USIPENDE KUJITENGA NA KUSANYIKO LA BWANA
*USIPENDE KUJITENGA NA KUSANYIKO LA BWANA
Pastor Sponga
Bahi _Dodoma
JESUS CO_WORKERS MINISTRY
1 Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe; Hushindana na kila shauri jema.
Mithali 18 :1
27 Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.
Zaburi 73 :27
28 Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.
Zaburi 73 :27
24 Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni Bwana, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa.
Mambo ya Walawi 20 :24
25 Kwa ajili ya hayo mtapambanua kati ya mnyama aliye safi na mnyama aliye najisi, na kati ya ndege aliye tohara na ndege aliye najisi; nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa machukizo kwa njia ya mnyama, au kwa njia ya ndege, au kwa njia ya kitu cho chote ambacho nchi imejaa nacho, niliowatenga nanyi kuwa ni najisi.
Mambo ya Walawi 20 :25
2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
Matendo ya Mitume 13 :2
3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.
Matendo ya Mitume 13 :3
Mtu yeyote anayejitenga na kusanyiko la Mungu nu mbinafsi
Mfano , Lutu alipojitenga na Ibrahim akaenda Sodoma na Gomora hiyo miji iliangamizwa .
Usijitenge na kanisa kwa sababu ya mgogiro unaoendelea , simama imara.
Ni Mungu pekee ndye awezaye kututenga na unajisi wa kila aina
Pia kumbuka watu hujitenga kwa sababu ya dhambi zao .
Watu hujitenga kwa sababu zifuatazo:
1. Kuepuka madhara
2.Kwa sababu ya nadhiri
Hesabu 6:5
Tunajitenga na kusanyiko ili kurudisha uhusiano wetu na Mungu.
3.Kujitenga na uovu
Mithali 14:16
Mithali 16:17
Mungu anaruhusu ujitenge na uovu .
Usijitenge na kusanyiko kwa sababu ya chuki , au kiburi utaangamia au utapotea.
Mungu akubariki sana
Maoni
Chapisha Maoni