USIJISIFU KWA KUWA MUNGU AMEKUINUA*

*USIJISIFU KWA KUWA MUNGU AMEKUINUA* 



Danieli 4:28-37

[28]Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza.

NEBUKADREZA ALIINULIWA NA MUNGU HADI VIWANGO HIVI
👇👇👇👇👇

[29]Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya *jumba la kifalme katika Babeli.*

ONA MAJIGAMBO YA MFALME
👇👇👇👇👇

[30]Mfalme akanena, akasema, *Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?*
👆👆👆 ETI NILIOUJENGA KWA UWEZO WA NGUVU ZANGU.
UNAPOFANIKIWA USISEME NI NGUVU ZAKO ZIMEKUFANIKISHA. UNAPOWAZA TU HIVYO, UJUE MUNGU ANAKUANGALIA NAYE ANASEMA "NITAKUONYESHA"
👇👇👇👇👇
USIJIFARIJI KWAMBA MUNGU NI MWINGI WA REHEMA, YEYE HAWI RADHI NA WAPUMBAVU
👇👇👇👇👇

[31]Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, *sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema,* Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; *Ufalme huu umeondoka kwako.*
[32] *Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni;*

USISEME NANI ATANIKOROMEA, MUNGU SIO SHEMEJI YAKO;
👇👇👇👇👇
 *utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako,*

KWANINI HAYO YOTE? MUNGU ANATAKA UJUE KITU HIKI
👇👇👇👇👇
 *hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.*

NA MUNGU ANAPOTAMKA HIVYO USIDHANI ITAKUWA MWAKANI  AU KESHO, ANGALIA HAPA
👇👇👇👇👇
[33] *Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza;* alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.

MUNGU ANAWEZA KUUA LAKINI HUYO HUYO ANAHUISHA

[34]Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, *fahamu zangu zikanirudia;*

WEWE ULIJUA WACHAWI TU NDO  WANAWEZA KUKUFANYA MSUKULE?? UMEMSAHAU ALIYEWAUMBA??

ROHO YA MNYAMA IKAMTOKA NEBUKADREZA, AKILI YAKE IKAMRUDIA, ANGALIA ALICHOKIFANYA
👇👇👇👇
 *nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;*

HUWEZI KUMPANGIA MUNGU CHA KUFANYA JUU YA MAISHA YAKO, WALA HUWEZI KUMUULIZA ANAFANYA NINI ISIPOKUWA UNA WAJIBU WA KUMKUMBUSHA TU MAANA YEYE ANAJUA CHA KUFANYA.

[35]na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, *naye hufanya kama atakavyo,* katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; *wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?*

NEBUKADREZA AKATAMBUA KUWA FAHARI ILE HAIKUWA KWA AJILI YA UTUKUFU WAKE ILA KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU MWENYEWE.
👇👇👇👇👇

[36]Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.

UKIJISHUSHA NA KUNYENYEKEA, MUNGU SIO DHALIMU LAZIMA ATAKUINUA TU.

MWABUDU MUNGU NA UMHESHIMU MAANA NJIA ZAKE NI ZA ADILI

[37]Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.


JE, UNASUBIRI KIBOKO CHA MUNGU  NDIPO UACHANE NA KIBURI? UNANGOJA KULISHWA NYASI NDIPO UJUE MUNGU YUKO JUU ZAIDI YAKO??

KAMUULIZE NEBUKADREZA KAMA HIYO MIAKA SABA YA KULA MAJAN KAMA ILIKUWA MICHACHE.


 *MSIFU MUNGU KWA KUWA AMEKUINUA.*

UBARIKIWE NA BWANA.

nabiisamweli@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*