USIOE AU KUOLEWA NA ASIYEOKOKA 💒

💫 USIOE AU KUOLEWA NA ASIYEOKOKA 💒


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


SAUTI YA MUNGU MINISTRY





🔥 Namwomba Mungu hili somo likufikie wewe kijana ambaye hujaoa au hujaolewa bado .



✍🏻 Kuna madhara makubwa kiroho kufunga ndoa na mtu ambaye hajaokoka au ameokoka lakini bado anatambika .


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



💫 Mtu yeyote aliye kinyume na Kristo huyo hakufai .



💻 15 Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake.

Kutoka 34:15

✍🏻 Mungu anaonya juu ya kufunga ndoa na asiyemwamini.


💫 Unapofunga ndoa na mtu asiyeokoka ujue kuna kutiwa roho za kuabudu miungu ya ukoo wa huyo mtu .



💫 Kuna shida kubwa hapa hasa kwa binti zetu wanaoolewa na wasioamini kuwa Yesu Kristo ni Bwana na mwokozi wa maisha yao .



 💫 Ukimwuliza binti anasema amempenda atamwokokesha huyo bwana wake matokeo yake akishaolewa anapelekwa vijijini anakutana na matambiko na chale nyingi sana .
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



 💫 Binti wengi wamemwacha Yesu kwa kuolewa na wapinga Kristo .



💻 16 Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.

Kutoka 34:16



💫 Biblia inasema , wakafanya uzinzi na miungu yao ,



✍🏻 Uzinzi wa kiroho



✍🏻 Kufanya uzinzi na miungu maana yake ni kumwacha Mungu na kugeukia kuabudu mizimu ya ukoo .


Binti wengi wakiolewa wanageuzwa kuabudu mizimu ya ukoo wa waume zao .



💫 Mungu aliliona hilo akakataza kabisa kwa mkristo kuolewa na mtu asiyeokoka .


✍🏻 Alijua kabisa kwamba ukiolewa na asiyemwamini Yesu umeenda kufa kiroho .



 💻 3 binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake.

Kumbukumbu la Torati 7:3




💫 Mungu anaonya watu wake juu ya kufanya agano na adui



 ✍🏻 Tunamwangalia adui kwa upande wa kutokuokoka ,

Mtu asiyemkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake ni adui wa Mungu .



 💫 Ukiolewa na adui wa Mungu huwezi kumtumikia Mungu .




💻 4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.

Kumbukumbu la Torati 7:4




💫 Ukiolewa na asiyemkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake atahakikisha unamwacha Yesu.

Atakukengeusha ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



💫 Suala la ndoa kwa wewe uliyeokoka zingatia kwanza wokovu maana ni jambo la msingi kuliko vyote hapa duniani .


� Suala la wokovu ni la milele , kwahiyo zingatia sana na uhakikishe huyo mtu unayemtarajia awe ameokoka  asije akakuua kiroho .



💻 1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

1 Wafalme 11:1

2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.

1 Wafalme 11:2



💫 Leo binti zetu wamekuwa na roho kama ya mfalme Selemani aliyewapenda wanawake ambao hawamchi Mungu wakamwangusha akatumikia miungu mingine .


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻




 💫 Binti zetu wanazimia kimapenzi kwa wanaume wasiookoka wakidai wanapendwa .Hawajali kufa kiroho

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻




✍🏻 Tuone mwisho wa mfalme Selemani alimaliza vipi baada ya kuoa wasiomcha Mungu

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



 💻 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.

1 Wafalme 11:3



 💫 Mfalme Suleiman alipooa wanawake ambao si wacha Mungu kilichofanyika wakamgeuza moyo wake

✍🏻 Walimgeuza akamsahau Mungu


💫 Baada ya kumsahau Mungu akageukia miungu mingine .


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



💻 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.

1 Wafalme 11:4




💫 Suleiman alipogeuzwa moyo wake akakosa ukamilifu mbele za Mungu yaani akakengeuka .Akawa mdhambi


✍🏻 Vivyo hivyo na vijana waliookoka wakifanya agano na wasiookoka hukengeuka .



💻 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

1 Wafalme 11:5

6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

1 Wafalme 11:6

7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

1 Wafalme 11:7

8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.

1 Wafalme 11:8



💫 Hatimaye tunamwona Suleiman amekubali kutumikia miungu mingine kwa kumwabudu mungu mke




💫 Hii hutokea sana kwa binti zetu wanapoamua kuolewa na wasiookoka

Hugeuka na kuitumikia miungu ya waume zao .

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



 💫 Alipogeukia miungu mingine Mungu akamkasirikia sana



💫 Hata kwa vijana naomba muelewe kuwa unapoolewa na asiyeokoka ukakubali kuitumikia miungu yake ukiona ndoa imekuwa ya mateso ujue Mungu anakuonya yaani anatoa fundisho kwako inawezekana hukusikiliza ushauri wa wazazi na watumishi wake .



💻 9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,

1 Wafalme 11:9

10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.

1 Wafalme 11:10

11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.

1 Wafalme 11:11



 💫 Kupitia kuoa Suleiman alimkosea Mungu na kupewa adhabu .



🖊 Msikilize Mungu katika kumpata mwenzi wa ndoa kama hajaokoka sitisha kabisa maana atairarua ndoa yako ukiona .

✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



 💫 Mungu akikuonya usifanye kitu acha usilazimishe kabisa .



💻 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

2 Wakorintho 6:14



 💫 Mungu aliliona hili suala na kuolewa au kuoa asiyeokoka akakataza maana anajua kuwa utatiwa roho ya kumsahau yeye na kutumikia miungu mingine



💫 Kwahiyo mambo ya kuoa mtu asiyeokoka au kuolewa na mtu hajaokoka ni chukizo mbele za Mungu .



Mungu akubariki sana

Nakutakia baraka za Mungu ziwe na wewe siku zote





💒💒💒💒💒💒💒

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*