UTAISHIJE NA MCHUMBA WAKO ILI MFIKIE MALENGO YENU πŸ’’*

πŸ’« UTAISHIJE NA MCHUMBA WAKO ILI MFIKIE MALENGO YENU πŸ’’*



SIKU YA SITA


Mwl.Peter Francis Masanja


0679392829



SAUTI YA MUNGU MINISTRY


Karibu tuendelee


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
 Tujifunze namna ya kuyapalilia  Uchumba wenu usiote magugu




πŸ’« Watu huuliza je nifanyeje ili tusiachane na mchumba Wangu ?



 ✍🏻 Sikiliza kwa makini sana tega sikio lako

🀣✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’« Uchumba umeshikiliwa na mawasiliano kati ya wawili wanaopendana .


πŸ’« Wataalamu wa Lugha husema hivi kuna kanuni tatu katika mazungumzo pale mtu anapohitaji ka kumjibu mtu .




πŸ’« Pale mtu unapopokea ujumbe kutoka kwa mtu wako unaweza ukachagua jambo moja kati ya haya matatu .



1⃣ Kujibu hapohapo


2⃣ Kutokujibu


3⃣Kuchelewa kujibu




πŸ’« Katika haya mambo matatu mawili huweza kubomoa mahusiano na kuleta kutokuaminiana



πŸ’« Mambo haya mambo matatu yanapima maswali haya matatu. ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻




1⃣ Je ananithamini ❓


2⃣ Je ananijali ❓


3⃣ Je yupo tayari kunisikiliza ❓



 πŸ’« maswali hayo matatu pia tunakuja kuyapima kutoka kwenye maandiko matakatifu kama ifuatavyo ✍🏻✍🏻✍🏻



πŸ’» Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

1 Wakorintho 13:8




πŸ’« Kama Mungu amekupa huyo uliye naye awe wako tambua kuwa upendo haupungui .



πŸ’« Pale upendo unapopungua utaona kila mtu yupo busy na mambo yake sasa kama mwingine aliingia mzima mzima atabaki anaumia na kuteseka huku mwingine anaona kawaida tu .



πŸ’« Ili mahusiano yenu myalinde hakikisheni mnamruhusu Mungu aachilie upendo usiopungua ndani yenu .



πŸ’« Katika eneo la mawasiliano hasa kwa vijana hawa wamejikuta mmoja kasafiri kaenda mkoa mwingine kikazi na ni wachumba .


✍🏻 Makosa makubwa wanayoyafanya vijana ni kutokujali simu za watu wao siku nzima , halafu inafika usiku wanaanza kusema ooooh baby kashakuwa mgomvi siku hizi ananigombea hata hajanioa .


πŸ’« Tambua kuwa kama zamani alikuwa anakutafta unamjibu mbona sasa umekuwa mzito ❓

Hapo ni kujiandalia mazingira ya kutokufikia malengo yenu .




πŸ’« Usidhubutu kumsumbua mtu akupendaye kwa kumsusia kana kwamba upo wewe tu duniani


Nani kasema akitoka kwako hatapata wa kumjali ❓


πŸ’« Hakikisha unamjali na ukiwa na kazi mwambie mapema aelewe kuwa mda fulani utakuwa busy ,


πŸ’« Vinginevyo utasema umelaaniwa kumbe unajiroga mwenyewe




 2⃣ Utani kupita kiasi


✍🏻 Utani ule mbaya wa kuleteana msongo wa mawazo na mashaka na mmoja wapo kuingiwa na roho ya kukata tamaa .


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻




πŸ’« Mizaha iliyopita kiasi inaweza ikawa moto utakaoteketeza mahusiano yenu mkaachana kabisa




πŸ’« Utasikia anawaambia marafiki zake alikuwa anakujaribu kama unampenda .


πŸ’« Nani kasema uchumba ni sehemu ya majaribio ❓



πŸ’« Siku mlipoamua mkisema mimi na wewe tuwe wachumba mkakubaliana ilikuwa ni siku ya kuacha mizaha na utoto na kuleteana majaribio .




πŸ’« Mtu mpaka anadhubutu kumkalia kimya mchumba wake siku nzima au siku tatu hakuna SMS wala kupokea simu hakuna akidai anamjaribu mchumba wake aone kama anapendwa

Huu ni utoto na kutokukomaa kiroho maana hiyo hujaokoka ✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻




πŸ’« mwingine anadiriki kusingizia magonjwa hatari et nimeathirika

Mwingine anasema

🎀 mimi na wewe basi tena


Eti anajaribu utafanyaje


Mwingine anakwambia ameoa au ameolewa


Yaani ukiona utani huu ujue huna mtu hapo bado hajaokoka



✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻




 πŸ’« Hakuna Uchumba ulioamriwa na Mungu halafu kila siku mtu akuletee mizaha mpaka siku yako inaharibika unakuwa na msongo wa mawazo .


🎀 Biblia imebaini kabisa ikasema watu wa mizaha ni hatari sana katika maisha yako ya kiroho wakimbie



πŸ’» 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Zaburi 1:1

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

Zaburi 1:2

3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Zaburi 1:3



πŸ’« Huwezi kupata mda mzuri wa kumtumikia Mungu kama unamchumba anakuletea mizaha kila wakati anakukwaza

πŸ’«Anavunja uhusiano wako na Mungu .



πŸ’« Na vijana wengi wanapunguza kazi ya kumtumikia Mungu wakijiingiza kwenye mahusiano na watu ambao si sahihi , saa zote makwazo .


Mara simu isijibiwe , mara hajisikii kuongea na wewe  , mara azime simu ,

Jiongeze usisubiri Mungu akupigie kengele .

πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂




πŸ’« Kwahiyo Yote haya ukimwuliza eti anakutania huyo hakufai


Na vijana mlimo humu hizo tabia zivueni halafu mtaona mahusiano yenu yanasitawi kila siku .




πŸ’« Hatari iliyopo ni kwamba madhara ya kutiwa presha na mtu ni makubwa sana


πŸ’« Uchumba wa mizaha mingi hupunguza uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo




 πŸ’« Uchumba wa makwazo mengi hupelekea mishipa ya moyo kutanuka na kuja kusababisha magonjwa ya moyo uzeeni .




πŸ’« Uchumba wa makwazo mengi huleta ugonjwa wa hasira kupita kiasi

Yaani mchumba wako  anakusababishia hasira unajikuta huwezi kujizuia kwa kila mtu akikuchokoza unampandia juu .




πŸ’« Ulishawahi kufanya utafiti kwanini walimu wengi kuna siku huchapa sana wanafunzi ❓


πŸ’« Utakuta wamekorofishana na wake zao sasa wewe mwanafunzi kosea uone atakavyokupiga bakora .

πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂πŸƒπŸ»‍♂




 πŸ’« Siyo kila kijana unayemwona anakujibu vibaya anadharau , wengine wameathiriwa na wachumba zao wakawa na hasira sugu 🀣🀣🀣🀣🀣🀣



✍🏻 Vijana naomba niishie hapo kwa leo


HITIMISHO


 Zingatia yafuatayo katika Uchumba wako ili kufikia malengo




1⃣ Epuka kumsusia mchumba wako

Kama utakuwa busy toa taarifa .



2⃣ Epuka mizaha na utani usio wa maana



3⃣ Acha majaribio , Uchumba siyo majaribio

Unaonja uone kama wapendwa utaambulia kubomoa




Ni mimi


Mwl.Peter Francis Masanja

0744056901


https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*