Hata baadhi ya binti kufua hawajui kwa sababu ya kudekezwa na mama zao
Kazi zote house girl ( binti wa kazi ).



πŸ’« Ili uwe mke mwema  fanya kazi za ndani kama vile kupika

Siyo unapika chakula kibichi πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂


Mfulie mumeo pia ,


Utakuwa mke mwema kwelikweli



πŸ’« Na wazazi wanaodekeza binti zao wasiguse kazi waache tabia hiyo .


Unakuta binti anaolewa hata kutandika kitanda hajui .


Alizoea kutandikiwa na binti wa kazi sasa anasota ndani ya ndoa



 πŸ’« Ndiyo hawa hugombana na waume zao kisa hawataki kuleta house girl





HITIMISHO

Mke mwema anatoka kwa Mungu lakini wazazi ni sehemu kubwa ya kumfanya binti awe mke mwema , unaweza kusema kwamba mke mwema huandaliwa na wazazi wakisaidiwa na Mungu .Malezi yanaweza kuamua binti aitwe mke mwema maana Mungu hamfundishi binti kazi , au kuheshimu watu , hii ni kazi ya wazazi kumwandaa binti yao kuwa mama mzuri katika familia yake .





Mungu akubariki sana


Tukutane siku nyingine



https://peterfrancismasanja.blogspot.com


0744056901

francispeter424@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*